Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent bado aendelea kushikiliwa na Polisi
Arusha. Jeshi la Polisi mkoa hapa linaendelea kumshikilia mmiliki
wa shule ya Lucky Vicent, Innocent Mosha kutoka na tuhuma za gari lake
kuzidisha idadi ya abiria na kusababisha ajali iliyogharimu maisha ya
wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.
Gari hilo lililopinduka katika eneo la Rotya wilayani Karatu, mkoani Arusha Mei 6, mwaka huu inadaiwa kubeba abiria 38 wakati uwezo wa gari ni kubeba abiria 30.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amesema kuwa wanaendelea kumuhoji mmiliki huyo wakisubiri jalada kutoka ofisi ya mwanasheria wa Serikali ili afikishwe mahakamani.
"Tunaendelea na uchaguzi na faili, likirudi kutoka ofisi ya mwanasheria wa Serikali tutamfikisha mahakamani,"amesema.
Akizungumzia ukaguzi wa magari ya shule, Ilembo amesema kuanzia sasa ukaguzi utakuwa wa kudumu.

No comments:
Post a Comment