SERIKALI YAZINDUA MPANGO KAZI WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.(Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (kulia) akiongea na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Joakim Mhagama ) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akionesha kwa wadau mbalimbali Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimkabidhi nakala ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Injinia Stella Manyanya baada ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wadau (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akiongea na wadau (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Joakim Mhagama akiongea na wadau (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez akiongea na wadau (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura akiongea na wadau (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Naibu Waziri Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura (kulia) akifurahia jambo na kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Injinia Stella Manyanya baada ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam Leo.
Na Eliphace Marwa – Maelezo
13/12/2016
SERIKALI imezindua Mpango Kazi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto unaolenga kushirikisha wadau wengine katika jitihada jumuishi za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto na hivyo kusaidia wahanga wa ukatili huo kupata huduma stahiki ili kudhibiti ukatili nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa jamii inajukumu la kuhakikisha ukatili wa wanawake na watoto unapigwa vita kwa vitendo.
“Serikali inaikumbusha jamii kupambana na vitendo vya ukatili kwani ukatili unafanyika kuanzia ngazi ya familia hivyo ni jukumu la wananchi kutoa taarifa za ukatili wa wanawake na watoto ili vyombo vya dola viweze kuwachukulia hatua za kisheria”, alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa Kumekuwepo na matukio mengi ya ukatili yanayosababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umaskini katika familia, mila na desturi potofu zenye athari katika jamii, malezi na makuzi mabovu na sheria kandamizi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Asasi za Kiraia zinazoshughulika na utetezi wa haki za watoto (TCRF) Bw. Erick Guga amesema kuwa watoto ndiyo wahanga wakubwa wa ukatili huu hivyo ni wakati muafaka kwa mpango kazi kuanza kazi ili kuwanusuru wanawake na watoto katika ukatili.
“Mpango Kazi huu wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto nchini Tanzania utakuwa ndiyo dira kwa wadau wote wa masuala ya maendeleo ya wanawake na watoto hapa nchini hivyo ni vema Serikali kushirikiana na wadau kila inapohitajika”, alisema Bw. Guga.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga amesema kuwa, kabla ya kuandaliwa kwa Mpango Kazi huu, Tanzania ilikuwa na mipango kazi minane (8) ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha Bi. Sihaba ameongza kuwa mipango hiyo haikuwa na mfumo wa pamoja wa kufuatilia na kutathmini ufanisi unaopatikana. Vilevile, kutokana na madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maendeleo ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wakuu wa nchi wanachama waliazimia kwa pamoja kutokomeza ukatili huo kupitia utekelezaji wa lengo Na. 5 na 6 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030.
“ Tanzania ni kati ya nchi nne (4) za kwanza duniani na nchi pekee katika Afrika iliyowezeshwa kupitia jukumu lilioanzishwa la kusaidia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuandaa mpango wa kuzuia na kuitikia afua za kudhibiti ukatili ili kuwa na mipango thabiti ya upatikanaji wa haki, usawa na maendeleo kwa wote”, alisema Bibi.Sihaba.
Akieleza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Sera na Mipango Emmanuela Achayo aliseama kuwa Mpango kazi huo wa aina yake una maeneo makuu manane (8) yatakayotekelezwa na wadau wa maendeleo ya wanawake na watoto.
“Maeneo hayo ni kuimarisha uchumi wa kaya, Uzuiaji wa mila na desturi zenye madhara na Uboreshaji wa mazingira salama katika jamii”, alisema Achayo.
Maeneo mengine ni Kuendeleza mazingira salama ya mafunzo shuleni na stadi za maisha na kuhuisha mahusiano, malezi na makuzi katika familia, Utekelezaji na usimamizi wa sheria, Utoaji huduma kwa wahanga na Uratibu, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mpango kazi wa miaka mitano kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 20121/21022.
Mpango huu mahususi unatarajiwa kuwa na matokeo makubwa baada ya miaka mitano ya utekelezaji kwani utawezesha kuondoa ukatili dhidi ya wanawake kwa asilimia 50 kufikia mwaka 2021/2022; na Kuondoa ukatili dhidi ya watoto kwa asilimia 50 kufikia mwaka 2021/2022, na hivyo kuleta mabadiliko makubwa kwa kuwa na familia salama, na jamii yenye utulivu.
Kazi zitakazotekelezwa na kila mdau kuanzia familia, jamii, halmashauri, mikoa, wizara, sekta binafsi, asasi za Kiraia na wabia wa maendeleo Mpango umeweka mfumo fungamanishi wa uratibu, ufuatiliaji na tathmini ambao utaratibiwa katika ngazi ya Taifa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ngazi ya mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, na ngazi ya halmashauri na Wakurugenzi Watendaji.
No comments:
Post a Comment