Aliyekuwa meneja wa zamani wa Diamond, Rich Mavoko, Nay wa Mitego
pamoja na wasanii wengine, Meneja Maneno, amefunguka kwa kutaja majina
ya baadhi ya wasanii anaodai wanaamini ushirikina huku akikiri kuna
wasanii wengine ambao yeye mwenyewe aliwapeleka kwa waganga wa kienyeji
kwa ajili ya kuroga.
Meneja Maneno amedai Rich Mavoko, Sam wa Ukweli ni moja kati ya wasanii wanaoamini ushirikina huku akidai katika wote Diamond Platnumz ndiyo zaidi yao.
“Ndele ni sehemu ambayo
baadhi ya wasanii waliiamini sana lakini Mungu akisema ‘Yes’ ni ‘Yes’ tu
kwa hiyo nakumbuka wasanii ambao nilikwenda nao kwa waganga kuroga ni
pamoja na Rich Mavoko tena tulienda mbali kabisa huko Kigamboni ndani
ndani huko tumeenda ndugu yangu, nilisharusha nazi katikati yaani usiku
ule unajifanya chizi kama umevurugwa,” Meneja Maneno alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Aliongeza,
“Hata Sam wa Ukweli siwezi kukataa, ni watu ambao imani yao iliwapeleka
huko lakini mimi nakumbuka kazi yangu niliyokuwa nafanya sikutaka
kwenda kwa waganga…. ila sasa huyu Mondi sasa nimepata taabu naye, mara
leo twende kwa mjomba, tunapeleka unga, leo tunapeleka mchele na mganga
alivyo mshenzi hajawahi kuagiza samaki, yeye ni jogoo, mbuzi,”
Diamond atajwa kuwa Kinara wa ushirikina kwenye Muziki
Reviewed by
Unknown
on
May 28, 2017
Rating:
5
No comments:
Post a Comment