Samatta apiga bao, KRC Genk ikishinda 3 - 0
Hilo linakuwa bao lake la 20 Samatta katika mechi 59 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC. Na kwa ushindi huo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B katika kuwania tiketi ya Europa League 2018 ikifikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 10.
Samatta alifunga lake dakika ya 55 jana akimalizia pasi ya beki wa Jamhuri ya Czech, Jakub Brabec, baada ya kiungo mkongwe Mbelgiji mwenye umri wa miaka 36 Thomas Buffel kufunga la kwanza dakika ya 32 na kiungo Mholanzi, Jean-Paul Boetius kufunga la pili dakika ya 43.
Kati ya mechi hizo 59, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 41 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 37 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 27 msimu huu.
Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 19, 14 amefunga msimu huu na tano msimu uliopita.
Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa: Ryan, Uronen, Colley/Janssens dk84, Brabec, Castagne, Berge, Malinovskyi/Heynen dk70, Writers, Boetius/Naranjo dk76, Buffalo na Samatta.
No comments:
Post a Comment