ELIMU:Waziri wa Elimu awasimamisha kazi vigogo wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako leo Jumatatu
jioni amewasimamisha kazi Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicholas Bureta na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TIE), Dr. Elia
Kidga kufuatia sakata la kasoro zilizopo katika vitabu vya kujifunzia
wanafunzi.
Waziri Ndalichako ametangaza hatua hiyo kufuatia kuibuka kwa mjadala bungeni leo jioni kuhusu kasoro kwenye vitabu hivyo ambavyo vimechapishwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kufundishia. Miongoni mwa makosa yaliyobainika kwenye vitabu hivyo, ni kurasa ulioandikwa kuwa Dodoma ndio mji mkubwa Tanzania.
Waziri Ndalichako amewasimamisha viongozi hao na ameliambia bunge kuwa uchunguzi wa kina unafanyika na baada ya kukamilika hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.
Wabunge walitishia kuzuia kupitisha bajeti ya Wizara ya Elimu hadi hapo wizara itakapotoa uamuzi wenye mantiki katika kutatua tatizo hilo lililozua mvutano mkubwa.
“Kwa mamlaka niliyonayo, namuagiza Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), kuondoka ofisini mara moja ili kupisha uchunguzi,” alisema Ndalichako
Baada ya waziri kutoa agizo hilo, wabunge waliridhia kupitisha bajeti ya wizara hiyo.

No comments:
Post a Comment