Trending News>>

SORRY MADAM -Sehemu ya 15 & 16 (Destination of my enemies)


MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA 
Daktari huyo alijikuta akimuita Rahab, na kuishia katikati mara baada ya kumtazama Shamsa aliye simama pembeni yake. Daktari akabaki kimya akiwa katika hali ya kunto kufahamu asememe nini mbele ya mke wa raisi. Akaingiza mkono wake kwenye mfuko wa koti, akatoa simu yake na kuiwasha. Alipo hakikisha imewaka, akaingia upande wa meseji na kuandika maneno mafupi kisha akamkabidhi Rahab. Rahab kabla hata hayaisoma akastukia akipokonywa simu na Shamsa, hakuamini alicho kiona kimeandikwa kwenye simu hiyo kwa herufi kubwa
(MUHESHIMIWA AMETUTOKA) 
Taratibu Shamsa akaiachia simu hiyo, huku miguu ikimlegea na kujikuta akianza kwenda chini, kabla hajafika sakafuni Rahab, akamdaka.

ENDELEA
“Mpelekeni wodini”
Rahab aliwaamuru askari waliopo katika eneo hilo, wakambeba Shamsa na kumpeleka kwenye moja ya wodi kwa ajili ya kupumzishwa. Rahab akaingia kwenye chumba alicho lazwa Eddy, akawakuta madaktari wakiwa wamemfunika shuka,
Ukimya mwingi ukatawala ndani ya chumba hicho, kila aliye kuweomo ndani ya chumba, huzuni ilimtawala katika moyo wake.
‘EDDY, EDDY’
Rahab aliita kimoyo moyo, huku akiwa ameyafumba macho yake.
‘EDDY EDYYY EDDYYY’

Rahab alizidi kuita kwa hisia kubwa pasipo mtu yoyote kuweza kuhisi kitu chochote, jinsi alivyo zidi kumuita Eddy, kuizuia roho yake isiweze kwenda mbali na ulimwengu huu, ndivyo jinsi nguvu za mwili wake zilivyo zidi kumuishia, akazidi kumita hadi damu za pua zikaanza kumtoka. Gafla Eddy akazinduka kutoka katika usingizi  wa kifo na kukaa kitako kitandani, jambo lililo wastua madaktari wote, wengine nusura wapige ukelele. Taratibu rahaba akaanguka chini, akiwa amechoka kwani ni kwakiasi kikubwa ametumia nguvu nyingi katika kumpigania Eddy.

“Madam Madam”
Nesi mmoja alimuwahi kumuita Rahab baada ya kumkuta akiwa amekaa chini, huku damu za puani zikiwa zinamwagika.
“Nipo sawa”
Rahab alizungumza huku taratibu akinyanyuka, macho yake yote alimtazama Eddy, jinsi anavyo endelea kuhema kitandani. Eddy akamtazama Rahab, wote wakajikuta wakitabasamu kwa pamoja.
                                                                                                  ***
“Sasa ni nini mpango wako?”
Mzee Tukuyu alimuuliza Mzee Godwin baada ya kumaliza kumsimulia historia nzima ya maisha yake.
“Nahitaji kuchukua kiti cha madaraka katika hii nchi?”
“Mmmmmm……. Sasa utajiunga na chama gani cha siasa wakati tayari wewe ni muhalifu?”
“Si kwakutumia siasa, ila ni kwakutumia mtutu”
Bwana Tukuyu akastuka, akajikuta wasiwasi wake ukistukiwa na Mzee Godwin.
“Sa…sa kwa nini unahitaji kulifanya hilo wakati nchi yetu ni nchi ya amani?”

“Amani ni hapo zamani, ila nahitaji kulipiza kisasi kwa wale wote walio weza kuniharibia maisha yangu”
“Godwin kumbuka hilo swala unalo lifanya ni swala moja la hatari sana?”
“Nafahamu, ila itabdidi niweze kulifanya hilo”
Ukimwa ukatawala kati yao, akili ya bwana Tukuyu ikazidi kuwa na mashaka na rafiki yake huyo. Akili yake ikamtuma kwenda kuweza kuita askari ambao wataweza kumkamata Mzee Godwin, na kumsalimisha katika mikono ya serikali, kwani mpango wake utakwenda kusababisha mauti kwa wananchi wengi wasio na hatia.

“Mbona upo kimya unawaza nini ndugu yangu?”
“Aahaa… haapana bwana”
Mzee Tukuyu, alitabasamu huku taratibu akisimama kuingia ndani ya nyumba yake. Mzee Godwin akamtazama Mzee Tukuyu, kisha na yeye akasimama na kuingia ndani, akamkuta mzee Tukuyu akivaa shati pamoja na suruali.
“Unakwenda wapi?”
“Na….naa kwenda hapo mbele”
Kubabaika kwa mzee Tukuyu tayari kulisha mpa alama ya hatari mzee Godwin, aliye anza kuikunja ngumi yake ya mkono wa kushoto taratibu. Gafla Mzee Godwin akachomoa mkanda wa suruli ya Mzee Tukuyu, alio kuwa amening’inia kwenye suruali yake.

“Una……..”
Mzee Godwin akamuwahi Mzee Tukuyu kwa kuuzungusha mkanda kwenye shingo ya mzee huyo, bila hata ya huruma akamkaba Mzee Tukuyu hadi akapoteza maisha yake
“Pumbavu sana”
Mzee Godwin alizungumza kwa dharau kubwa, kisha akaupandisha kitandani mwili wa mzee Tukuyu, akamfunika vizuri kwa shuka kama mtu aliye lala fofofo.
“Tutaonana katika maisha yajayo”
Mzee Godwin alizungumza huku akiyafunika macho ya mzee Tukuyu. Mzee Godwin akatoka nje ya nyumba hiyo na kusimama kila kona, kabla hajapiga hatua hata moyo ya kuondoka, akamuona kijana mmoja akija katika eneo hilo.

“Shikamoo”
“Marahabaa, nikusaidie nini?”
“Nahitaji kumuona mzee, kwani huu ni muda wa kwenda kutega nyavu?”
“Ahaaa mzee kidogo anajisikia vibaya, ila kama huto jali ninaweza kuichukua nafasi yake”
Kutokana kijana ni miongoni mwa vijana walio weza kumuokoa mzee Godwin jana usiku, na kiongozi wao mzee Tukuyu, alikiri kwamba huyo ni rafiki yake wa muda mrefu, basi hakuona ni tatizo kuweza kuongozana na Mzee Godwin kuelekea maeneo ya baharini.

“Mzee anasumbuliwa na nini?”
“Homa ilimshika asubuhi, nimemtafutia dawa amemeza”
“Ahaaa, ila vipi na wewe hali yako?”
Kijana huyo mwenye umri si chini ya miaka ishirini alionekana kuwa mchangamfu sana kwa Mzee Godwin tofauti sana na jinsi mzee Godwin alivyo weza kuhisi
“Mim naendelea vizuri. Unaitwa nani?”
“Mimi?, mimi naitwa Thomas, ila watu wengi hapa kijijini wamenizoea kuniita TOM”
“Una jina zuri”
“Asante na wewe je?”
“Mimi niite babu tu”
“Babu nani?”
“Babu kama babu”

Mzee Godwin hakuhitaji maswali zaidi kutoka kwa Tom, wakafika maeoneo ya fukwe za bahari, wakakuta vijana wengine wawili wakiwasuribi kwenye boti inayomilikiwa na mzee Tukuyu
“Mzee leo anauwa hatokuja”
Tom aliwaambia wezake huku akikunya suruali yake kwa ajili ya kuingia ndani ya maji, hapakuwa na aliye kuwa na swali lolote, zaidi ya kumshangaa mzee Godwin, anaye ambatana nao. Wakawasha boti na kuondoka.

“Tunaelekea mpaka wapi?”
Mzee Godwin aliwauliza, wakiwa tayari wamefika mbali sana na kutoka nchi kavu
“Hapa tunakwenda mbali sana, katikati huko ya kina, ndipo tunapo tegaga nyavu”
“Kwahiyo huwa munazama ndani ya maji?”
“Ndio, tunazama ndani kabisa, huwa tunatumia hiyo mirija ya kuhemea kuzama ndani ya maji”
Maswali yote aliyajibu Tom, aliye onekana kumpenda sana mzee Godwin, pasipo kufahamu kwamba ni moja kati ya watu magaidi wanao isumbua nchi ya Tanzania, na pia ni mtu aliye waulia mzee wao waliye mtegemea sana.

Wakafika hadi sehemu ambayo wanazoea kutega nyavu, ili kuweza kupata samaki wengi sana, Vijana wawili wakajiandaa, Tom naye akataka kujiandaa ila mzee Godwin akamzuia kwa ishara na Tom akatii pasipo kuelewa ni kwa nini mzee Godwin amemzuia. Vijana hao wawili wakipemba, wakajitosa ndani ya maji, huku wakionekana kuwa ni hodari katika zadi hiyo, wakaipokea nyuvu waliyo shushiwa na Tom pamoja na mzee Godwin, kisha wakazama nayo ndani ya maji.
“Watachukua muda gani hadi kutoka?”
“Zaidi ya dakika kumi na tano, kutokana hawa ni wazoefu sana”
“Ahaaa sawa tuachane na hayo. Nyumbani unaishi na nani?’
“Peke yangu?”
“Wazazi wako?”

“Wazazi wangu walisha fariki dunia siku nyingi sana, nimelelewa na majirani zangu wema, hadi leo nimekuwa hivi”
“Una umri gani?”
“Miaka ishirini na moja”
Nzee Godwin alitingisha kichwa huku akitabasamu. Tom akasimama kwenye boti hiyo na kuangalia magharibi kwake.
“Babu unauona huu usawa huu?”
“Ndio”
“Kuna siku mzee Tukuyu aliniambia kwamba kuna msitu, kuna hazina yake ya thamani ameiweka, hata siku nikifa basi nikaichukue”
Maneno ya Toma yakamstua mzee Godwin na kujikuta na yeye akisimama, akatazama sehemu ambayo Tom anamuonyesha.

“Ni hazina gani hiyo?”
“Yeye aliniambia zipo kwenye msitu, upande huu, ila ni vitu vya thamani sana”
“Unaonaje tukaenda kuvitazama?”
“Sasa hivi!!!?”
“Ndio”
“Kuna wezetu humu hatuwezi kuwaacha”
“Hao ni mahodari wa kuogelea, tunakwenda mara moja kisha tunarudi”
Tom akamuangalia usoni mzee Godwin, kutokana ni mzee aliye weza kutambulishwa na babu aliye mchukulia kama ni baba yake, basi akaamua kuufwata ushauri wa mzee Godwin.

Wakawasha boti hiyo inayo kwenda kwa kasi kutokana namshine zake mbili kuwa na uwezo mkubwa sana. Ikawachukua zaidi ya lisaaa moja kuweza kufika kwenye moja ya msitu mkubwa, ulipo pembezoni mwa bahari. Wakashuka na kuiweka boti pembeni, kutokana kagiza kilisha anza kuingia, Tom akachukua tochi kubwa ambayo huwa wanaitumiaga sana kwenye maswala ya kuwavuta samaki kipindi wakivua nyakati za giza.
“Ila aliniambia kwamba msitu huu una wanyama na wadudu wabaya sana”
“Kwani hapa ni wapi?”
“Huu msitu, upo maeneo ya mkoa wa pwani”
“Pwani…..!!”

“Ndio, ukizunguka kivile utakuta mji wa pwani”
Tom alimuelekeza mzee Godwin kwa njia ya baharini. Wakaanza kuingia kwenye msitu huo, huku ujasiri wa Tom ukizidi kumvutia mzee Godwin.
“Mbona hatufiki, alikuambia ni wapi?”
“Mbele kidogo aliniambia kuna miti mitano mirefu sana, kisha chini kuna handaki lenye mfuniko ulio wekewa jiwe kubwa juu yake”
“Ahaa sawa”
Wakazidi kutembea zaidi ya lisaa zima jingnine hadi wakafanikiwa kufika katika sehemu ambayo, Tom alielekweza na Mzee Tukuyu na kila alicho elekezwa alikikuta katika eneo hilo.

“Hapa ndipo penyewe”
Tom alizungumza huku akishangaa shangaa eneo hilo, wakalisukuma jiwe hilo kubwa, ambapo kweli kwa chini wakakuta mfuniko wa chuma. Kutokana Mzee Godwin ananguvu nyingi, aliweza kuufungua mfuniko huo ulio jaa kutu. Wakakuta ngazi nyingi zilizo jengwa kwa saruji zikielekea chini.
“Lete tochi”
Mzee Godwin akachukua tochi, akatangulia mbele huku Tom akifwata kwa nyuma. Wakaingia ndani ambapo katika kumulika mulika mzee Godwin aliweza kuona swichi ukutani. Akaiminya na taa za ndani zote zikawaka

“Waooooo……!!!”
“Tom alishangaa sana, kwani hakuamini kama eneo hilo ni kubwa kiasi hicho na linapendaza sana kwa kiasi kikubwa. Wakakuta baadhi ya computer zikiwa katika eneo hilo, inavyo onekana kama kuna watu walikuwa wanaishi hapo kipindi cha nyuma. Tom akaanza kukagua chumba kimoja baada ya kingine, chumba cha kwanza aliweza kukuta kitanda pamoja na nguo za kike.

“Babu kuna nguo za kike huku”
Alimuita Mzee Godwin, aliye mfwata na kuzishuhudia nguo hizo, wakaingia kwa pamoja kwenye chumba cha pili na kukuta nguo nyingine za kike. Wakaingia chumba cha tatu wakakuta nguo za kike pamoja na bastola, ikiwa kitandani, Tom akaichukua
“Hii ni bunduki……!!!”
Aliitazama huku akiishangaa sana kwani alisha zoae kuiona silaha hiyo kwenye filamu za kizungu za mapambano.

“Ndio ni bastola, hembu ilete”
Akamkabidhi mzee Godwin, aliye itazama vizuri na kugundua ipo sawa, na magazine yake ina risasi za kutosha, japo inaoenekana zimesha tumiwa. Wakaingia kwenye chumba cha nne, wakakuta nguo nyingi za kike zikiwa zimemwagwa kitandani, wakaingia chumba cha tano na kukuta mabegi mawili walipo yafungua wakakuta simu moja ya thamini sana. Samsung Galaxy note two, pamoja na nguo za kike.
“Ina maana walio kuwa wakiishi humu ni wanawake?”
Tom alimuuliza mzee Godwin huku akishangaa
“Ina wezekana”
“Sasa ni kina nani hao, hadi waishi kwenye hili handaki?”

“Mmmm kusema kweli safahamu”
Wakatoka na kuelekea kwenye chumba cha sita, hapo ndipo wakajikuta wamebaki wameduwaa, kwani chumba hicho, kina mlango wa chumba ambao kufunguliwa kwake kunahitaji kuingizwa namba za siri, ili ufunguke.
“Njoo huku”
Mzee Godwin alizungumza, wakaelekea kwenye meza yenye computer sita, akaziwasha zote, kwa bahati nzuri ziliwaka. Akashusha pumzi kidogo akisubiria zimalize kuwaka, ila kilicho mshangaza zaidi, computer zote zilihitaji namba za siri ili kuwaka.

“Eheee”
“Nini tene babu?”
“Zinahiutaji namba za siri”
“Sasa tunazijulia wapi?”
“Hembu lete hiyo simu”
Tom akamkabidhi mzee Godwin simu, akaiwasha kwa bahati nzuri ikawaka pasipo tatizo la aina yoyote, huku ikiwa imebakiwa na kiasi kidogo cha chaji.

“Simu nzuri hiyo”
Tom alizungumza huku akitabasamu sana, mzee Godwin akaingia upande wa picha kuangalia kama ataweza kubahatika kuona sura ya mmiliki wa simu hiyo. Kwa bahati nzuri wakakuta picha nyingi sana, moja ikiwaonyesha wasichana watano waklwa pamoja.

Sura hizo hazikuwa ngeni sana kwa Mzee Godwin, kwani alisha weza kuziona sehemu, huku sura moja akiwa anaitambua vizuri sana, kwani ni mke wa raisi Praygod, bi Rahab. Mzee Godwin akajikuta akimeza mate, huku akiwa ameyatumbulia macho kwenye picha hiyo, kwani Rahab anamfahamu sifa yake, ni miongoni mwa watu walio weza kuvuruga mipango yake yeye pamoja na makamu wa raisi, mwaka mmoja na nusu ulio pita.
                                                                                              ***
Vurugu na ubabe zinazidi kutawala ndani ya gereza la Pentagon, ila wasichana watatu wanazidi kujijengea umaarufu kwa uwezo wao mkubwa wakuweza kuwaparanganyua, maadui zao ambao walijitia vihere here katika kujaribu kupambana nao. Makundi ya wasichana wababe yalizidi kuongezeka siku hadi siku, hadi ikafikia hatua ulinzi katika gereza hilo kwa upande wa wanawake ukaongezwa mara dufu, ili kuzuia fujo zinazo tokea kila siku.
“Unakwenda wapi?”
Fetty alimuuliza Anna aliye simama gafla
“Nakwenda kuoga”
“Kuoga, mida hii?”
“Ndio”
“Kuwa makini si unajua tuna windwa humu ndani?”
“Usijali”

Anna akajifuta amjani majani kwenye nguo yake, sehemu ya makalio, kisha taratibu akaondoka katika eneo hilo la wafungwa kufanyia mazoezi. Moja kwa moja akaelekea kwenye maeneo ya bafu, kwa bahati mbaya akakuta kikundi cha wasichana wengine wenye asili ya Marekani wakimpiga binti mmoja wakizungu. Anaa akataka kupita, ila kila alivyo muangalia binti huyo anavyo chezea kipigo, roho ikamuuma, akatizama idadi yao wapo wangapi, kwa haraka haraka akagundua wapo sita.

‘Ninawamudu’
Ana alizungumza kimoyo moyo, huku akipiga hatua kwenda kwenye eneo hilo
“Heiii nyinyi muacheni huyo”
Anna alizungumza kwa lugha ya kimarekani, huku akiwatazama wasichana hao walio simamisha zoezi hilo na kumtazama vizuri.
“Wewe malaya unasemaje?” 
Kiongozi wao alizungumza huku akichomoa kisu chake na kuanza kupiga hatua kusonga mbele akimfwata Anaa katika sehemu alipo simama.

SORRY MADAM (16) (Destination of my enemies)

Kitendo cha mkuu wao, kumkaribia Anna, ikawa ni kama kosa la jinahi kwake, kwani akakukutana na teke zito la shingo, lililo muangusha chini, huku kisu chake kikiangukia pembeni. Anaa baada ya kufanya shambulizi hilo akajiweka sawa suruali yake na kukunja ngumi tayari kwa kupambana. Walipo muona kiongozi wao amelala chini, kunyanyua anajishauri, hapakuwa na aliye weza kufanya chochote zaidi ya kumnyanyua kiongozi wao na kuondoka katika eneo hilo la sivyo nao wanaweza kukumbana na dhahama aliyo ipata kiongozi wao.
“Vipi umeumia?”
Anna alimuuliza binti huyo, anaye onekana kuwa na mwili mdogo mdogo na nimnyonge sana

“Ndio”
Akamsaidia kumnyanya, akampeleka bafunia, kwenda kumfuta damu zinazo mwagika mdomoni, kwani kipigo alicho kutana nacho ni kikali sana.
“Asante dada”
Binti huyo alizungumza huku akimtazama Anna machoni.
“Usijali”
“Unaitwa nani?”
Binti huyo alimuuliza Anna huku akiwa ametabasamu.
“Jina langu kwa sasa si lamuhimu sana kulifahamu”
Anna alizungumza huku akivua nguo zake, akasimama kwenye bomba la mvua, taratibu akaanza kuoga, muda wote binti huyo akiendelea kumtazama Anna umbo lake zuri ila limejaa mikwaruzo mingi sana ya mateso ambayo anaonekana kuweza kuyapa miaka ya nyuma.

  ***  
“Ni kina nani hawa wadada?”
Tom alimuuliza Mzee Godwin huku wakiendelea kuwatazama Rahab na wezake kwenye picha katika simu hiyo.

“Siwafahamu”
Mzee Godwin alizungumza huku akiendelea kutazama tazama picha nyingine, akatoka upande wa picha na kuingia upande wa mesiji ambapo akakutana na meseji moja iliyo tumwa na doktar William. Akaifungua na kukuta maelezo.
(Namba ya siri ya computer zote ni HHrJ93, Namba ya siri ya chumba ni HHRj94)
Mzee Godwin akatabasamu, huku akiitazama meseji hiyo, kwa haraka akaiingiza neno la siri alilo lisoma, nayo computer hiyo ikafunguka.

“Bingoo”
Mzee Godwin alifuraha sana kwa kufanikiwa kwa tukio hilo, akasimama na kwenda kwenye chumba walicho shindwa kufungua, akaingiza namba za chumba hicho, ambapo mlango wake ukafunguka. Wote wawili wakabaki wakiwa wamesimama wameduwaa, kitu wanacho kiona mbele yao.

Vibunda vingi vya pesa vilivyo pangiliwa vizuri kwenye vimbao vidogo vilivyo jengewa ndani ya chumba hicho, kilicho kaa kama duka dogo, vikawafanya wote wasimama kwa muda kisha Mzee Godwin akaanza kuingia ndani  na kuhakikisha kwamba ni pesa wanayo iona au yupo kwenye ndoto.

Vibunda vya pesa za kitanzania pamoja na dola ya kimarekani, viliweza kuwatoa ufahamu mzee Godwin na Tom, kwani wanashangilia na kuruka ruka kama watoto wadogo, muda mwingine wakajikuta wakikumbatiana na kuruka ruka sana.

“Tumesha kuwa matajirii”
Mzee Godwin alizungumza huku akizidi kumkumbatia Tom, kila mmoja akajikuta akimwagikwa na machozi ya furaha. Kwa upande mmoja wa ukuta wa chumba hicho wakakuta mlango mdogo ulio rudishiwa, Tom akausukuma ukafunguka. Wakakuta bunduki nyingi zikiwa zimepangwa vizuri pamoja na risasi nyingi zilizopo kwenye viboksi vingi.

“Mmmmmmmm…….!!!!”
Mzee Godwin akamsogeza Tom pembeni, kisha akaingia ndani ya chumba hicho, akaanza kukagua bunduki hizo, akagundua kwamba ni mali ya jeshi la Tanzania, na inavyo oenekana ziliibiwa kwa usiri mkubwa katika moja wapo ya kambi za jeshi. Hapa ndipo mzee Godwin akaanza kupata picha ya wasichana alio weza kuwaona kwenye picha.

“Inabidi tufanya mpango wa kuchukua kila kitu tuondoke hapa”
“Sasa babu tutakwenda wapi?”
“Tutajua pa kwenda, ila unaweza kuendesha gari?”
“Hapana”
Mzee Godwin akawaza kitu kichwani mwake haraka haraka, kisha akachukua vibunda viwili vya dola laki moja moja. Akaingia kwenye moja ya chumba alipo ona moja ya koti jeusi, akaona litamfaa, akalivaa, kwa bahati nzuri akakuta moja ya kofia, akaivaa vizuri
“Hapo ninaonekanaje?”
“Umependeza sana babu”
“Basi ninahitaji kwenda Dar er salaam mara moja, ninakuomba uningojee hapa”
“Unakwenda kufanya nini?”
“Utaona ila usitoke katika hili eneo sawa”
“Sawa babu”

Mzee Godwin akarudi kwenye chumba akachuku kibunda kingine cha noti za shilingi elfu kumikumi, akahakikisha bastola yake inasila za kutosha, akachukua moja ya magazine ya akiba iliyo jaa risasi, kisha akaondoka na kumuacha Tom peke yake ndani ya handaki hilo. Akainaza safari kwa miguu, akifwata muelekeo wa barabara iliyo jaa majani mengi, na inavyo onekana hapo awali ilikuwa ikitumika.

Hadi inatimu majira ya saa kumi na moja alfajiri tayari, akawa amefika katika barabara ya mkoani, inayo tokea Dar kuelekea mikoa ya Tanga na Arusha. Kwa jinsi alivyo vaa si rahisi kwa mtu kuweza kumgundua mara moja. Akaanza kusimamisha magari yanayo pita, ila mengi hayakuweza kusimama katika eneo hilo la porini, kwa bahati nzuri akamsimamisha muendesha pikipiki mmoja, aliye weza kusimama.

“Kijana unaelekea wapi?”
“Chalinze”
“ Bei gani hadi hapo?”
“Nitakufanyia elfu  ishirini”
“Sawa”
Mzee Godwin hakuhitaji kupoteza muda kwani anafahamu ni kitu gani ambacho anakwenda kukifanya Dar es Salaam, isitoshe jeshi la polisi linamtafuta kwa udi na uvumba. Safari ikawachukua takribani masaa mawili kuweza kufika Chalinze pasipo kuweza kustukiwa na askari polisi. Akamlipa muendesha pikipiki huyo kiasi cha pesa walicho kubaliana. Akapanda basi la Abood linalo toka mkoani Morogoro kuelekea Dar es Salaam. Akiwa ndani ya gari, pembeni yake kuna kijana binti mmoja, ameshikika gazeti lililo pambwa kwa kichwa cha habari kilicho mstua sana.

‘PIGO WAZIRI MKUU MSTAAFU, MJUKUU WAKE NA MKWE WAKE WAFARIJI DUNIA HOSPITALINI’
Mzee Godwin akaitaza vizuri picha ya mke wake, pamoja na mjukuu wake kipindi cha enzi za uwahi wapo. Maandishi madogo ya chini ya kichwa cha habari hicho yakazidi kumuogopesha Mzee Godwin.

(Mauaji ya mama na mke wa waziri Eddy yamefanywa na mume wa waziri mkuu mstaafu general mstaafu GODWIN)
Mzee Godwin akaishusha kofia yak chini kidogo ili kuificha sura yake, hakuhitaji binti huyo aweze kuiona sura yake. Wakafanikiwa kufika ubungo majira ya saa nne asubuhi, Mzee Godwin akashuka huku moyoni mwake akiwa na hasira kubwa pamoja na huzuni, kwani hakujua ni kwanini kesi ya mauji ya mke wake ameweze kusukumiwa yeye.
“Ila wamenirahisisia kazi”
Mzee Godwin alizungumza huku akitoka kwenye geti kuu la stendi ya basi ubungo.
                                                                                             ***
Mipango ya mazishi ikaanza kufanywa na serikali ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania. Huzuni kubwa ikazidi kutanda kwa ndugu jamaaa na marafiki ambao wanamfahamu waziri Eddy, hata baadhi ya wananchi walio tokea kumpenda waziri Eddy, wakajikuta wakiwa katika simanzi kubwa kwani kiongozi huyo ni muda mchache tangu aingie madarakani amekubwa na tukio ambalo hatoweza kulisahau  kwenye maisha yake.

Ulinzi mkali na madhubuti ukandelea kuimarishwa nyumbani kwa waziri Eddy, ambaye tayari alisha toka hospitalini pamoja na Shamsa. Viongozi wengi wakiserikali, kutoka baadhi ya nchi wakazidi kufurika katika jumba la Eddy, kuhuzuria msiba huo, ulio chukukuliwa uzito, mkubwa na serikali, huku ikitolewa amri ya kumtafuta Mzee Godwin popote ndani na nje ya Tanzania.

Picha za mzee Godwin zikaendelea kusambazwa kwenye kila eneo la nchi ya Tanzania, hadi mitaani picha zake ziliweza kubandikwa, huku kukiwa na zawadi nono kwa yule atakaye fanikisha kukamatwa kwake.

Hasiri dhidi yam zee Godwin ikazidi kujijenga moyoni mwa Eddy, safari hii akazidi kujiapiza moyoni mwake ni lazima aweze kumuua mzee Godwin kwa mikono yake yeye mwenyewe. Kila alipo tazama picha ya Junio, Phidaya pamoja ya mama yake, Eddy machozi yakazidi kumwagika.

“Muheshimiwa kuna mgeni amekuja kukuona”
Mfanya kazi mmoja alimnong’oneza Eddy sikioni, akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia, akaongozana na mfanya kazi huyo, wanao shuhulikia maswala ya msiba kwa ujumla, akampeleka ndani sebleni.
Eddy akamkuta Rahab akiwa amekaa kwenye sofa, huku amevalia mavazi meusi pamoja na miwani nyeusi.
Rahab alipo muona Eddy akanyanyuka na kumkumbatia kwa nguvu. Eddy akashindwa kuyazuia machozi yake na kujikuta akilia kama mtoto mdogo.

“Naomba mutupishe”
Rahab aliwaambia walinzi wake, wakatoka nje na kubaki wao wawili sebleni, wakakaa kwenye masofa.
“Eddy pole kwa kila jambo, lililo teokea kwani ni kazi ya mola haina makosa”
“Asante madam”
“Natambua ya kwamba una uchungu mkubwa sana moyoni mwako kwani kuondokewa na mama, mke pamoja na mtoto ni jambo ambalo ni zito sana.”
“Wewe ni mwanaume, miongoni mwa watu ambao ninawaona watakuja kuwa ni watetezi wa taifa hili mmoja wapo ni wewe”

“Kivipi sijakuelewa muheshimiwa”
Eddy alizungumza kwa sauti ya upole huku akimatazama Rahab machoni mwake.
“Usijali utakuja kufahamu tu. Ila nimetangulia mimi kufika hapa kutoa rambi rambi zangu, ila raisi atakuja kesho, leo kidogo mambo yameingiliana”
“Sawa mama”
Kikaletwa kitabu cha kuandika rambi rambi za wageni walio weza kuhudhuria katika eneo hilo, Rahaba akaandika mchango wake kama mke wa raisi.
                                                                                                  ***
Mzee Godwin  moja kwa moja akaelekea kwenye hospitali ya mhimbili, kuoanana na mmoja wa marafiki zake ambao ni madaktari bingwa wa kutengeneza sura bandia. Akajumuika na wananchi wanao kwenda kuwaona ndugu zao, kuingia kwenye geti la hospitali hiyo pasipo mtu kuweza kumstukia. Moja kwa moja akaongoza kwenye gorofa la maabara, akaanza kupandisha ngazi taratibu kuelekea juu. Akiwa gorofa ya kwanza kwenda gorofa ya pili, akakutana na askari wawili wakishiuka chini, akaishusha kofia yake chini kidogo, akapisha na askari hao wakimtazama.

“Ngoja kwanza”
Askari mmoja alizungumza baada ya kushuka ngazi sita kwenda chini, akatoa picha iliyopo mfukoni mwake.
“Ndio huyu tunaye mtafuta”
Askari mmoja alizungumza na kuanza kupandisha kwenda ngazi za juu huku akikimbia, kwa bahati nzuri akafanikiwa kumuona mzee Godwin akitembea kwenye moja ya kordo.
“Simama polisii”  
Askari huyo alizungumza huku bunduki yake akiwa amemnyooshea mzee Godwin kwa nyuma.

    ==> ITAENDELEA

No comments:

Powered by Blogger.