Trending News>>

Kampeni zazua balaa, mmoja achomwa mkuki


Mikoani. Kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani zimeanza kuingia dosari baada ya mfuasi wa Chadema, Martha Maenda (33) mkazi wa Kichangani, Manispaa ya Morogoro kuchomwa mkuki mkono wa kulia tukio linalohusishwa na masuala ya kisiasa.

Maenda aliyelazwa wodi namba tatu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, alichomwa mkuki juzi saa 10:00 alfajiri, tukio  linalohusishwa na uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kiwanja cha Ndege mkoani hapa.

Akiwa hospitali, Maenda aMEsema akiwa pamoja na wenzake wakiandaa chai kwenye kambi ya Chadema iliyopo Mtaa wa Kimunyu, walivamiwa na watu wenye silaha za jadi ambao anadai ni wafuasi wa CCM.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro, Fikiri Juma aMEkana chama hicho  kuhusika akitaka Chadema waseme ukweli wa kilichotokea.

ManyamaJr

No comments:

Powered by Blogger.