Trending News>>

Siku 39 zimtolewa Kodi Ya Majengo Iwe Imelipwa Mwanza

Kamishna Mkuu wa TRA nchini,Charles Kichere, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani

Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia  Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani na kutozwa faini.

Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.

“Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili  na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere.

Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.

Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela.

No comments:

Powered by Blogger.