Trending News>>

USIKOSE KUSOMA HADITHI YAKO KALI INAYOKUJIA KILA MARA KUTOKA KWA MTUNZI KAHIRI..

SIMULIZI: DOKTA SIUMWI HUKO
SEHEMU: YA KUMI NA MOJA
MTUNZI: Mr ManyamaJr
MAWASILIANO: 0767464766


ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA: 
Baadaye kidogo, Sulee alisikia sauti ya kulalamika ya Monica akisema Dokta mimi siumwi huko, mmh!
RUKARUKA NAYO SASA 
Moyo ukazidi kumwenda kasi Sulee, alijua kilichokuwa kikiendelea kati ya Monica na Dokta Kisarawe.

"Yaani kweli Kisarawe anaweza kunifanyia hivi?.," Sulee alijikuta akisema kwa sauti na kuwafanya baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamekaa kwenye benchi wamwangalie kwa jicho la kumshangaa kutokana na sauti yake.

"Haiwezekani, nasema haiwezekani hapa ni lazima nifanye kitu" akazidi kuwaza huku akifikiria njia ya kuzuia kilichokuwa kikiendelea kati ya Monica na Dokta Kisarawe.

Kitendo cha Dokta Kisarawe kumuita Monica aliyefika mwishoni na kuwatangulia baadhi ya wagonjwa kilileta kero kwa baadhi ya wagonjwa na kuanza kumjadili kwa tabia yake hiyo.

"Mh, ina maana huyu dokta hajaona kama kuna wagonjwa wengine hapa tuliowahi?" alihoji kwa sauti ya juu mama mmoja aliyekuwa amekaa kwenye benchi la wagonjwa.

"Shangaa, halafu kila akiingia na mwanamke ni lazima afunge mlango," alishadadia mwanamke aliyekuwa ameketi jirani kabisa na Sulee.

Mjadala juu ya tabia ya Dokta Kisarawe ulizidi kupamba moto baina ya wale wanawake waliochukizwa hasa kwa kitendo chake cha kumuita Monica licha ya kuwakuta baadhi yao wakiendelea kusubiri zamu yao ifike.

"Hapo kutakuwa na kitu, siyo bure nyie niaminini mimi," alisema mwanamke mwingine aliyeonekana kuwa na umri mkubwa kuliko wote.

"Mama yangu vile, haiwezekani watu tumewahi kufika halafu mwingine anafika na kuitwa, hapo kuna jambo, nyie fuatilieni sana," alisema dada mmoja aliyeonekana kuwa na haraka kutokana na kukosa pozi maalum, ilikuwa mara asimame, mara akae, kifupi alikosa utulivu.

Sulee alizidi kuwaza mambo mengi sana, kwanza moyoni alianza kujilaumu ni kwa nini alimuonesha Monica kwa Dokta Kisarawe. Alijua kamwe hawezi kuukwepa mtego wa dokta huyo kwani licha ya yeye mwenyewe kuwa mgumu hadi wanaume wengi mtaani kwao kushindwa kumpata, lakini kwa Dokta Kisarawe alishindwa kupindua, hivyo aliamini hata Monica hawezi kukwepa.

Fujo za Dokta Kisarawe zilizidi kumchanganya Monica kule chumbani, kwani alipokuwa akimpima mikono yake ilikosa staha hivyo akawa anayagusa maeneo hatarishi ya mwanamke huyo mrembo.

Mwanzoni alionekana kuwa mtulivu huku akimuuliza Monica maswali ya kutaka kujua kama tatizo liko kwake au kwa mumewe.

"Kweli kabisa na urembo wote huu, bado hujapata mtoto Monica;?" Dokta Kisarawe alianza kuuliza maswali yake ya mtego.

"Nimeshapata" Monica alijibu kwa sauti kavu tena isiyokuwa na masihara hata kidogo.

"Umeshapata;?" Dokta Kisarawe aliuliza kwa mshangao aliposikia kuwa Monica alikuwa ameshapata mtoto.

"Ee, unajua dokta nakushangaa sana, sasa kama ningekuwa nimeshapata muda ningekuwa niko hapa?"

"Mh, hapa nimepatikana, lakini atalainika tu, mimi ndiye Dokta Kisarawe bwana" Dokta Kisarawe aliwaza moyoni baada ya kugundua kuwa Monica alikuwa mwanamke mtata kuliko alivyokuwa akifikiria.

Oke, sasa hebu kaa hapo;," Dokta Kisarawe alisema na kumuonesha Monica kiti kilichokuwa karibu yake.

Monica alikaa kwa utulivu na kumwangalia dokta kwa macho ya; nakusikiliza’.

"Ni wanawake wengi sana walikuja na tatizo kama la kwako, lakini kupitia mikoni hii waliondoka hapa wakiwa na furaha;," alisema Dokta Kisarawe na kumfanya Monica atabasamu japo kwa mbali.

"Kweli kabisa dokta;?" aliuliza Monica.
"Mama yangu vile;"
"Unafanyaje;?"

"Mimi siyo daktari kwa matokeo ya mtihani, bali ni mtaalam wa taaluma;," Dk. Kisarawe alijibu.

Dokta alisogeza kiti karibu kabisa na alipokuwa amekaa Monica, alianza kumshika tumboni na maeneo mengine.

Mwanzoni Monica alionekana kutulia lakini kadiri mikono ya Dokta Kisarawe ilivyokuwa ikikosa staha, ndivyo alizidi kuhisi kitu cha ajabu kikimtokea.

Dokta alimsimamisha Monica, akawa anamshika kifuani na kumwambia kuwa alikuwa anaangalia kama mishipa ilikuwa ikipeleka vyema damu.

Kwa kuwa Monica hakujua chochote kutokana na taaluma ya kidaktari kumpita kushoto, ilibidi atulie na kumuacha Dokta Kisarawe aendelee na utaratibu wake.

"Aaah, sasa Dokta mbona unanishika huko tena;," Monica aliuliza baada ya mikono ya dokta kushika yale matunda mawili yaliyokuwa yamesimama wima kifuani kwa Monica, wakati akisema hayo alikuwa akijigeuza na kusababisha kiti alichokalia kizidi kutoa mlio wa kuashiria kitu kisicho cha kawaida.

Je, nini kiliendelea hapo? USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA.

No comments:

Powered by Blogger.