BALOZI WA LUPEMBE AIPA MKONO WA BARAKA AZAM KWENYE MECHI YA MARUDIANO J'PIL
BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe, ameweka wazi kuwa Azam FC ni moja ya timu zinazowatia moyo Watanzania wanoishi nje ya nchi, huku akiipa mkono wa ushindi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows ya Afrika Kusini.
Lupembe alitoa kauli hiyo wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
“Kwa kweli nimefarijika sana kwa kuiona Azam FC tena kama nakumbuka mlikuja hapa mwaka jana, mlikuja hapa kucheza na Bidvest nikawa mgeni rasmi na mkono wangu ukawa wa kheri mkashinda, nawahakikishieni nitawashika tena mkono na ninauhakika mtashinda tena,” alisema Lupembe
Alisema kuwa atakuwa pamoja na timu hiyo kwa kipindi chote itakapokuwa jijini hapa hadi Jumamosi itakapoelekea Swaziland huku akiitakia kila la kheri kuelekea mtanange huo unaosubiriwa na mashabiki wengi wa timu hizo.
“Ndio tunafahamu kuwa kuna timu kubwa za Simba na Yanga, lakini Azam FC inatia moyo kwa sisi watu ambao tulioko nje nawatakia kila la kheri, mazoezi mema mimi nipo hapa kama balozi, na nitahakikisha nitakuwa na nyie mpaka siku mtakapoenda kucheza mpira,” alisema,
Lupembe aliitembelea Azam FC jioni wakati ikielekea kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo huo.
Mara mwisho Balozi huyo kuishika mkono Azam FC iliichapa Bidvest Wits mabao 3-0 jijini Johannesburg katika mchezo wa raundi kama hii, ambapo kutokana na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza kwa sasa timu hiyo inahitaji ushindi wowote au sare ili iweze kusonga mbele.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe akiwa pamoja na wachezaji wa Azam wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.alip
Kocha wa Azam ... akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
Beki wa Kulia wa Azam, Shomari Kapombe akiwa anagombania mpira na Kingue wakati wa mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
Kiungo wa timu ya Azam, Frank Domayo (kushoto) akijaribu kumtoka mchezaji mwenzake wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
Nahodha wa timu ya Azam Himid Mao akijaribu kuutuliza mpira ulipigwa kwake wakati wa kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
Ramadhani Singano akiwa anapambana na Shomari Kapombe wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
No comments:
Post a Comment