Tume ya Mipango kuanza Safari ya kuhamia Dodoma Mwezi Machi
Katika
kuitikia na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la Serikali kuhamia Dodoma, Tume
ya Mipango inatarajia kuanza kuhamisha watumishi wake kuelekea Makau
Makuu ya Nchi ifikapo mwezi Machi Mwaka huu.
Taarifa
hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi
Florence Mwanri alipokutana na watumishi wa taasisi hiyo Ijumaa Januari
26, 2017 kwa lengo la kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu taasisi
hiyo.
Pamoja
na agenda zingine kujadiliwa katika kikao hicho, suala la kuhamia
Dodoma lilionekana kuchukua nafasi kubwa miongoni mwa wafanyakazi mara
baada ya ratiba ya zoezi hilo kutolewa rasmi ambapo wengi walionesha
kufurahishwa na kutendo cha kutimiza ahadi ya Rais kwa wananchi ya
kuhamia Dodoma.
Mwanri
alieleza kuwa Tume ya mipango itahamisha watumishi wake katika awamu
tatu ambapo makundi mawili yanatarajiwa kuhamia Dodoma ndani ya mwaka
huu.
“Kundi
la kwanza kwa upande wa Tume ya Mipango litaondoka mwezi Machi mwaka
huu ambapo pamoja na mambo mengine, watumishi wa kundi hili watakuwa na
jukumu la kuandaa mazingira kwa ajili ya kuwapokea watumishi wengine
watakaohamia baadae,” alisema Mwanri.
Aliongeza
kuwa sehemu ya pili ya watumishi inatarajiwa kwenda Dodoma kuanzia
mwezi Septemba mwaka huu ambapo pamoja na watumishi wengine, kundi hilo
linajumuisha Mkuu wa Taasisi ambaye ni Katibu Mtendaji akiambatana na
Wakuu wa Klasta, Idara pamoja na Vitengo na kundi la mwisho linatarajiwa
kuhama kuanzia mwezi Machi, 2018.
Kikao
hicho pia kilitoa fursa ya kutolewa kwa taarifa ya utekelezaji wa
majukumu ya Tume ya Mipango katika kipindi cha nusu mwaka, kuanzia Mwezi
Julai hadi Disemba kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Omary Abdallah
alieleza kuwa katika Kipindi hicho Tume ya Mipango imefanikiwa
kutekeleza majukum mbalimbali ikiwemo; kuandaa mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/18na kuendesha mafunzo kuhusu mwongozo wa usimamizi wa Uwekezaji wa Umma katika ngazi ya Sekretarieti za mikoa na mamlaka za Serikali za mitaa nchini.
Mafanikio mengine ni kuendelea kusambaza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21) kwa wadau pamoja na kuendelea kuandaa mikakati minne ya utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaendelea (Mkakati wa utekelezaji, Ugharamiaji, Mawasiliano na Ufuatliaji na Tathmini).
Aidha Tume ya Mipango ilifanikiwa kufuatilia
utekelezaji wa baadhi ya Miradi ya Maendeleo ya Kitaifa katika mikoa ya
Mwanza, Dodoma, Tabora, Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es salaam kwa lengo
la kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa miradi na kuelewa changamoto
zinazokabili utekelezaji wa miradi hiyo.
Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akiongea jambo na Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Sekta za Uzalishaji Bw. Maduka Kessy wakati wa mkutano na watumishi wa taasisi hiyo. |
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Omary Abdallah
akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mipango katika
kipindi cha nusu mwaka, kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba kwa mwaka wa
fedha 2016/17.
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Abdulrahman Mdimu
akiwasilisha mada juu ya maadili kwa watumishi wa umma katika mkutano
uliowahusisha wafanyakazi wa Tume ya Mipango.
Mwanasheria wa Tume ya Mipango, Bibi Nyanzala Nkinga akichangia jambo katika mkutano wa wafanyakazi wa Tume ya Mipango.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
No comments:
Post a Comment