Wanawake Wabainika Kusuasua Uhitimu Masomo ya Sayansi
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya amebaini uwapo wa idadi ndogo ya wanawake wanaohitimu elimu ya juu katika fani ya sayansi.
Manyanya alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Ardhi cha Dar es Salaam.
Alisema Serikali imeweka nguvu kwenye shule za msingi na sekondari na kusahau wanafunzi wa vyuo vikuu.
“Nilihudhuria mahafali ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, hakuna mwanamke aliyehitimu kwenye fani ya sayansi, leo (juzi) pia nimejionea kati ya wanafunzi sita waliohitimu katika shahada ya uzamivu wa kitivo cha sayansi ya ardhi hakuna mwanamke.
“Hii ni changamaoto kwa Taifa, inatakiwa ifanyiwe kazi, haiwezekani sayansi wasome wanaume tu, kwani wanawake wako wapi?” alihoji Manyanya.
No comments:
Post a Comment