NEWS:Fedha za mfuko wa jimbo zaibua mjadala mzito Bungeni
Mjadala
mkubwa umetokea Bungeni mjini Dodoma mapema hii leo mara baada ya
wabunge wa viti maalumu kuhoji uhalali wa kutokuwepo kwenye mgawo wa
fedha za mfuko wa jimbo.
Mjadala
huo umeibuka mara baada ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,
Suleiman Jafo kusema kuwa fedha hizo haziwahusu wabunge hao hali ambayo
imeibua maswali mengi kwa wabunge hao.
Akijibu
hoja hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene
kuhusu mgawo wa fedha za mfuko wa Jimbo, amesema kuwa mfuko huo upo kwa
ajili ya majimbo na si kuwalipa wabunge wa viti maalumu.
Amesema
kuwa yeye yupo kwa ajili ya kusimamia mfuko huo uliopo kwa mujibu wa
sheria za bunge hivyo hana nanma ya kubadilisha sheria hiyo ili
kuwawezesha wabunge hao kupata fedha hizo.
Aidha,
Katika hatua nyingine, Simbachawene ameongeza kuwa kwa upande wa
Zanzibar kuhusu fedha hizo amesema kuwa atawasiliana na Ofisi ya Makamu
wa Rais ili kuweza kuweka utaratibu maalum wa kuharakisha upatikanaji wa
fedha hizo.
“Mfuko
huu hauwahusu wabunge wa viti maalum, napata wakati mgumu kama Jimbo
moja linakuwa na idadi kubwa ya wabunge wa viti maalum, ina maana fedha
hizi zitaishia kwenye mgawo wa wabunge,”amesema Simbachawene.
No comments:
Post a Comment