Trending News>>

SIMULIZI :: Jini Mahabati Sehemu ya Kumi na Sita (Kwa wenye miaka 18+)




SIMULIZI : JINI MAHABATI
SEHEMU YA KUMI NA SITA
MTUNZI: MANYAMASON
AGE: 18+
ILIPOISHIA
Kwa hiyo mzee huyu alikuwa na uwezo wa kuwaona majini hapo zamani lakini sasa hivi alishangaa uwezo huo hakuwa nao tena.Lakini majini yalikuwa yanamuona hivyo kufanya vita hiyo kuwa ngumu sana.Ikumbukwe binadamu wa kawaida hawezi kuwaona viumbe hawa mpaka awe na utaalamu maalumu.Ingawa mafundisho ya vitabu vya dini vinaeleza kuwa wanyama kama mbwa, paka na punda wanaweza kuwaona majni na ndio maana ukisikia mbwa abwekabila sababu basii jua kamwona jini.Basi wakati kikao cha majini kikiendelea. Mzee Said na yeye mda huo huo akamua kumuita jinni anayemtatiza mwanaye kwa***
SONGA NAYO.
Basi wakati kikaao cha majini kinaendelea mzee Said na yeye akawa mda huo huo anamwita jini makata ili amuonye juu ya mchezo wanaomfanyia wa kumdhuru mwanye. Akawa anataja majina mbali mbali mara nyingi. Akaanza na jina la salsal, salsal akalitaja mara 1000, kisha akataja, akamash, akamash mara 1000 na akamalizia na jina la Laash, laash mara 1000. Alikuwa akitamka majina hayo huku akipuliza ubani maka na majani ya mnazi wa kipemba. Basi ukatokea moshi mweusi mbele yake na kwa tabasamu zito mzee huyo akaanza kuliagiza jini hilo kitu akitakacho.
“Najua nimekutorosha kwenye kikao chenu ila mimi sitaki ugomvi na wewe bali nakuagiza ushindi mumuache mwanangu aendelea na masomo alisema mzee Said baba mzazi wa Tariq. Ghfla ule moshi mweusi ukazidi kuwa mkubwa na wenye harufu kali. Kinyume na matarajio ya mzee huyo kuwa ataongea na jini Makata kirahisi hali ilikuwa tofauti kabisa manaa ule moshi mweusi ukaanza kumpalia mzee huyo kabla ya kusikika sauti ya ajabu kutoka ndani ya Moshi ule “Ni ngumu ni ngumu sana, vita hii ni ngumu sana na kamwe hutoweza kushinda” sauti hiyo ilitoka kwa mtindo wa mwangwi.
Mzee Said baba mzazi wa Tariq akaanza kupaliwa na moshi ule. Alihisi kitu kumkaba kooni kabla ya kupiga kelele za kuomba msaada. Kelele zile zilifika kwa mke wake na mwanaye. Wote kwa pamoja walikuja kumpa msaada. Tariq naye akajaribu kuonesha ujuzi wake kwa kusoMa dua yakufukuza jini. Jini Makata likamtoka mzee yule lakini hakuweza kuogea kitu wakati ule.
Alikuwa ni kama bubu au kiziwi hasiyeelewa nini kinaendelea. “Lakini mme wangu si unajua sharia za kuita majni kwanza uwe katika hali safi na pia usiwe muoga” alihoji mkewe huku akimtingisha tingisha kujaribu kumshtua lakini wapi mzee huo alikuwa kimya kama zezeta tu. Hali haikuwa shwari kwa kweli na wote kwa pamoja walichanganyikiwa. Tariq alionesha kupata afueni lakini hali ya mzee ilikuwa ni ya kusikitisha zaidi.
************************************ 
Radhia yeye alifika salama nyumbani kwao akawakuta wazazi wake kama alivyowaacha. “Karibu sana mwanangu, tulikuwa tumekumiss sana tukasema hata tukuandalie kuku kwa ajili ya usiku wa leo” ilikuwa ni sauti ya mama yake Radhia ikitoa ukaribisho na hapo walikuwa mezani wakijipatia chakula cha usiku. “Asante sana mama yangu, nimefurahi sana kuwakuta wote mpo salama” alijibu Radhia huku akilivuta na kulila paja la kuku lilokuwa limepikwa kwa ufundi mkubwa. “Nimeona siku hizi kuna mabadiliko na hata hamjanitambulisha” aliuliza Radhia. “Yeah huyo kijana uliyemwona anaitwa Shaban anatokea matombo huko Morogoro yupo hapa kwa ajili ya kutusaidi kazi za hapa na pale” alifafanua baba yake. “Ni vizuri sana japo sioni kama kuna kazi nyingi mpaka mkawa na mfanyakzi wa kike na kiume” aliponda Radhia. “Yeah mwanangu hata hivyo kesho kutwa ataondoka atarudi kwao maana kuna matataizo ya kifamilia” alisema baba yake huku wakiendelea kufurahi chakula cha usiku chenye mapocho mapocho kibao. Kimoyo moyo Radhia akawa anajisemea hakuna cha matatizo ya kifamilia wala nini ni kwamba wanamuondoa kwa sababu yeye amekuja hivyo wanaogopa majanga yanaweza kutokea.
Basi waliendelea kula na walipomaliza waliendelea kupiga stori za hapa na pale. Radhia siku hiyo alikuwa kinara wa stori hasa za chuoni kwao. “Ujitahidi sana kusoma mwanangu na degree ya pili tutakupeleka nje ya nchi alisema baba yake. Stori zikaendelea lakini mama yake kila alipomwangali Radhia aligundua kuwa kulikuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye mwili wa biti huyo. Radhia huyu hakuwa yule aliyemzoea. Huyu alikuwa amezidi utamu, anang’aa kama mbalamwezi ya asubuhi. “Inaelekea huko Tanga pamekukubali sana mwanangu maana naona umezidi kupendeza tu” alijikuta akisema maneno hayo mama yake mzazi kabla ya baba yake kuunga mkono hoja hiyo “Exactly mwanangu Radhia amezidi kuwa mrembo alisema baba yake.
Usiku ukawa mkubwa na baba mtu akawa wa kwanza kuaga na kwenda kulala. Kama unavyojua kazi ya mama ni kuhakikisha anachunga biashara yake na biashara yake kubwa ilikuwa ni mme wake hivyo isingeacha kumuacha mumewe akalale alafu yeye aendelee kung’aa sharubu hapo sebuleni. Radhia akabaki pale sebuleni na mfanyakazi wa kike wakawa wanapiga stori za hapa na pale. Mara Shaban naye akaja wakaendelea kuangalia tamthiliya na kupiga story za hapa na pale.Uzuri wa Shabani naye alikuwa ni muongeaji tena ule uongeaji wa kufurahisha tu. “kumbe dada Radhia ndo mzuri hivi kila siku mama alikuwa akilitaja jina lako nikawa nahisi kama kila siku tupo nawe” alisema Shaban.
“Mimi wa kawaida bhana sio hata mzuri, wazuri ni kina Wema na Zari” alijitetea Radhia. “Hamna wale sio wazuri bali ni masupa star. Wewe unafikiri wana uzuri wowote basi tu ni kwa sababu wanaonekana kwenye luninga sana na headlines zao ndo zinawapandisha chati. Wakati story zikiendelea hali ya Radhia ikaanza kubadilika. Akaanza kujihisi tena ule mshawasha wake wa mapenzi ukianza kumpanda.
“Mungu wangu hiki ni nini tena alijisemea Radhia huku akitamani hata kupitisha mikono yake huko kunako na kujaribu kujikuna. Hali ilikuwa imebadilika ghafla na alitamani kuondoka hapo sebuleni na kukimbilia huko chumbani kwake lakini akaona bado haitakuwa suluhisho la tatizo hilo. Sehemu zake za siri zikazidi kuumuka huku ule muwasho ukizidi kumkolea. Alimwangalia Shabani kwa macho ya matamanio sana na akatamani hata amwibe na kwenda kulala naye chumbani kwake. Stori zilizokuwa zikipigwa zikawa zinaingilia huku na kutokea kule. Hali ilipozidi kuwa mbaya Radhia alijinyanyua pale sebuleni na kukimbilia chumbani kwake. Kuondoka kwake kuliwashangaza waliobaki maana aliondoka utazani ameshikwa na tumbo la kuhara.
Radhia akaenda kujibwaga pale kitandani huku akihisi mapigo yake ya moyo yanongezeka. Mshawasha wa huba ukazidi kumsumbua akajikuta anaanza kupunguza nguo mpaka akabaki uchi wa mnyama. Yaani mzimu wa jini Barike ulivyoambiwa uongeze spidi kweli uliongeza spidi maana Radhia alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa. Akaenda kwenye kioo na kujiangalia jinsi alivyo. Yeye mwenyewe alijishangaaa maana alijona amezidi kuwa mzuri. Mara matiti yake yakaanza kumcheza cheza huku yakisimama na kutuna. Akaanza kujipapasa mwenyewe huku akiyanyanyua nyua na kuyapandisha juu. “Uuuuuuuuuuuuh , uuuuuuhhhh alianza kulalamika binti huyo mara baada ya kuhisi kama ute ute mzito ulikuwa ukishuka kutoka kwenye viungo vyake vya sehemu ya siri.
Sio huko chini sio kwenye matiti kila mahali mshawasha na muwasho uliongezeka. Akajikuta anaanza kupiga piga miguu maana hamu ya kufanya mapenzi ilizidi mara mia ya ile aliyokuwa akiisikia.
****ITAENDELEA***

No comments:

Powered by Blogger.