Trending News>>

VIKWAZO VISIVYO VYA KIKODI KATI YA TANZANIA NA RWANDA VINATAKIWA KUONDOLEWA KATIKA KUKUZA BIASHARA KATI NCHI MBILI



Waziri wa Biashara, Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Francois Kanimba akizungumza katika mkutano kujadili masuala ya biashara kati ya Tanzania na Rwanda leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano, Mh. Edwin Ngonyani akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika mkutano kujadili masuala ya biashara kati ya Tanzania na Rwanda leo jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mamlaka za Rwanda na Tanzania pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania.
Viongozi wa waandamizi wa Tanzania na Rwanda wakitembeleo baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini na Kampuni ya Rwanda leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya viongozi waandamizi kati ya Tanzania pamoja na wafanya biashara wa Rwanda.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ni wa kimaendeleo hivyo lazima kuondolewa kwa vikwanzo visivyo vya kikodi.

Ngonyani ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa siku mbili kati Tanzania na Rwanda kujadili masuala ya maendeleo ya biashara kati ya nchi hiyo, amesema kuondolewa kwa vikwanzo visivyo vya kikodi kutaongeza maendeleo katika nchi zote mbili katika ukuaji wa uchumi.

Amesema bidhaa zinazozalishwa nchini  Tanzania  zikifika Rwanda ziweze kukubalika hivyo hivyo na bidhaa za Rwanda zikubalike na mamlaka zilizopo hapa nchini.

Ngonyani amesema Tanzania imeweka mazingira bora ya uwekezaji ambapo wananachi wa Rwanda wanaweza kuwekeza  hapa nchini .

Nae Waziri wa Biashara , Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki wa nchini Rwanda, Francois Kanimba amesema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania ni maendeleo ya kibiashara katika sekta mbalimbali ikiwemo ya sekta ya usafirishaji.

Aidha amesema  mkutano huo utatoa matumaini mapya kwa nchi hizi mbili kuweza kunufaika na kibiashara pamoja na  kutatua changamoto  wanazozipata wafanyabiashara wa nchi hizo.

No comments:

Powered by Blogger.