Trending News>>

Twitter: Jinsi ya kuzuia au kuwezesha meseji binafsi (DM) kutoka kwa watu wote


Makala hii itakusaidia kufahamu jinsi ya kuzuia au kuwezesha meseji za Inbox (DM) kutoka kwa mtumiaji mwingine yeyote kwenye mtandao wa Twitter, awe anakufollow au hakufollow.

Kwa sasa hivi kupitia app ya Twitter kuna uwezo wa kutuma ujumbe kupitia Inbox bila sheria ya herufi 140, hivyo unaweza andika ujumbe mrefu kuliko ukitumia njia ya kutweet.

Kwa kawaida ukijiunga tuu Twitter mtandao huu huwa umezuia wewe kupokea ujumbe wa DM kutoka kwa mtumiaji mwingine yeyote – inatakiwa anakufollow na wewe uwe unamfollow.

Tuanze kwa watumiaji mtandao: Twitter.com

1.Bofya kwenye alama ya Profile (Profile Icon), hii ipo juu upande wa kulia…alafu chagua Settings

2.Upande wa kushoto kwenye orodha – nenda kwenye Security and Privacy – bofya hapo. twitter ruhusu au zuia meseji za dm

3.Shuka chini na utaona sehemu kumeandikwa Receive Direct Messages from Anyone – yaani pokea ujumbe wa moja kwa moja (inbox) kutoka kwa mtu yeyote twitter Jinsi ya kuzuia au kuwezesha meseji binafsi


4.Bofya kuweka kaalama kuruhusu kupokea ujumbe wa DM kutoka mtu yeyote, ondoa chaguo/alama kuzuia.

Kwa watumiaji wa app ya Android


  1. Fungua app, nenda kwenye Settings
  2. Kwenye orodha nenda na bofya Privacy and content
  3. Angalia na tafuta ‘Receive Direct Messages from Anyone – yaani pokea ujumbe wa moja kwa moja (inbox) kutoka kwa mtu yeyote
  4. Bofya kuweka kaalama kuruhusu kupokea ujumbe wa DM kutoka mtu yeyote, ondoa chaguo/alama kuzuia.

Kwenye watumiaji wa app ya iOS


  1. Ingia kwenye app na bofya eneo la Me, kisha nenda kwenye Settings
  2. Kwenye orodha nenda na bofya Privacy and content
  3. Angalia na tafuta ‘Receive Direct Messages from Anyone ‘, chagua kuwasha (On) kupokea ujumbe kutoka kwa mtu yeyote na zima kuzuia.

No comments:

Powered by Blogger.