Trending News>>

STORI ZA MAHABA NA KUELIMISHA KILA SIKU

SIMULIZI: DOKTA SIUMWI HUKO
SEHEMU: YA KUMI NA NNE
MTUNZI: Mr ManyamaJr
MAWASILIANO: 0767464766


ILIPOISHIA
"Wewe ndiyo chanzo cha usaliti, kwani mimi nilikuambia naumwa huko, ulipoanza kushika sehemu ambazo hazihusiani na ugonjwa wangu nilikuambia kabisa kuwa dokta mimi siumwi huko, lakini hukusikia, lengo lako lilikuwa nini?

ENDELEA NAYO  SASA!!!
"Unajua Monica hatupaswi kulaumiana sana kwa hili?" alisema Dokta Kisarawe huku akionesha uso wa huzuni japo moyoni alikuwa akifurahia na kujipongeza kwa kitendo cha kufanikisha kula tunda la mtoto mzuri kama Monica.

"Unasemaje wewe, hivi una akili kweli?" Monica aliendelea kung'aka chumbani humo.

Kutokana na maneno matamu na kuonesha heshima aliyokuwa akiyatoa Dokta Kisarawe, kwa kiasi fulani yalichangia kumlainisha Monica na kuanza kushuka taratibu.

"Sawa lakini siyo vizuri bwana"
"Sawa jamani, naomba tuchukulie kama bahati mbaya mama," alisema Dokta Kisarawe.

Kitendo cha daktari huyo kutumia jina la mama wakati wa kumuita Monica, kilimfurahisha sana mrembo huyo kwani tangu aolewe hakuwahi kuitwa kwa jina hilo na mumewe.

"Poa, nimekuelewa, nimekuelewa baba;" Monica naye alijibu kwa sauti ya chini lakini alijikuta akimalizia kwa neno la baba hali iliyomshangaza na kumchanganya sana Dokta Kisarawe.

Kwa pamoja walivaa nguo zao huku kila mmoja akikumbuka utundu na utaalamu wa mwenzake.

"Ila twende mbele turudi nyuma, huyu dokta ni kiboko kwa mambo ya chumbani, sasa kama amenifanyia utundu wote huu kwenye eneo lisilokuwa na uhuru kama hili, vipi kama tukikutana ndani ya chumba tukiwa na muda wa kutosha, itakuwaje?" Monica aliwaza huku akimalizia kuvaa nguo yake ya ndani kabla ya kumalizia kwa zingine.

"Dah! Hata Mungu aliposema nitakufanyia msaidizi, aisee alikuwa akimaanisha huyu, mama yangu vile nakuambia...," Dokta Kisarawe alijisemea kimoyomoyo huku akifunga mkanda wa suruali yake pana kiunoni.

"Sasa kwa hiyo kuhusu tiba dokta;?" Monica alimuuliza Dokta Kisarawe huku akimuangalia kwa macho ya; Ila unayaweza sana.'

"Aaah, kuhusu tiba inabidi uje baada ya siku mbili lakini kwa sasa nitakupa vidonge f'lani, sawa?" alijibu dokta huku akimuangalia Monica kwa jicho la hata hii si ni sehemu ya tiba?'

Baada ya muda waliagana na Dokta Kisarawe akampa Monica vidonge f'lani vya rangi nyekundu na kumpa maelekezo ya namna ya kuvitumia.

"Basi sawa, lakini dokta nitakushukuru mno kama nitapona na hatimaye kupata mtoto, ujue nina hamu sana ya kuitwa mama jamani;," Monica alisema huku akimtolea macho Dokta Kisarawe hali iliyobadili kabisa hali ya mzunguko wa damu wa daktari huyo mwenye uchu wa warembo wazuri kama alivyokuwa Monica.

"Usijali Mamie, mimi ndiyo Dokta Kisarawe bwana, si umeona mfano kwa rafiki yako Sulee, naye alikuja hapa akiwa haamini kama wewe lakini kwa sasa ni mama kijacho..."

"Mmh! Sawa kama kweli basi mimi naenda bwana"
"Sawa, tutaonana"

Monica alifungua mlango na kuwakuta wateja wengine wakingojea huduma ya Dokta Kisarawe.

Walimtupia Monica macho ya chuki kwani kitendo cha kuitwa yeye kwanza na kuwaacha waliokuwa wametangulia kiliwakera na kuwaudhi vibaya mno.

"Muone kwanza, watu wengine wanajirahisi kwa madaktari wakidhani ndiyo njia pekee ya kutibu magonjwa yao sugu;," yalikuwa mazungumzo ya akina mama wawili waliokuwa wamekaa kwenye benchi la kusubiri zamu huku wakimuangalia Monica kwa jicho baya.

Monica alimkuta rafiki yake Sulee amenuna bila kujua chanzo na sababu ya yeye kufanya hivyo. Moyoni akawaza huenda kilichomuudhi Sulee ni kitendo cha yeye kuchelewa chumbani kwa dokta.

Hali ilikuwa tofauti kabisa kwa upande wa Sulee, wivu wa mapenzi ya Dokta Kisarawe ulikuwa umemkaba hadi shingoni na sasa alikaribia kuzimia kwa hasira.

Kitendo cha kusikia meza na viti vikitoa sauti ya kusukumwa kila mara kilichangia kwa asilimia nyingi sana kwa Sulee kuamini kuwa ni lazima kwa vyovyote vile Monica atakuwa ametembea na Dokta Kisarawe jambo ambalo lilimuumiza kuliko ncha ya wembe kupita kwenye kidonda kibichi.

"Vipi rafiki yangu mbona unaonekana umenuna sana, pole kwa kuchelewa mwaya, "Monica alijibalaguza huku akimshika begani Sulee bila kujua hali mbaya ya wivu iliyokuwa ikimtesa mke huyo wa mtu.

"Ina maana kweli Monica unaweza kunifanyia hivyo;?" aliuliza Sulee kwa sauti ya kukwaruza.

"Nimefanya nini tena Sulee, si nimekuomba msamaha kwa kuchelewa jamani?"

"Si umetembea na Dokta Kisarawe wewe;," alijibu Sulee kwa sauti ya juu na yenye hasira.
Je, nini kitatokea kuhusu penzi la Dokta Kisarawe na wawili hao?⁠⁠⁠⁠

No comments:

Powered by Blogger.