Trending News>>

BADO TUPO PAMOJA KATIKA STORI YETU TAMU YA KUSISIMUA NA KUBURUDISHA

SIMULIZI: DOKTA SIUMWI HUKO
SEHEMU: YA KUMI NA TANO
MTUNZI: Mr ManyamaJr
MAWASILIANO: 0767464766


ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
"Si umetembea na Dokta Kisarawe wewe;" alijibu Sulee kwa sauti ya juu na yenye hasira.

JIMALIZE NAYO SASA
"Mimi Sulee, una akili kweli au? Kwa nini unifikirie hivyo jamani?"

"Akili ninazo tena nyingi sana Monica. Sasa ile kukurukakara ya viti kutoa mlio ilikuwa nini? Ndiyo matibabu yenyewe?"

"Sasa je? Madokta we Sulee unawajua, wakimpima mwanamke mara wamshike makalio, mara watamani kumbusu, kama hukutumia akili yako unaweza kujikuta umemalizwa."

"Mh! Mi siamini Monica."
"Kwa nini huamini? Kwanza naomba nikuulize Sulee, umekuwa ukiniwekea wingu kuonana na dokta, kwani ni nani yako?"

Sulee alishtuka kwa swali hilo hasa alipokumbuka kwamba, mumewe na mume wa Monica ni marafiki na wao pia ni marafiki. Mambo yanaweza kufika mbali

"Mi nimeuliza tu, si nani wangu wala nini!"
"Sasa ni kwa nini umenitolea mimacho kwamba nimetembea na dokta kisa ulisikia viti vikilialia ndani?"
"Maana yangu usije ukamsaliti shemeji."

"Mmmh! Au wewe siku ulipotembea naye mliliza viti? Sema ukweli Sulee."

Ilibidi Sulee acheke ili kupoza mambo, akabalaguza kwa kuanzisha hoja nyingine kabisa nje ya hiyo.

Lakini Monica alishapata ujumbe, aliamini kuna kitu kati ya Sulee na Dokta Kisarawe

"Amekupa dawa lakini?" aliuliza Sulee.
"Ndiyo, amesema nitumie hizo kisha niwasiliane naye.

Walifika kwanza nyumbani kwa Sulee, baadaye Monica akaenda nyumbani kwake.

Alifikia kwenye kiti akiwa amechoka sana kwa purukushani za Dokta Kisarawe

"Lakini kama asingetumia nguvu walahi vile asingenipata, ana bahati sana, kidogo nimpigie kelele

"Lakini lo! Dokta anayajua mambo yule, sijui ni dokta wa mapenzi au wa mwili. Kama ofisini kwake tena chapchapu ni vile. Je, tungekuwa chumbani?" Monica alijikuta akiwaza mengi sana kuhusu dokta na mazingira yote yaliyotokea. Ilikuwa mara yake ya kwanza kumsaliti mumewe na akahisi kuna tofauti kubwa kati ya mumewe na Dokta Kisarawe.

"Kwanza mume wangu hana pawa sana kama dokta. Halafu mume wangu utadhani hahemi, dokta anatoa mhemo mpaka unajua mwanaume yuko kazini," alisema moyoni Monica.

***********************
Dokta Kisarawe alikaa kwenye kiti akimuwaza Monica

"Huyu mwanamke ni mzuri sana kuliko wengine. Da! Bonge la mwanamke. Sijawahi kukutana na mwanamke mzuri kama huyu, ngozi nzuri, laini, hana kipele wala manundunundu kama wengine," aliwaza moyoni daktari huyo ambaye inawezekana mpaka kwa Monica ni mwanamke wa mia mbili tangu aanze kutoa tiba.

***********************

Usiku wakiwa kitandani, mume wa Monica ndiye aliyeanza mazungumzo

"Mke wangu, kwa dokta kuliendaje leo?"

Monica moyo ulimlipuka, alihisi aliulizwa swali lile kwa maana kwamba mumewe amesikia alitembea naye palepale kazini.

"Kwani vipi mume wangu?" Monica aliuliza kwa sauti ya chini.

"Ulikwenda hukwenda?"
"Nilikwenda dear."
"Si ndiyo nakuuliza kulikuwaje?"
"Ooo, alinipa dawa akasema nitumie nikimaliza nirudi kumwambia."

"Basi, tusubirie. Asubuhi unioneshe hizo dawa."
"Sawa."

********************

Nyumbani kwa Sulee, mumewe alikuwa akilishikashika tumbo la Sulee akijifanya ndiyo anaulea ujauzito huo kwa mapenzi ya dhati

"Natamani uzae hata leo mke wangu."

Sulee alicheka huku moyoni akisema

"Ungejua mtoto si wako, wala usingejipongeza, mwenzako mwenye nguvu za kusababisha mtoto ndiyo amehusika."

************************
Asubuhi, mume wa Monica akiwa ameshajiandaa kutoka kwenda kazini alikumbuka kitu, akamwita mkewe;

"Abee."
"Nipe zile dawa."

Monica alikwenda chumbani, akatoka na kipakti;

"Tena dokta alisema nikitaka kuzinywa lazima niwe nimekunywa chai ya kutosha," alisema huku akimpa dawa hizo mumewe

"Khaa! Mbona ni dawa mpya za mafua mke wangu, vipi kwani?"
"Dawa mpya za mafua?"

"Ndiyo. We hukumbuki siku zile mama alipokuja akawa anasumbuliwa na mafua nilinunua dawa hizi?"
"Mh! kweli? Kwani zile si zipo, ngoja nikazilete."

Monica alikwenda kwenye bakuli kubwa la plastiki, akachakurachakura na kuona kipakti cha dawa hizo.

"Kweli mume wangu, si hizi hapa!"
"Si ndiyo sasa."
"Mh! Ina maana Dokta Kisarawe kaniingiza mkenge siyo?"

"Haya, kumbe dokta mwenyewe anaitwa Kisarawe! Kisarawe si walaya ya mkoa wa Pwani, tangu lini likawa jina la mtu! Makubwa haya."

Monica alifedheheka, akaanza kuhisi Sulee amemwingiza mkenge kwa kumpeleka kwa daktari feki na si yule aliyemsaidia yeye

"Lakini kama ni feki, mbona pale nje palikuwa na wanawake wengine wengi tu tena wasiofahamiana na Sulee. Au..?" alishindwa kumalizia.

Baada ya dakika tano mumewe kuondoka, Monica alishika simu, akampigia simu Dokta Kisarawe;

"Dokta za leo, mimi Monica"

"Ooo, Monica mpenzi, umeamkaje? Vipi, umenimisi my dear?"
"Sikiliza Dokta Kisarawe

Je, unajua nini kiliendelea? Usikose .

No comments:

Powered by Blogger.