Trending News>>

Je, 'Daudi Bashite' Atajibu Maswali Haya 24? Ni kesho Mei 22


By Pascal Mayalla
Wanabodi,
Hili ni bandiko la uhamasishaji, kesho make sure you don't miss this session!. Macho na masikio yetu yote ni Star TV, wakati kesho itakuwa ndio mara ya kwanza kwa Daudi Albert Bashite kujitokeza rasmi. Swali la msingi ni jee atajibu maswali haya, jee ungekuwa ni wewe ungependa kumuuliza swali gani?.
Kanuni ya kwanza ya haki kote duniani ni "No one is condemned un heard", yaani hakuna mtu anaweza kuhukumiwa bila kusikilizwa!, mtu yoyote mwenye tuhuma zozote, kabla hajahukumiwa, lazima kwanza apewe fursa ya kujieleza na kujitetea.
Wakati Tume ya Mwakyembe ilipomhukumu Edward Lowassa bila kumpa nafasi ya kusikilizwa, sisi wengine humu tuliilaani na kuishutumu kamati ile.
Ni kwa muda mrefu sana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Daudi Albert Bashite, ametuhumiwa kwa tuhuma lukuki zikiwemo kughushi vyeti vya elimu, kutumia majina yasiyo ya kwake, kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake kama mtumishi wa umma, kuvamia kituo cha Clouds TV akiwa na askari wenye silaha za moto na mavazi ya makirikiri etc. etc.
Hakuna hata wakati mmoja, mtuhumiwa huyu alipewa fursa ya kujieleza na kusikilizwa, bali alifikia hadi kuhukumiwa na Jukwaa la Wahariri TEF, bila kusikilizwa.
Lakini hatimaye kituo cha Televisheni cha Star TV, kwa busara kubwa, kesho siku ya Jumatatu, kimeamua kumpatia fursa na haki ya kusikilizwa tena akiwa live, mubashara moja kwa moja kutokea studio, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi.
Ni matumaini yangu, wapenzi wote wa haki za binaadamu, na wapenzi wa the right to information, wapenzi wa freedom of expression, wapenzi wa nothing but the truth, wataiunga mkono hatua hii nzuri ya Star TV, na wale wenye nafasi, watahakikisha, they never miss session, watasikiliza.
Mimi kwa upande wangu, kesho asubuhi nitasitisha shughuli zangu zote na kuelekeza macho na masikio yangu kule Star TV, ili nisikie mwenyewe kwa masikio yangu huku nikishuhudia kwa macho yangu, tone ya kujibu maswali, pulse ya adrenaline, na eye contacts,ili tukidanganywa, tuwaeleze members humu kipi amesema kweli na kipi amedangaya bila hata ya kutumia lie detectors.
Maswali ni mengi kumhusu Daudi Albert Bashite, swali ni jee maswali haya yatajibiwa?.
Muongozo kwa waulizaji maswali, wasiulize maswali kwa mtindo wa simple questions, bali wamuulize kwa mtindo wa interrogations, ili wauliza maswali kuonyesha, they did their homework well.
Mswali 10 ya mwanzo ni intro tuu kwa kumwambia ajitambulishe kwa simple questions na maswali kumi ya pili ni concrete questions zilizofungwa bila mlango wa kutokea, lazima mtu aseme ukweli.
1. Alizaliwa lini, wapi, na aliitwa kwa majina gani?.
2. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
3.Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale Kolomije, alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani?, shule gani na matokeo ni nini, alipasi au alifeli .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5. Alitumia majina gani matatu sekondari, Pamba, alihitimu mwaka gani na alipata matokeo gani?
6. Alijiunga chuo cha Nyegezi kusomea nini, mwaka gani, kwa cheti gani na majina gani?.
7. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa cheti gani chenye majina gani? .
9. Alijiunga chuo cha Ushirika kusomea nini, mwaka gani kwa vyeti vipi, alihitimu lini?
Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.
10. Alipoteuliwa alitumia majina gani.
Baada ya hapa, ndipo waje na interrogation questions
11. Uchunguzi wetu umeonyesha ulianza shule mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije ukitumia majina ya Daudi Albert Bashite, na mwaka 1991 ulirudia darasa la nne, kulitokea nini hadi akarudia darasa?.
12. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition), na uliishi kwa Mama Kamese, jee ulifanya kosa gani hadi kufukuzwa kwa Mama Kamese na nguo zako kwenda kutupwa Stendi ya Kolomije, wasamaria wema wakaziokota na kuzipeleka kwa wazazi wako?.
13. Uchunguzi wetu umeonyesha Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 shule ya Nyanza, lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali, uliwezaje kujiunga na Shule ya Sekondari ya Pamba mwaka 1997 kwa kidato cha kwanza wakati ulifeli Nyanza?.
14. Inasemekana Mwaka 2000 ulihitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero) lakini mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002. Jee uliwezaje kupata cheti cha Paul Christian?, ulikiiba au alikupa mwenyewe?
15. Inasekana Mwaka huohuo 2002 ukitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005, kwa nini uliendelea kutumia majina ya Paul Christian badala ya kubadili majina baada tuu ya kujiunga Nyegezi?.
16. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yako ya uvuvi, kwa nini aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada kilimo bila kubadili majina ya watu?.
17. Baada ya kukosa nafasi kusoma Sokuone, uliwezaje kwenda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta wakati hamna undungu wa aina yoyote?.
18. Mwaka 2006, alipopata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa nini uliendelea kutumia vyeti vyako halali vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani) lakini kwa kutumia majina ya Paul Christian?.
19. Ulipojinga Chuo cha Ushirika, ulidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting na mwaka 2007 ulimaliza first year, kwa nini ulishindwa kuendelea na 2nd year?.
20. Mwaka huohuo 2007 kwa nini uliomba Admission upya? lakini mwaka uliofuata wa 2008 kulitokea nini hadi ukaamua kuacha chuo? na badala yake akaenda kuomba tena udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine wakati mwanzo uliishajaribu lakini akakosa?.
21. Kwa nini mwaka 2009 ulirudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya kwa kaachana na CMA ulisomea hapo mwanzo, na badala yake ukachukua Community & Economic Development (CED)?.
22. Mwaka 2012 alipohitimu shahada yako ya kwanza ya Community & Economic Development, kwa nini uliendelea kutumia jina la Paul C hristian badala ya majina yako halisi ya Daudi Albert Bashite?.
23. Ulipo kula kiapo mahakamani cha kubadili majina, kwa nini uliendelea kuapa kiapo cha uongo kwa kutumia majina ya wizi ya Paul Christian Muyenge na kuwa Paul Christian Makonda ya badala ya kutumia majina yako halisi ya Daudi Albert Bashite?. Jee unajua kula kiapo cha uongo mahakamani ni kosa la jinai?.
24. Kwa nini ulitumia jina la uongo kuolea mke, jee unajua kiapo cha uongo kwenye ndoa, kinaweza kuibatilisha ndoa?. Pia umetumia majina ya bandia kuombea hati ya kusafiria ya Tanzania, jee unajua ni kosa la jinai?.

No comments:

Powered by Blogger.