Mume amuua mkewe kwa kipigo
Mwanamke mmoja amekutwa akiwa
amefariki dunia chumbani kwake huku mwili wake ukiwa na majeraha baada
ya kupigwa na mumewe, wilayani ilemela mkoani Mwanza.
Muonekano wa sehemu ya Jiji la Mwanza
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kwamba tukio hilo
limetokea leo tarehe 30, Mei 2017 saa 9:09 alfajiri katika mtaa wa
Pasiansi Mashariki wilayani humo.
Kamanda Msangi amesema tukio hilo
limetokea baada ya kuzuka kwa ugomvi kati yao ambapo mwanamke huyo
aliyefahamika kwa jina la Ester Charles (30) alipigwa na mumewe na
baadaye mwanamume huyo anayefahamika kwa jina la Charles John (35)
kutoroka kusiko julikana.
Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa akiishi
nyumbani kwao na mumewe lakini kwa kipindi chote wakiwa kwenye
mahusiano wawili hao walikuwa kwenye migogoro ya mara kwa mara ya ndani
ya familia kwani mwanamke alikuwa akimtuhumu mumewake kwamba anatoka
nje ya ndoa.
DCP Ahmed Msangi
JINSI ILIVYOKUWA
Inasemekana kuwa usiku huo majirani
walisikia ugomvi ukiendelea kati ya wawili hao huku mwanamke akipiga
kelele akiomba msaada, lakini majirani hawakwenda kuwasaidia kwani
walizoea kuwasikia wakipigana na baadaye kuelewana kisha kuendelea na
maisha kama kawaida.
Baada ya muda kupita hapakusikika tena
ugomvi hivyo majirani walijua tayari wameelewana, lakini baadaye
alisikika mtoto akilia kwa muda mrefu ndipo walipata mashaka kisha
walitoa taarifa kituo cha polisi.
Polisi walifika eneo la tukio kisha
kumkuta mwanamke huyo akiwa tayari amepoteza maisha, huku mwili wake
ukiwa na majeraha ya kupigwa na kitu kizito maeneo mbalimbali ya mwili
wake na shingoni kwake kukionekana kukabwa na kitambaa kigumu na mumewe
aliyekuwa wakipigana kisha baada ya kuona mkewe amefariki dunia
alitoroka kusiko julikana.
Amesema polisi wapo kwenye msako mkali wa kuhakikisha mtuhumiwa wa mauji hayo anakamtwa, huku upelelezi ukiwa unaendelea.
No comments:
Post a Comment