Trending News>>

MESUT OZIL AWATOA HOFU MASHABIKI WA ARSENAL

Kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil amewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kufuatia kuwepo na tetesi kuwa staa huyo wa timu ta taifa ya Ujerumani anegondoka katika klabu hiyo baada ya kumalizika mkataba wake ambao kwa sasa umebakiza miezi 18 kumalizika.
Ozil alisema kuwa hana shida yoyote ambayo itamfanya aondoke Arsenal na kwasasa yupo tayari kusaini mkataba mpya ila tu kama kocha Wenger atamhakikishia kuwa ataendelea kufundisha Arsenal kwani yeye ndiyo mtu ambaye aliyemsajili na anayemwamini.
“Ninafuraha sana kuwa Arsenal na ihakikishie klabu kuwa nipo tayari kusalia hapa na kusaini mkataba mpya, mashabiki wanataka hivyo, nitakuwepo na mengine ni kwa klabu,
“Wanajua nipo hapa zaidi sababu ya Arsene Wenger. Ndiye aliyenisaini hapa na ni mtu ambaye nina imani kwake. Pia klabu inatambua kuwa nataka kuweka kila jambo sawa jambo ambalo meneja atalitekeleza,” alisema Ozil.
Kwa msimu wa 2016/2017, Ozil ameichezea Arsenal michezo 23 ambapo katika michezo hiyo amefunga magoli tisa na kutoa pasi za magoli sita

No comments:

Powered by Blogger.