Sababu 5 kwanini mvuto wa mechi ya Arsenal na Manchestet unapungua
Siku ya Jumapili kuna pambano la kukata na shoka katika
uwanja wa Arsenal Emirates, Arsenal watakuwa nyumbani kuwakaribisha
Manchester United. Takwimu zinaonesha upinzani kati ya Arsenal na
Manchester United unaoungua siku hadi siku huku zifuatazo zinaonekana
kuwa sababu za upinzani huo kupungua.
1.Pesa za Kirusi. Mwaka 2003 tajiri wa Kirusi Roman Abromovich
aliinunua rasmi klabu ya Chelsea, kabla ya hapo Chelsea walikuwa
wakionekana wakawaida sana na United na Arsenal walikuwa watawala lakini
pesa za Abromovich zimeleta mapinduzi ya soka na Chelsea kuonekana
mpinzani sana hali iliyopelekea mechi kati ya Arsenal na United siku
hizi inaonekana sio kali kama Chelsea na United.
2.Pesa za kiarabu. Baada ya Mrusi kuleta pesa zake Epl, baadae
waarabu walimjibu na kuwekeza pesa zao katika klabu ya Manchester City,
City nao kama ilivyo kwa Chelsea wakaanza kuleta upinzani mkubwa kwenye
ligi kiasi cha kuanza kukaa juu ya Arsenal na Manchester United, hii
kidogo ikaanza zipoteza Arsenal na United kwenye mbio za ubingwa na hata
mvuto wao ukapungua.
3.Kustaafu kwa Alex Ferguson. Ni kweli vita ya Mourinho na Wenger
inaifanya mechi hii kuwa na mvuto lakini uwepo wa Alex Ferguson kwenye
benchi la Manchester United uliifanya mechi hii kuwa na mvuto zaidi,
Ferguson alikuwa mshindani haswa na asiyependa kufungwa na timu za juu
na hii iliifanya mechi hii kuwa ngumu sana na yenye mvuto.
4.Sio tena wapinzani wa makombe. Zamani kabla ya mwaka 2007 klabu
hizi mbili zilikuwa zikipigana vikumbo kileleni, mara nyingi mechi zao
huwa zinatoa taswira ya ubingwa kama sio wa FA baasi wa EPL lakini sasa
kama mechi hii ya Jumapili Arsenal yuko nafasi ya 6 na United yuko
nafasi ya 7 haina athari yoyote katika mbio za ubingwa.
5.Kuondoka kwa Patrick Viera na Roy Keane. Viungo hawa wawili
walikuwa wakifanya mechi hii kuwa na mvuto, vyombo vya habari vingi
vilikuwa vinaisubiri mechi hii ili kuona Roy Keane na Patrick Viera
watafanya kitu gani, baada ya wawili hao kuondoka kwa sasa timu hizi
zinakosa wachezaji wenye kuifanya mechi hii kuonekana ya upinzani mkubwa
kama zamani kipindi wapo
No comments:
Post a Comment