Trending News>>

Jelly: Simu janja ndogo zaidi, ya kutosha kiganjani inayokuja na mfumo wa 4G


Imezoeleka ukitaka kufurahia teknolojia za kisasa zaidi basi itakubidi kununua simu ghari zaidi, ila kwa simu ya Jelly ni tofauti. Utapata simu yenye mfumo wa 4G, na Android 7.0 na kwa bei nafuu zaidi.

Simu ya Jelly inasifa ya kuitwa simu janja yenye umbo dogo zaidi duniani inayokuja pia na teknolojia ya mawasiliano ya 4G na pia toleo la kisasa la Android 7.0

Muonekano wa simu ya Jelly
Simu hii ni simu nzuri tuu yenye uwezo wa kuzishinda simu nyingine nyingi za Android zinazouzwa kwa bei ya juu tuu na huku zikikosa sifa ya kuja na Android 7.0 na kuwa na uwezo wa 4G LTE.

Simu ya Jelly inakuja katika matoleo mawili, Jelly ya kawaida inayokuja na RAM ya GB1 na diski uhifadhi wa GB 8, itauzwa kwa dola 109 za Kimarekani, yaani takribani Tsh 220,000/=. Pia kuna Jelly Pro yenye GB 2 ya RAM na diski uhifadhi wa GB 16, hii itaenda kwa dola 125 (Takribani Tsh 250,000/=).

Simu zote hizi kwa sasa zinapatikana kwa bei pungufu kwa watu wanaochangia matengezo ya mkupuo wa kwanza wa simu hizo. Watu wanaotaka matoleo ya simu hizo kwa haraka zaidi wanaweza kufanya malipo kupitia mtandao wa Kickstarter ambapo simu zitaanza kutumwa duniani kote kuanzia mwezi wa nane mwaka huu.

Sifa kwa uchache

  1. Android 7.0 Nougat
  2. 4G LTE
  3. Laini mbili (ukubwa wa Nano)
  4. 1.1GHz quad-core processor
  5. Kioo mguso (Touchscreen/display) cha inchi 2.45 (240×432 resolution)
  6. RAM GB 1 (GB 2 kwa Jelly Pro)
  7. GB 8 ya diski uhifadhi /storage (GB 16 kwa Jelly Pro)
  8. Betri ya mAh 950, kutokana na udogo wa display/screen kiwango hichi ni sahihi na hakina tatizo.
  9. MP 2 kwa kamera ya selfi, na MP 8 kwa kamera kuu
  10. Teknolojia ya WiFi
  11. Toleo la Bluetooth 4.0

Simu hii inaweza kuwa nzuri sana kama simu yako ya pili. Kuweza kukusaidia kuibeba ata sehemu ambazo ungekuwa na wasiwasi wa kupoteza au kuibiwa simu yako ya gharama zaidi. Inatengenezwa na moja ya kampuni ifahamikayo kwa jina la Unihertz ya jijini Shanghai.

Udogo wa simu ya Jelly.

No comments:

Powered by Blogger.