Trending News>>

Ndoto ya Himid Mao yafifia Randers FC


Copenhagen, Denmark .Ndoto ya kiungo wa kimataifa wa Tanzania na Azam, Himid Mao kucheza soka la kulipwa itasubili kidogo baada ya klabu ya Randers FC kushindwa kumpa mkataba.

Himid katika majaribio yake alionyesha soka ya kiwango cha juu, lakini si aina ya mchezaji anayetakiwa na klabu hiyo kwa sasa.

Randers: Himid Mao hatopewa mkataba kwa sasa na Randers FC.

Klabu ya Randers iliweka wazi baada ya kikao cha benchi la ufundi kilichofanyika Jumanne usiku, ambako mkurungezi Michael Gravgaard, mkuu wa kuibua vipaji Rasmus Bertelsen na kocha Olafur Kristjansson kumfanyia tathimini kiungo huyo mwenye miaka 24, ambaye amekuwa naye tangu wiki iliyopita na kucheza mechi moja ya wachezaji wa akiba Jumanne dhidi ya Horsens .

"Himid Mao ni mchezaji mwenye kipaji kinachonekana wazi na mwenye uzoefu wa kucheza mechi za kimataifa kutokana na kuichezea nchi yake katika mechi za kimataifa," alisema Rasmus Bertelsen.

"Lakini pamoja na hayo bado tunatafuta aina nyingine wa kiungo wa kati tunayemtaka kumsajili kwa sasa.

Kwa hiyo hatopewa mkataba?

"Siyo kwa sasa. Kwa mfano, kama baadhi ya viungo wetu waliopo sasa wataondoka, tunaweza kumwita tena. Lakini kwa kikosi chetu cha sasa kilivyo, si aina ya kiungo tunayemtaka kumuongeza, alisema Rasmus Bertelsen.

"Kama tulivyosema awali, tunahitaji kiungo wa aina ya  Christian Keller," alisema Bertelsen, ambaye hakukataa kuwa kutakuwa na wachezaji wengi watakaofanyiwa majaribio msimu huu.

Himid Mao aliondoka Jumatano kurejea Tanzania, akitegemewa kucheza mechi dhidi ya Toto African.

No comments:

Powered by Blogger.