Kivuko kipya Magogoni-Kigamboni chafanyiwa majaribio
Hatimaye
kivuko kipya cha MV KAZI kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na
magari kwa mara ya kwanza Jijini Dar es Salaam baada ya kukamilika kwa
matengenezo yake.
Majaribio
hayo yalifanyika kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini
ambayo inavitaka vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya
kuanza kazi ili viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness
Certificate”.
Awali
wataalam kutoka Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) waliweza kupima
ubora na uimara wa kivuko hicho kwa kutumia utaratibu wa kuweka mawe
yenye kilo zinazolingana na uwezo wa kivuko pamoja na magunia ya mchanga
ili kuweza kupima uwezo wa kivuko kulingana na mahitaji yaliyoainishwa
kabla hakijabeba abiria na mizigo.
Zoezi
hili pia lilihusu kufanyika kwa kipimo cha kuhakikisha kuwa kivuko
hakilali upande mmoja yaani “Inclination test” ambapo kilionyesha Kivuko
kiko sawa. Taarifa ya zoezi hili itakuwa sehemu ya vitu vya
makabidhiano wakati wa upokeaji wa Kivuko.
Ujenzi
wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo
wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170. Kivuko hicho
kitakabidhiwa rasmi hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni Jijini
Dar es salaam na kuongeza idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia
vitatu.
Kivuko
cha MV KAZI kikiondoka kwa mara ya kwanza kutokea Magogoni kuelekea
Kigamboni kikiwa na abiria na magari. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa
majaribio mara baada ya ujenzi wake kukamilika kabla ya kukabidhiwa kwa
TEMESA.
Abiria
wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande
wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba
abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment