Ommy afungukia 'ubize' wa mastaa
Msanii Omary Nyembo 'Ommy
Dimpoz' amefunguka na kuweka wazi kwamba mastaa wengi wanapenda kujipa u
- bize wasiokuwa nao kwa sababu tayari wameshakuwa na majina makubwa
mjini.
Ommy Dimpoz
Ommy
amefunguka hayo kwenye 'story' tatu ya Planet Bongo ndani ya East
Africa radio na kusema kuwa wasanii mkubwa wanapotafutwa na msanii mdogo
kwa ajili ya kazi mara nyingi hujivalisha u-bize wasiokuwa nao kwa
sababu tu tayari ni staa.
"Msanii mkubwa ni mkubwa
tuu, kuna wakati unaweza kumpigia simu akakwambia nipo bize kuna ishu
naifanya kumbe miyeyusho tu, labda kalala zake anachati. Wasanii wengi
wakubwa wanajipa ubize wasiokuwa nao. Kusema suala la kufanya kazi na
msanii mdogo mi nadhani unaweza kufanya tuu kinachomata zaidi ni kazi
nzuri." - Ommy alifunguka.
No comments:
Post a Comment