SHEREHE ZA HARUSI ZA KIFAHALI ZAPIGWA PINI HUKO SOMALIA
Kamishna wa wilaya ya Bula Hawa karibu na mpaka wa Kenya, Mohamud Hayd Osman amenukuliwa akisema kwamba ni idadi ya mbuzi wasiozidi watatu ndio wanaofaa kuchinjwa pekee ili kuwalisha wageni na kwamba sherehe katika hoteli hazitaruhusiwa.
Amesema kuwa mahari itakuwa chini ya dola 150 pekee. Uamuzi huo umefikiwa baada ya maafisa wa Serikali ya nchi hiyo kubaini kwamba takriban watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa hivi karibuni.
Kamishna huyo ameongezea kwamba gharama ya harusi, ukosefu wa ajira na kiangazi ndio maswala yanayowafanya watu kulihama eneo hilo.
Waandishi wanasema sio kawaida kwa familia ya bwana harusi kutumia takriban dola 5000 katika harusi nchini Somalia.
"Mafunzo ya kiislamu yanasema kuwa ndoa inafaa kuwa ya gharama ya chini, alisema Osman.
Hatua hiyo ya kupunguza matumizi katika sherehe za harusi za kifahari ni pamoja na matumizi mengine baada ya maafisa kugundua kwamba ni kwa nini watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa mjini humo.
Wasichana walikuwa wanakataa kuolewa hadi pale kitita cha pesa kitakapotumika kwa dhahabu pamoja na fanicha, alisema.
No comments:
Post a Comment