Mzee aliyebuni na kuchora Nembo ya Taifa apatiwa matibabu na Serikali
Mzee aliyebuni na kuchora Nembo ya Taifa apatiwa matibabu na Serikali
Serikali
ya imelazimika kumuhamishia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mzee
Francis Maige Ngosha aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Amana kwa
kipindi cha siku moja kwaajili yakupatiwa matibabu zaidi.
Akitoa
tamko la serikali Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Khamisi Kigwangalla amesema mzee huyo ambaye ni
mmoja wa wachora Nembo ya Taifa amesema wameamua kumuhamishia katika
hospital hiyo ya Taifa Muhimbili ili kufanyiwa uchunguzi wa kina na
wataalamu wa magonjwa mbalimbali ili kubaini na kutibiwa.
Dkt.
Kigwangalla amesema serikali itahakikisha inampa tiba kamili na malezi
kwa kuzingatia haki ya kuishi ya binadamu na kuthamini mchango wa wazee
na waasisi wa taifa.
Kwa
upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya dharura kutoka Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga amesema wanasubiri majibu ya
vipimo wanavyomchunguza na pindi watakapobaini tatizo atapatiwa matibabu
yake.
Kwa
upande wake Francis Maige Ngosha ambaye ni mmoja wa wachora Nembo ya
Taifa ameishukuru serikali na jami iliyokuwa ikimlea kwa miaka yote bila
malipo.
No comments:
Post a Comment