Trending News>>

TAARIFA KWA UMMA: SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUKARIRISHA DARASA, KUHAMISHA AU KUFUKUZA WANAFUNZI KWA KIGEZO CHA KUTOFIKIA WASTANI WA UFAULU ULIOWEKWA NA SHULE

WAZIRI  WA ELIMU, SAYANSI NATEKNLOJIA PROF. JOYCE NDALICHAKO ATEMBELEA TUME YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU
 Wizara imebaini kwamba BADO kuna baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari hususan zisizo za Serikali na hasa zinazomilikiwa na Mashirika ya Dini  ambazo zinaendelea kukaririsha, kuhamishia shule nyingine au kuwafukuza shule wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia alama za ufaulu zilizowekwa na shule ambapo ni kinyume cha sheria.
Kufuatia kuwepo kwa baadhi ya shule zinazoendelea na utaratibu huu, Wizara inatoa maagizo yafuatayo kwa utekelezaji:-
  1. Shule zote zilizowataka wazazi/walezi kuwahamishia watoto wao shule nyingine kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu wa shule husika zinaagizwa kufuata agizo hilo na kuendelea na wanafunzi hao bila masharti yoyote.
  2. Wazazi na Walezi wenye Wanafunzi waliorudishwa nyumbani kwa sababu zilizotajwa hapo juu, wahakikishe wanawarudisha watoto wao kwenye Shule walizokuwa wakisoma ili waendelee na masomo kama kawaida.
  3. Shule ziwe na utaratibu wa kuinua viwango vya taaluma kwa wanafunzi wenye ufaulu mdogo, na hivyo sio ruhusa kukaririsha darasa mwanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu uliowekwa na shule.  Ikitokea ni lazima kufanya hivyo taratibu zilizopo zifuatwe.
  4. Wathibiti Ubora wa Shule, Kanda na Wilaya, Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya wanaelekezwa kusimamia utekelezaji wa agizo hili katika maeneo yao.
  5. Shule yoyote itakayokiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria zilizopo.
IMETOLEWA NA:
Nicolas J. Buretta
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU

No comments:

Powered by Blogger.