MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
Daktari akaingia haraka, ndani ya chumba tulichopo. Kwa haraka akaanza kumuhudumia mama huku akiniomba niweze kutoka nje nimuache aifanye kazi yake kiufasaha. Nikatoka nje huku machozi yakinimwagika. Phidaya akanifwata kwa haraka baada ya kuniona ninatokwa na machozi mfululizo
“Baby kuna nini?”
“Mama anakufa”
Phidaya kwa haraka akaingia ndani ya chumba cha mama na kuufunga mlango, Shamsa akamchukua Junio na kumpeleka nje, kwani hakustahili kuendelea kushuhudia matukio yanayo endelelea kwa muda huu, ukitegemea kwamba umri wake bado ni mdogo sana. Blanka naye akaanza kutokwa na machozi, akanifwata na kunikumbatia
“Ohhh Mungu saidia mama yetu apone, kwa nini inakuwa ni hivi jamani?”
Blanka alizungumza huku akiwa ameendelea kunikumbatia, machozi yakimwagika. Tukaendelea kusubiri nje kwa muda mrefu pasipo Phidaya wala doka Angelina kutoka nje. Wasiwasi juu ya kifo cha mama ukazidi kunipanda, mara kadhaa nilihitaji kwenda kuufungua mlango ili kutazama hali ya mama ila Blanka alinizuia akiniomba niweze kuwapa muda walipo ndani kufanya wanacho kifanya kwa muda huu.
Baada ya masaa kama manne Phidaya akawa wa kwanza kutoka ndani ya chumba huku jasho likimwagika usoni mwake.
“Baby vipi?”
Nilianza kumuuliza Phidaya mara tu alipo simama mbele yetu, akatutizama kwa sekunde kadhaa, mimi na Blanka kisha akashusha pumzi nyingi, iliyo nizidisha kuchanganyikiwa.
“Tumejitahidi kadri ya uwezo wetu katika……katika kumuokoa mama, na…..naa….na….”
Kigugumizi cha Phidaya kikaanza kunipa wasiwasi ulio nifanya na mimi, kijasho chembaba kuanza kunimwagika usoni mwangu.
“Nini mbona huzungumzi?”
“Hali ya mama, si nzuri sana ila bado anapumua kwa kutumia mashine”
“Anasumbuliwa na nini?”
“Mmmmm alipata mstuko ulio pelekea mapigo yake ya moyo kwenda kwa spidi kubwa iliyo mfanya awe katika hali kama ile ila kwa sasa amerudi katika hali yake ya kawaida”
Niliona Phidaya akinichanganyia mada, mara aniambie hali yake ni mbaya mara aniambie hali yake imerudi kama kawaida. Nikataka kuingia chumbani ila Phidaya akanishika mkono.
“Kwa sasa mama anabadilishwa nguo na Angelina”
Nikamtazama Phidaya machoni, kwa kuhitaji kujua anacho kizungumza kina ukweli wowote ndani yake.
“Blanka nenda kamuangalie mama”
Nilimuagiza Blanka, taratibu akapiga hatua za kuelekea chumbani kwa mama, nikabaki na Phidaya tukiwa tumetazamana usoni. Baada ya muda Blanka akatoka akiwa ameongozana na dokta Angelina.
“Vipi?”
“Mama anaendelea vizuri kidogo”
Blanka alizungumza, jambo lililo anza kunipa faraja kidogo moyoni mwangu. Ila Angelina akaniambia siwezi kumuona mama kwa wakati huu kutokana amepumzika.
***
Hali ya mama ikaanza kurudi taratibu kadri ya siku zilivyo zidi kukatika, afya ya mwili wake ikaanza kujijenga taratibu baada ya matunzo mazuri anayo pewa na dokta Angelina pamoja na Phidaya. Kumbukumbu taratibu zikaanza kumrejea na kuwatambua watu baadhi jambo lililo zidi kutufurahisha katika familia yetu. Alipo kaa sawa nikamuelezea mama mpango wote alio kuwa ameupanga Sheila dhidi yake.
“Kumbe yule mtoto alikuwa mshenzi kiasi kile eheeee?”
“Ndio mama, hata yule Fredy wamemuua wao”
“Aiseee, ila kama umesha waua hakuja haja tena ya kuwaadisia kwa maana, hicho ndicho walicho vuna kwa yale mauovu waliyo yafanya”
“Ni kweli mama”
“Pia nisamehe Eddy wangu, kwa kuto kukusikiliza na kumuona mke wako hana maana kwangu, nikidhani waarabu wote ni magaidi”
“Hakuna haja mama ya kuniomba msamaha kwa maana mimi pia nimekukosea mengi”
Nikamkumbatia mama, akiwa kitandani amelala, ikawa ni moja ya ukurasa mwengine tulio uanza kimaisha kama mama na mwanaye. Phidaya akamuanzishia mama mazoezi ya kujifunza kutembea asubuhi na mapema pamoja na jioni, kwani kutokana na kuparalaizi, aliweza kupoteza uwezo wa kutembea na kuzungumza vizuri.
Ndni ya miezi nane mfululizo ya mazoezi pamoja na kupewa dawa za kuipa nguvu mifupa yake pamoja na mwili kwa ujumla, mama akaanza kujimudu kutembea mwenyewe kwa kutimia fimbo maalumu inayo msaidia pale anapokuwa amechoka sana. Furaha ikazidi kuongezeka katika familia yetu, huku mama akizidi kuipenda familia yangu, hadi ikafikia hatua akaanza kutulazimisha mimi na Phidaya tuweze kufunga ndoa mapema, itakavyo wezekana.
“Mama tutafunga tu ndoa”
Phidaya alizungumza huku akiwa amemshika mkono mama, akimfanyisha mazoezi ya jioni ya kutembea tembea kuzunguka nyumba.
“Sawa, unajua mukikaa sana, pasipo kufunga ndoa mutapata uvizu wa kufunga ndoa”
“Ila mama tulikuwa tunakusubiria wewe upone ili nimuoe mke wangu, mtarajiwa”
“Ndio nimesha pona sasa, unaona ninaweza hata kutembea mwenyewe, ninakula mwenyewe”
“Hahaaaaaa”
Mimi na Phidaya tukacheka kwa jinsi mama alivyo kuwa akiruka ruka, akiashiria kwamba amepona kabisa
“Mama angalia usije ukaanguka”
“Siwezi kuanguka, hembu niachie uone leo situmii fimbo kutembea, nitatembea peke yangu”
Phidaya akamuachia mama, na mimi nikaishika fimbo yake anayo itumia kuitembelea. Taratibu mama akaanza kupiga hatua za kutembea. Jambo lililo tushangaza sote, kwani kutoka kitandani hadi leo anaweza kutembea mwenyewe ni kwa msaada wa mwenyezi Mungu ndio umemfikisha hapa.
“Munaona munaona naweza kutembea mwenyewe”
Kadri tulivyo zidi kwenda mbele ndivyo jinsi mama alivyo zidi kuongeza mwendo wa kutembea kwa haraka, japo ule mwendo wake nilio kuwa nimeuzoea haujarudi bado.
“Bibi……!!!.”
Junio alimshangaa bibi yake, baada ya kukutana naye akitembea mwenye, kwani amesha zoea kumuona akitembea kwa msaada wa mtu pemben au fimbo yake ya kisasa, inayo tumia umeme wa kuchaji.
“Twende twende”
Mama alimuambia mjukuu wake, wakaendelea kuongozana, wakaanza kushindana kutembea kwa haraka. Mimi na Phidaya tukabaki tukiwa tunawatazama.
“Asante Mungu wewe ni muweza wa kila jambo”
Phidaya alizungumza huku akimtazama mama anavyo cheza na mjukuu wake. Hapa ndipo nilipo amini kwamba usimdharau mtu usiye mjua kwa maana hujui atakuja kukusaidia katika lipi, na endapo kama mama alivyo kuwa amemkataa Phidaya sidhani kama leo hali yake inge tengemaa na kutembea mwenye. Kwa ni watu wachache sana wanao paralaizi, na kurudi katika hali zao za kawaida.
“Nikuoe lili mke wangu?”
“Hata leo hii”
“Kweli?”
“Ndio”
Nikamkumbatia Phidaya wangu, mwanamke aliye weza kunisaidia katika kipindi changu chote cha maisha yangu, hadi nimefikia hatua ya kubahatika kupata mtoto aliye zidi kuongeza furaha kwenye mioyo yetu. Tukaanza kupanga mipango ya harusi, ambayo hatukuhitaji watu wengi wahudhurie, kwani tunaifungia katika viwanja vya hapa nyumbani kwa mama na si kanisani kama wapendavyo watu wengi sana katika nchi hii ya Tanzania.
“Kabla hamujaingia kwenye ndoa, mimi ninaombi moja tu”
Mama alizungumza mara baada ya kumaliza kikao cha mwisho cha harusi, yetu kilicho hudhuriwa na marafiki wa chache wa mama wengi wao wakiwa ni wafanya kazi wa serikalini.
“Ombi gani mama?”
“Nahitaji, Junio aishi kwangu”
“Sawa mama hilo halina tatizo na wenyewe mumesha zoeana”
Phidaya alizungumza kwa furaha huku akimtazama maama usoni,
“Baba mtu mbona hazungumzi?”
“Mama mimi kwenye hillo sina tabu, tutamtafuta mdogo wake Junio”
“Huyo ndio atakuwa wa kwenu, ila huyu ni wakwangu nataka amrithi baba yako”
Sote tuajikuta tukicheka kwani mama, tangu apone amekuwa muongeaji sana, Junio mwenye tulipo mfikishia habari za kuhamia nyumbani kwa bibi yake moja kwa moja alifurahi sana, kwani ni mara kadhaa alikuwa akikaa kwa bibi yake hata wiki mbili bila hata ya kurudi kwetu.
“Kwahiyo dady mimi nitakua siji huku?”
“Utakuwa unakuja kusalimia, pia sisi tutakuwa tunakuja huko”
“Ila ukienda kwa bibi yako, uli mtindo wako wa kuchungulia chungulia madirishani ukiwa gorofani siku utaanguka hilo bichwa lako livunjike”
“P usimuombee mtoto hivyo”
“Huju mtoto wako asikii, mkorofi kama nini, na ukichukulia bibi yake atakavyo kuwa anamdekeza basi atazidi kuwa mkorofi”
Phidaya alizungumza huku akimtazama Junio aliye jikausha baada ya kuambiwa hivyo na mama yake katika hali ya ukali, sikutaka nimtetee sana Junio kwani mama naye anapaswa kuchukua nafasi yake kama mama, ikanilazimu kubadilisha mada.
“Shamsa mwanangu wewe je unahitaji nini?”
“Mimi nahitaji kusomea udaktari kama mama hapa”
“Ahaaa sasa inabidi tutafue vyuo vya udaktari, ambavyo vinatoa elimu bora”
“Unataka nje ya nchi au humu ndani ya nchi?” Phidaya alimuuliza
“Nje ndio kwenye elimu bora”
“Sawa tafuta tafuta chuo ambacho, wale watu wako hawata weza kukudhuru, wala kukufikia kiurahisi”
“Sawa baba”
Shamsa akaaga na kwenda chumbani kwake, naye Junio akaaga na kwenda chumbani kwake, tukabaki mimi na mke wangu mtaraijiwa Phidaya. Nikamnyanyuka kwenye kiti nilicho kikalia na kumbeba mke wangu na kwenda naye chumbani.
“Leo mbona umenibeba muwe wangu?”
“Ninachukua mazoezi ya siku ya harusi yetu, kwa maana kwa sasa umenenepa”
“Mmmmm ndio unibebe jamani?”
“Ndio mke wangu”
Phidaya akanivuta kitandani na kuanza kunipa haki ya tendo la ndoa, linalo stahili sisi kuweza kulipata kama mmoja ya furaha katika mahusiano yetu.
***
Siku ya harusi ikawadia, watu si chini ya thelathini wakawa wamehudhuria kwenye harusi yetu tuliyo ifanya nyumbani kwa mama yetu, hatukuhitaji kwenda kanisani kuepuka maswala ya kigaidi kama yaliyo tokea kwenye harusi ya kwanza ya Fredy na Sheila. Hatua zote za ndoa, zikaendeshwa na mchungaji kama vile anavyo ziongoza akiwa kanisani
”NDIO NIMEKUBALI NA MUNGU ANISAIDIE”
Phidaya alijibu swali la mchungaji alilo ulizwa kama yupo tayari kuishi na mimi milele hadi pale kifo kitakapo tutenganisha. Taratibu nikamvisha pete mbele ya mashahidi walio kuja kushuhudia tukio hili, akiwemo raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Muheshimiwa Praygod Makuya.
“EDDY GODWIN Je upo tayari kuishi na PHIDAYA EDDY, kuwa mke wako kwenye shida na raha tabu na shinda, hadi pale kifo kitakapo watenganisha?”
Ilibidi Phidaya achukue jina langu la Eddy kwani, jina la baba yake lilikuwa la kiarabu, na siku zote hakulipenda jina la baba yake kutokana na matatizo yao ya kifamilia.
“NDIO NIMEKUBALI NA MUNGU ANISAIDIE”
Phidaya akanivisha pete, huku machozi ya furaha yakimwagika. Nikataka kumbusu ila mchungaji akatuzuia kwa kutumia ishara ya mkono
“BASI NINAWATANGAZA YA KWAMBA EDDY NA PHIDAYA, MUMEKUWA MWILI MMOJA. SASA BWANA EDDY UNARUHUSIWA KUMBUSU MKE WAKO”
Baadhi ya waalikwa wakacheka kwa tukio hilo, kwani nilimvuta kwa haraka Phidaya na kumbeba na kuanza kumnyonya mdomo huku sote tukiwa tumefumba macho yetu na kuwaacha mapaparazi kupiga picha kwa tukio hilo.
Nikamuachia Phidaya, akawapa mgongo waalikwa na kulishika vizuri uwa lake, alilo kuwa amelishika tangu anafika kwenye hii bustani ya maua tunapo fanyia shuhuli hii. Akalirusha na Blanka akafanikiwa kulidaka, ikiashiria kwamba katika familia hii, Blanka atafwatia kuolewa.
Sherehe ikaendelea kufanyika huku kila mtu akitupa pongezi ya kufunga ndoa, muheshimiwa raisi akatufwata sehemu tulipo mimi na Phidaya.
“Hongera sana vijana”
“Asante muheshimiwa”
“Kuna kitu nahitaji nikupe kama zawadi”
“Kitu gani muheshimiwa?”
“Nahitaji kukupa nafasi ya uwaziri wa ulinzi je utaimudu hiyo kazi?”
Tukatazamana na Phidaya, ambaye akanikonyeza kwamba niweze kukubaliana na ombi hilo la muheshimiwa Raisi.
“Ndio muheshimiwa”
“Basi ukimaliza mapumziko ya harusi uje ofisini kwangu nikupe majukumu hayo rasmi, kabla sijatengua baraza la mawaziri kutokana mama yako ameomba kustafu katika kuitumikia serikalini na yeye alikuwa ni waziri mkuu”
“Sawa muheshimiwa raisi, nimekuelewa asante sana”
Raisi akatupa mikono kisha akatuacha tukiendelea na kusheherekea,
“DADY, MOM NINAWAPENDA SANA”
Junio alizungumza huku akiwa amesimama mbele yetu, taratibu Phidaya akachuchumaa na kumkumbatia mtoto wetu, nami nikachuchumaa na kuwakumbatia wote kwa pamoja.
“Tunakupenda pia mtoto wetu”
“Ila dady, mimi nataka kuanza shule”
“Ohhhh basi mwaka ujao utaanza kusoma sawa mwanagu”
“Ndio baba”
Phidaya akampiga busu Junio upande wa kushoto, kisha nami nikampiga Junio shavu upande wa kulia, mpiga picha akatuomba tunate hivyo hivyo kwenye pozi letu, tukapiga picha ya tukio hilo.
“Yeaaaahh”
Tukapiga picha nyingi tukliwa na mtoto wetu kama kumbukumbu ya maisha ya baadaya. Usiku wa siku hiyo hatukutaka makuu sana, ya kwenda kusheherekea nje ya nchi, tukepelekwa katika hoteli ya Serena, ambapo ilitupasa kukaa hapo wiki mbili, kwa ajili ya kuanza ukurasa mpya wa maisha kama mume na mke.
“EDDY UNATAKA NINI NIKUFANYIE MUME WANGU”
Phidaya alimiuliza swali, tukiwa kitandani, mara baada ya kumaliza kuoga na kujitupia kitandani.
“Nahitaji unipatie mtoto mwingine”
“Kweli”
“Ndio mke wangu”
“Basi njoo tumtengeneze, mwengine kwani leo nipo katika siku hatari”
“Kweli?”
“Ndio baba Junio”
Phidaya akajigeuza na kunikalia mapajani mwangu na kunitazama kwa macho malegevu, mkono wake mmoja akaupeleka kwenye swichi, iliyopo pembeni ya kitanda na kuzima taa, giza likatawala ndani ya chumba chetu na shuhuli ya kumtafuta mtoto mwengine ikaanza taratibu, huku kila mmoja akifurahia utengenezaji wa mtoto wetu huyu mpya, ambaye jina lake hatukulijua ataitwa nani.
MWISHOOOOO…………!!!!
No comments:
Post a Comment