Mbaraka wa Kagera, Niko tayari kurudi Simba
Mshambuliaji wa Kagera Sugar na timu ya taifa Mbaraka Yusuph amesema
yupo tayari kurudi Simba endapo klabu hiyo itatimiza mahitaji yake kabla
ya kusaini mkataba wa kuitumikia.
“Nipo tayari kurudi Simba endapo watakidhi mahitaji yangu,” amesema Mbaraka wakati akizungumza na Sports Extra ya Clouds FM.
Mbaraka alitolewa kwa mkopo kwenda Kagera Sugar, lakini baada ya mkataba wake na Simba kumalizika akajiunga na Kagera Sugar ambayo inammiliki kama mchezaji wao halali tofauti na Simba wanavyodai kwamba bado ni mchezaji wao halali.
“Mimi ni mchezaji halali wa Kagera Sugar, makataba wangu na Simba ulishamalizika kwa hiyo kama wananihitaji inabidi tukae chini na kuzungumza.”
Mbaraka amesema malengo yake katika msimu uliopita yalikuwa ni kuwa mfungaji bora lakini hakufanikiwa badala yake akaishia kufunga magoli 12 magoli mawili nyuma ya Simon Msuva na Abdulrahman Musa walioshinda tuzo hiyo kwa kufunga magoli 12 kwa msimu mzima.
“Nilipanga niwe mfungaji bora msimu huu lakini kwa bahati mbaya malengo yangu hayajatimia, nashukuru kwa hii tuzo niliyoshinda ya mchezaji bora chipukizi.”

No comments:
Post a Comment