Trending News>>

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 45 & 46


Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   
Majibu ya mlinzi huyo mwenye roho ya kikatili sana, yakaustua moyo wa makamu wa raisi kwani ameamini kwamba taarifa hiyo si nzuri kwa upande wake.
“Raisi Praygod Makuya anaelekea hospitalini kuonana na Samson”
“WHAT………!!!”   
Makamu wa raisi alijikuta akiishiwa na nguvu, akajibwaga kwenye sofa lililopo karibu yake akibaki amemtumbulia mimacho mlinzi wake huyo.
                                                                                     
ENDELEA   
Makamu wa raisi akakaa kimya kwa muda akifikiria ni kitu gani anaweza kukifanya, gafla akasimama huku akitabasamu
“Bimgo”
Alizungumza huku akimuomba mlizi wake simu. Akaminya baadhi ya namba kisha  akaiweka simu yake sikioni, baada ya dakika kadhaa ikapokelewa na sauti nzito ya kiume.
“Yaa ni mimi”
 
Makamu wa raisi alizungumza, na kumfanya mtu aliye ipokea simu hiyo kuweza kujua anazungumza na nani.
“Kuna mgonjwa hapo hospitalini kwako, somebody Samsoni. Ninahitajia umuondoe kwenye ramani ya dunia”
“Sawa nimekuelewa muheshimiwa, uishi daiama”
“Asante”
Makamu wa raisi akakata simu huku akiwa katika tabasamu pana. Ulinzi kwenye hii hoteli yake aliyo ijenga kwa usiri mkubwa pasipo serikali ya Tanzania kuweza kuifahamu, uliendelea kuimarika kila kona huku vijana wake wanao muunga mkono wakiwa makini sana kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaye weza kufahamu kwamba kiongozi huyo anaye tafutwa na serikali ya Tanzania yupo kwenye hoteli hii kubwa ya kitalii.
                                                                                              ***
Tayari mawasiliano yalisha fanywa kwenye hospitali ya Muhimbili, ili chumba alicho lazwa Samson kifanyiwe ulinzi wa hali ya juu. Askari wenye bunduki nzito walisha weka ulinzi eneo zima la hospitali wakihakikisha kwamba anapofika Raisi Praygod Makuya, kila jambo linakuwa kwenye mstari na hakuna tatizo la kijinga litakalo kwenda kujitokeza.
 
Hali ya Samson, kidogo inaleta matumaini kwa madaktari, hii ni baada ya kutolewa risasi mwlinini mwake, ambazo kwa bahati nzuri hazikuweza kuleta madhara makubwa sana kwenye mwili wake.
“Nahitaji kumcheki mgonjwa”
Daktari mkuu wa kitengo cha upasuaji aliwaambia askari wawili walio simamam mlangoni mwa chumba alichopo Samson. Mmoja wa askari akachukua kitambulisho kinacho ning’inia kwenye kifua cha daktari huyo na kulisoma jina lake, ili kudhibitisha kwamba kweli ni daktari wa hospitali hiyo, alipo jiridhisha akamruhusu daktari huyo kuingia ndani ya chumba hicho.
 
Dokta Maliki, akasimama pembeni ya kitanda alicho lalala Samson, anaye hemea kwa mashine maalumu za kupumulia.
“Nilazima umfe mwanaharamu wewe”
Dokta Maliki alizungumza huku akivaa gloves zake nyeupe kwenye viganja vyake, ili kutoweza kuacha alama za vidole pale atakapo fanya mauaji yale alio agizwa na Makamu wa raisi. Alipo hakikisha gloves zake zipo vizuri, akachomoa mashine iliyo wekwa kwenye kinywa cha Samson, akasababisha Samson kuanza kujitingisha tingisha taratibu, akijaribu kuipigania roho yake na umauti kwani hewa iliyokuwa inaingia kwenye mapafu yake imekatishwa.
                                                                                             ***
“Endesheni haraka”
Rahab alizungumza huku akihangaika hangaika kwenye siti aliyo kalia hadi Raisi Praygod akamshangaa kwani ni kama mtu anaye hitaji kuweza kuliwahi jambo fulani.
“Kwani vipi mke wangu?”
“Kuna tatizo fanyeni haraka”
“Wapi…!!?”
 
“Dereva ongeza kasi tafadhali”
“Madam sote tunakwenda kwenye mwendo mmoja nikiongeza kasi mimi naweza kusababisha ajali”
Dereva anaye waendesha alizungumza kwa ukanini wa hali ya juu kwani ndivyo sheria ya kazi yake inavyo zingatia, kwenye msafara kama huo wote huwa wanaendesha katika mwendo kasi unao fanana.
“Lakini tunakaribia kufika mke wangu”
Raisi Praygod alimtoa wasiwasi Rahab, aliye yafumba macho yake kwa haraka, kama mtu anaye jaribu kuvuta hisia ya jambo fulani. Kila alipo jaribu kuvuta hisia dhidi ya jambo linalo kwenda kumtokea Samson, akashindwa kuona ni nini kinacho kwenda kutokea. 
 
“Pleaseeeee”
Rahab alizungumza kwa sauti ya juu huku akizidi kuyafumba macho yake kwa nguvu, hadi damu za puani zikaanza kumchuruzika taratibu, Raisi Praygod akajaribu kumshika mkono mke wake kutazama ni nini kinacho msumbua, ila akajikuta mkono wake ukisogezwa kwa nguvu na mke wake huyo hadi akabaki ameduwaa.
Rahab, akashuhudia jinsi shingo ya Samson inavyo kandamizwa kwa nguvu na mtu aliye valia mavazi meupe, baada ya muda kidogo Samson akatulia kimya, ikiashiria tayari amesha yapoteza maisha yake. Rahab akayafumbua macho yake huku akishusha pumzi taratibu, machozi ya uchungu yakaanza kumwagika usoni mwake.
 
“Mke wangu unatatizo gani?”
Raisi Praygod aliuliza huku akiwa na wasiwasi mkubwa, Rahab akatingisha kichwa akidai hakuna tatizo ambalo limejitokeza. Rahab akajifuta damu zilizo kuwa zikimwagika, huku akiamini kwamba safari wanayo iendea haina umuhimu tena kwao. Kwani mtu wanaye mfwata tayaria amesha uawa kinyama, na mtu amabaye hakuiona sura yake.
                                                                                                  ***
Dokta Maliki, alipo hakikisha kwamba tayari amesha muua Samson kwa kuiminya shingo yake, akarudishia kila kitu alicho kitoa kwenye mwili wa Samson, ikiwemo mashine inayo msaidia kuhema. Baada ya mashine hiyo kurudishiwa kwenye mdomo wa Samson, ikaaonyesha mstari  mwekundu ulio nyooka, ukiashiria kwamba mtu huyo tayari amesha poteza maisha. Dokta Maliki akatoka ndani ya chumba hicho.
“Hakikisheni hakuna anaye ingia humu ndani, mgonjwa anahitaji kupumizika”
 
Aliwaambia askari hao ambao hakuna aliye kuwa akifahamu ni kitu gani kinacho endelea, Dokta Maliki akaanza kutembea kwenye kordo ndefu kuelekea nje, na muda huu hakuhitaji kukaa tena hospitalini kwani tayari anatambua ni kitu gani alicho kifanya na endapo atajulikana kama yeye ni muuaji, basi adhabu kali itaambatana naye.
Akiwa katika eneo la maegesho ya magari, gari kadhaa zinazo ashiria zimembeba kiongozi mkubwa zikasimama, ikamlazimu kuangalia ni kiongozi gani ambaye anashuka. Mlango wa gari moja ukafunguliwa akashuka binti mmoja pamoja na jaama ambaye ni mara yake ya kwanza kuiona sura yake
 
“Huyu ni nani?”
Alijuliza, huku akiendelea kumtazama jamaa huyo anaye wekewa ulinzi mkubwa kama kiongozi wa nchi. Macho ya dokta Maliki yakagongana na macho ya Rahab, aliye mtazama kwa muda huku akionekana kama msichana huyo anamtambua Dokta Maliki. Raisi Praygod baada ya kumuona mke wake anamshanga sana dkatari aliye simama kwenye moja ya gari huku akiwa na funguo mkononi, ikambidi amshike mke wake mkono.
 
“Baby twende ndani”
Rahab akaondoka na Raisi Praygod ambaye sura yake halisi imefunikwa na sura bandia ambayo hakuitaji sura yake iweze kuonekana na mtu wa iana yoyote zaidi ya walinzi wake wanao fahamu kwamba ni yeye. Dokta Maliki akiingia ndani ya gari lake na kuondoka katika eneo la hospitali ya Muhimbili huku moyoni mwake akiwa na furaha ya kuweza kukeleza kazi ya kiongozi wake anaye mtumikia.
 
       Raisi Praygod moja kwa moja akapelekwa kwenye chumba alicho lazwa Samson, huku akiwa na mke wake pamoja na daktari mkuu wa zamu, aliye weza kuitambua sauti ya raisi Praygod.
“Samahani dokta. Dokta Maliki ameagiza asiingie mtu ndani ya chumba hichi”
Askari walio achiwa jukumu la kulinda katika chumba hicho waliwazuia Raisi Praygod, Rahab pamoja na daktari huyo wa zamu pasipo kufahamu kwamba huyo wanaye mzuia ndio raisi wao
                                                                                                ***
       Baada ya hali kutulia, kwenye hoteli alkliyo fikizia waziri wa mambo ya nje ya Marekani, mkuu wa askari nchini Russia akiwa ameongozana na vijana wake wawili, wakaelekea sehemu walipo fichwa viongozi hao wawili. Kila mmoja akashikwa na butwaa baada ya kukuta miilii ya walinzi wote ikiwa imezagaa chini huku ni raisi wao akiwa amekaaa kwenye sakhafu huku akiendelea kuugulia maumivu makli ya jeraha la risasi aliyo pigwa.
 
Kwa haraka wakafanya mawasiliano na askari wengine wa markani waliopo nje ya hoteli hiyo wakiendeleza ulinzi. Kuhakikisha kiongozi wao anaye lindwa ndani hapatwi na tatizo lolote. Kitendo cha kukuta kiongozi wao ameua, kila mmlinzi akajikuta akichanganyikiwa, kwani hakuna aliye elewa tukio hilo limefanywa na nani, huku walinzi wote wakuaminika wakiwa wameuwa kikatili.
 
Wakafanya mawasiliano haraka moja kwa moja kwenye ikulu ya Marekani na kutoa taarifa hiyo iliyo wachanganya kuanzia raisi pamoja na jopo lake zima la ulinzi. Uchunguzi wa kina ukaanza kufanyika kwa kina, huku kamera za eneo hilo zikichunguzwa kujaribu kumuona nani ameusika na mauaji hayo. Cha kushangaza kamera zote za eneo lililo tokea maauji, hazikuweza kuonyesha tukio hilo, hapo ndipo wakagundua kuna mchezo ambao umefanyika.
 
(muda mchache kabla ya tukio)
Baada ya Agnes, kushindwa kumuua waziri wa mambo ya nje wa Marekana, akiwa mbali kwenye sehemu walipo jificha, akili ya Anna ikatambua moja kwa moja ikatambua kwamba ni lazima Agnes atashuka na kwenda kutekeleza tukio hilo kwenye hoteli hiyo. Kifaa maalimu kilicho ingizwa mwilini mwa Agnes, kiliweza kumuonyesha kila sehemu anayo kwenda.
Anna akaomba kupewa kazi moja ya kumlinda rafika yake huyo ambaye anaiendea kazi moja ya hatari sana.
“Utamsaidiaje?”
 
Bwana Rusev alizungumza huku akimtazama Anna machoni. Anna akamuomba muendesha mitambo katika chumba hicho walichopo aweze kumpisha kwenye kiti kwani kuna kazi anahitaji kuweza kuifanya. Kwa utaalamu alio kuwa nao Anna, akaanza kucheza na kamera za ulinzi zilizopo kwenye eneo hilo kwa kutumia computer iliyo unganishwa mitambo ya Satelaite, alicho anza kukifanya ni kutafuta namba za siri ambazo zinaongoza kamera zote zilizopo kwenye eneo hilo, kwa bahati nzuri akafanikiwa kuzipata, alicho kifanya ni kuweza kugandisha kila kamera anapo pita Agnes, jambo ambalo halikuweza kustukiwa na wataalamu walipo kwenye chumba maalumu kwenye hoteli hiyo katika kuongoza kameza zaidi ya alfu moja zilizopo katika eneo zima la hoteli. 
 
Tukio la Agnes kumteka kijana mwenye mavazi ya zima moto halikuweza kunaswa na kamera za hoteli, zaidi ya wataalamu hao kunao kila eneo lipo salama kupitia tv zao nyingi zilizomo ndani ya chumba hicho.
 
Agnes anaingia kwenye eneo walilopo viongozi, camera zote ziliweza kugandishwa na Anna, zikawa zinaonyesha uneo hilo likiwa limetulia, kumbe walinzi wanao walinda viongozi wao wapo kwenye wakati mgumu, wakiadamishwa na binti mmoja ila mwenye uwezo mkubwa kupita maelezo.
Hadi Agnes anatoka katika eneo hilo hapakuwa na camera iliyo weza kumnasa sura yake, na hapakuwa na mtu aliye weza kustukila swahala hilo. Watu waliomo ndani ya chumba hicho wakajikuta wakipiga makofi kwani kwa kazi waliyo ifanya mabinti hao, ni kazi kubwa sana yakutumia akili pasipo nguvu nyinngi.
                                                                                             ***
     Mahojiano ya haraka yakafanywa kwa Raisi wa Russia aweze kueleezea muuaji huyo wa kike anaonekana vipi. Huku akiendelea kufanyiwa matibabu na madaktari bingwa. Raisi akaendlea kutoa maelezo jinsi binti huyo anayo onekana. Wataalamu wa kuchora waziadi kuendela kuichora sara ya binti huyo hadi ikakamilika na kupata sura halisi ya Agnes. Picha hiyo kwa haraka ikatuma makao makuu ya ujasusi nchini Marekani Washinton DC. Sura hiyo ikaningizwa kwenye mitambo maalumu ambapo, kwa kutimia satalaite wakaanza kuitafuta ni wapi sura hiyo inapaikana.
“BINGOOOO”
 
Mtaalamu mmoja alizungumza baada ya kumpata msichana huyo ambaye bado anaonekana hajatoka kwenye nchi ya Rusia. Kila kona ya mipika picha ya Agnes ikasambazwa kwa haraka kwa kila askari, vituo vyote vya mabasi, reli, anga pamoja na bandari. Vikaimarishwa ulinzi mkali, huku askari wa kutosha kutoka Marekani, wakihakikisha wanamtia nguvuni binti huyo anaye onekana ni gaidi wa kimataifa.
 
Agnes pasipo kufahamu chochote kinacho endelea, akiamini kwamba kila kitu kipo sawa, akafika kwenye kituo cha treni. Akiwa katika moja ya dirisha la kukatia tiketi za treni, wanajeshi wawili wa kimarekani, wakiwa na mbwa wakasimama mbele yake huku wakimkazia macho, huku mmoja wao akijaribu kuchomoa bastola yake kwa ajili ya kumdhibiti Agnes kwani tayari wamesha mtambua yeye ndio muuaji wa kiongozi wao bwana Paul Henry Jr.
                                                                                     
                                   SHE IS MY WIFE(46)
   
Gafla, wanajeshi hao wawili walio simama, mbele ya Agnes, wakaanguka chini huku wakitoa milio mikali ya maumivu, mbwa walio washika wakatoa milio mmoja na kuanguka nao chini. Hata Agnes mwenyewe akabaki ameduwaa kwania hakujua ni nani aliye weza kulifanya tukio hilo la kuwaangamiza wanajeshi hao walio anza kuvuja damu kwenye miili yao. 

Wananchi walipo karibu wakaanza kupiga makelele huklu wakikimbia kimbia. Makelele hayo yakawafanya askari pamoja na wanajeshi wengine kwenye eneo hilo kukimbilia katika sehemu kelele hizo zinatokea. Agnes akataka kujijichanganaya na wananchi hao, gafla akadakwa mkono wake kwa nyuma, akageuka kwa haraka huku akiwa emerusha ngumi iliyo pita hewani baada ya mtu huyo kuweza kuikwepa kwa kubonyea chini kidogo kwa umakini mkubwa alio kuwa nao aliweza kuiona ngumi hiyo inavyo kuja kwa kasi.
 
     Macho ya Agnes yakakutana na macho ya mtu aliye vaa kinyago, huku sura yake yote ikiwa imefichwa na kinyago hicho cheusi. Mavazi ya mtu huyo yanarangi nyeusi tupu kuanzia chini hadi juu. Mgongoni mwake amechomeka sime ndefu  iliyopo kwenye sehemu yake maalumu.
“Twende huku”
 
Hapo Agnes ndipo aliweza kumtambua mtu huyo ni msichana, hii ni baada ya kumuambia maneno hayo kwa lugha ya kiswahili sahihi. Agnes akataka kusita ila binti huyo akamvuta kwa nguvu, wakanza kukimbia wakikatiza katika kwenye kundi la watu wanao kimbia kimbia pasipo kujielewa.
Kundi la askari wapatao sita wakasimama mbele yao wakiwa na virungu, Binti huyo akamuachia Agnes mkono, kwa kasi ile ile walio kuwa wanakimbia nayo, akajirusha hewani mita nne kwenda juu, huku akijiviringisha kwa sarakasi, akawapita askari hao kwa juu, akatua nyuma yao nakuwafanya askari hao kupagawa. Kila askari aliye jaribu kurusha kirungu, aliweza kukutana na teke zito lililo muangusha chini. Agnes baada ya kuona msichana huyo anamsaidia, naye akawajibika katika kujibu mashambulizi ya ngumi zinazo pigwa na askari hao walio chapika kisaswa sawa kama watoto wadogo.
Ndani ya dakika mbili, hapakuwa na askari aliye weza kusimama, kila mmoaja aliweza kushikilia kiungo alicho weza kuvunjwa.
 
Kwa bahati nzuri, kuna treni inayo kwenda kwa mwendo kasi ikawa imefika katika kituo hicho, abiria wakushuka wakashuka na abiria wakupanda nao wakapanda. Agnes na binti huyo wakajichanganya na kuingia ndani ya treni hiyo, hadi askari wanagundua hilo tayari terni hiyo ilisha anza kuondoka taratibu kwenye kituo hicho. Jambo ambalo liliwawia ugumu askani ni kuisimamisha terni hiyo kwani kwa mujibu na sheria ya treni hizo, hazipaswi kusimama pale zinapo ondoka, kutokana kufanya hivyo kunaweza kusabibisha treni inayo kuja kwenye kitua hicho kuweza kugongana na kusababisha ajali kukbwa na ubaya zaidi treni hizo huwa zinatumia dakika tano tano kukaa kwenye kituo.
 
     Kila abiria aliye waona Agnes na mtu huyo aliye valia ninja na kuificha sura yake, alikaa kimya huku kila mmoja akiwa na woga kwa upande wake, kwani wanaonekana ni watu hatari.
“Hii sio sehemu salama”
Binti huyo alizungumza huku akichungulia nje ya treni kwa kutumia vioo vilivyopo pembeni.
“Kutoka hapa hadi kituo kingine kuna msitu katikati, itatubidi kutoroka la sivyo kituo kinacho fwata nilazima tutakamatwa”
Sauti ya msichana hiyo ni ngeni masikioni mwa Agnes.
“Tunafanyaje sasa?”
“Twende juu”
“Juu…..!!!”
 
Agnes aliuliza huku akiwa amemtumbulia macho binti huyo, kwani mwendo wa treni hiyo ulivyo mkubwa ni hatari sana mtu kufungua hata kioo..
“Ndio twende juu”
Binti huyo alizungumza huku akichomoa jambia lake refu, watu wote waliomo ndani ya behewa hilo wakaka kimya kwani mlio wa kuchomolewa kwake tu, ulimstua kila mmoja. Binti huyo akapiga hatua mbili mbele kutoka katika sehemu alipo simama yeye na Agnes.
“KAMA UNAHITAJI KUISHI TOKA NDANI YA HILI BEHEWA”
Alizungumza kirusi, abiria wote wapatao kumi na tano wakaanza kutafuta ustaarabu wa kuingia katika mabehewa ya mbele au ya nyuma. Ndani ya dakika wakabaki wao wawili tu ndani ya behewa hilo.
 
“Ngoja kwanza wewe ni nani?”
“Hupaswi kunifahamu muda huu”
“Nani aliyeku………….”
Agnes hakuimalizia sentesi yake, jambia hilo linalo meremeta kama kioo, likawa limesimamishwa sentimita chache kutoka shingoni mwake.
“Huwa sipendi maswali ya kipuuzi nikiwa kazini”
Agnes akameza fumba la mate kwani tayari amesha gundua mwanamke mwenzake huyo ana uwezo mkubwa sana kuliko yeye na endapo atajaribu kupimana naye uwezo wa kupigana itakula kwake.
“Fwata nitakacho kuambia”
Alizungumza huku alilishusha chini jambia lake hilo, Agnes akashusha pumzi kubwa kwani shingo yake ingegawanyishwa vibaya.
                                                                                               ***
     Kwa haraka, Rahab akarusha ngumi za kasi zilizo tua shingoni mwa askari mmoja aliye kuwa kiherehere kuwazuia kuingia ndani ya chumba hicho. Mwengine kabla hajafanya chochote Raisi Praygod Makuta akampuka kiwiko cha uso askari huyo nakumfanya mikono yake yote aipeleke usoni mwake kwani giza la gafla liliyafunika macho yake. Rahab akaingia ndani ya chumba huku raisi Praygoda akifwatia kuingia
“Mambo mengine munajitakia wenyewe”
Daktari huyo wa zamu alizungumza huku akimsukumia pembeni askari aliye ufunika uso wake kwa viganja vyake. Dokta baada ya kuingia ndani ya chumba hicho na kukuta mashine ya kupumulia inaonyesha mstari mmoja mwenkundu ikiashiria mgonjwa huyo amefariki, akajikuta amechanganyikiwa.
 
“Si alikuwa hai huyu”
Daktari alizungumza huku akijaribu kumminya Samson kifuani mwake. Rahab akamshika mikono daktari huyo na kumzuia kufanya akacho kifanya
“Tayari ameshakufa ila naomba sindano”
“Sindano………!!!?”
“Ndio sindano”
Daktari huyo akajipapasa pasa kwenye mifuko yake, hakukuta sindano
“Dakika moja”
Akatoka kwa kasi na kuelekea sehemu ambapo anaamimi nanaweza kupata bomba la sindano. Rahab baada ya daktari huyo kutoka, akaufunga mlango kwa ndani na kusimama pembeni ya kitanda alipo simama mumewe.
“Sasa tunafanyaje na mgonjwa amesha kufa?”
 
Raisi Praygod aliuliza huku akiwa amekata kabisa matumaini yakundelea kukaa ndani ya chumba hicho.
“Ngoja nikuonyeshe kitu ila ninaomba iwe siri yako mume wangu”
“Siri? Kitu, kitu gani?”
“Subiri”
Rahab akachomoa bastola yake, akatoa magazine. Kwakutimia ncha ya kali ya chini ya magazine hiyo inayo hifadhia risasi, akajikata kwenye mkono wake wa kushoto sehemu yenye mshipa wa damu.
“Unataka kufanya nini mke wangu!!?”
“Subiri utaona mume wangu”
Rahab akamfunua Samson kinywa chake, akaanza kuyanyunyuzia matone ya damu yake kwenye kinywa cha Samson, baada ya kuridhika kiasi cha damua alicho kiingiza mdomoni mwa Samson kinatosha, akachanan kipande cha shuka, akajifunga sehemu ambayo damu inatoka. Akamsogelea Samson karibu, akampulizia pumzi kiasi Samson. Taratibu vidole vya miguu vya Samson vikaanza kucheza, ikiashiria uhai wake umesha rudi.
 
“Samson, Samson, Samson”
Rahab aliita mara tatu, Samson akayafumbua macho yake, huku macho yake yote yakiwa mekundu sana. Rahab akamkazia macho Samson, kila walivyo zidi kutazamana ndivyo jinsi macho ya Samson yalivyo rudi katika hali yake ya kawaidia. Raisi Praygod Makuya, na ujasiri wake wote akajikuta akitetemeka kwani tangu azaliwe hakuwahi kusikia kama kuna binadamua anaye weza kufufua binadamu mwengine.
 
“Fungu mlango”
Rahab alizungumza kwasauti nzito kidogo, iliyo mfanya Raisi Praygod kukimbilia mlangoni, kitendo cha kuufungua mlango dokta wa zamua akaingia, alipo muona Samson akinyanyuka na kukaa kitako kitandani, akajikuta akidondosha bomba la sindano. Mwili mzima ukamuishia nguvu akaanguka chini na kupoteza fahamu.
“Amezimia tu”
Rahab alizungumza huku akimtazama dokta huyo aliye lala sakafuni.
“ASANTE MADAM RAHAB”
Samson alizungumza kwa sauti nzito kiasi, Rahab akaachia taasamu pana akiamini jaribio lake limefanikiwa.
“Niagize chochote nitafanya Madam Rahab”
Samson aliendelea kuzungumza huku akimtazama Rahab aliye simama mbele yake. 
 
“Twende nyumbani sasa”
Rahab alizungumza. Sasmso akasimama wima akajigeuza geuza akiashiria yupo safi. Rahab akalishika la hospitalini alilo valishwa Samson, akalichana kwa nguvu na akabaki tumbo wazi. Hapakuwa na jeraha lolote mwilini mwa Samson. Raisi Praygod akabaki ameduwaa tuu, kwani kila linalotokea kwenye macho yake ni kama ndoto. Rahab baada ya kumtazama mume wake akagundua yupo kwenye hali ya woga. Akasogelea, akanyonya mate, yaliyo ufanya mwili wa Raisi Praygod kushikwa na kijiubaridi, kilicho utoa woga wote na kurudi katika hali ya kawaidia.
 
“Twende zetu Praygod”
“Sawa”
Wakatoka wakiwa wameongozana na Samson, askari wanao endelea kuugulia maumivu, baada ya kuona mgonjwa waliye amini ni mahututi akitoka anatembea huku akiwa hana hata bandeji moja mwilini wake wala kidonda, wakabaki wakiwa wameduwaa kila mmoja akiwa haamini wanacho kiona.
                                                                                              ***
“Muheshimiwa kazi yako nimesha imaliza”
Dokta Maliki alizungumza kwa kutumia simu yake ya mkononi huku akizidisha mwendo kasi wa gari gari lake.
“Unauhakika kama Samson amefariki?”
Makamu wa raisi alizungumza kwa kufoka sana hadi dokta Maliki akashangaa kwani si kawaidia ya kiongozi wake huyo kuzungumza kwa sauti ya ukali kama hivyo
“Ndio muheshimiwa”
“Pumbavu wewee, mtu hajakufaa unaniletea ujinga unjingaa hapaaa”
Makamu wa raisi alizungumza kwa kufoka, hadi dokta Maliki akajikuta akifunga breki za gafla, na kusimamisha gari lake pembeni ya barabara
 
“HAJAKUFAA……!!!?”
“Fala wewe, unamuuliza nani”
Makamu wa raisi akakata simu. Dokta Maliki akabaki anaishangaa simu yake, kila alvyo jaribu kuvuta kumbukumbu zake, anakumbuka aliweza kumnyonga Samson hadi amefariki, sasa inakuwaje makamu wa raisi aseme Samson yupo hai.
 
Akiwa katika dimbwi la mawazo ujumbe wa meseji kupita whatsapp, ukaingia kwenye simu yake, kwa haraka akaufungua na kukutana na namba ngeni iliyo tuma picha ambayo bado inaendela kusoma kwa ajili ya kufunguka.
“Comen comennnn”
 
Dokta Maliki alizungumza na simu yake hiyo, mara baada ya kuona picha  hiyo inachelewa kufunguka kutokana na mtandao wa internet katika sehemu alipo kuwa ni mdogo. Picha hiyo ikafunguka hapo ndipo dokta Maliki alipo amini kwamba Samson yupo hai. Kwani picha hiyo inamuonyesha Samson akiwa ameongozana na watu watatu ambao alipishana nao mara baada ya kuwaona wakiingia hospitalini.
“Shitiiiiiii Fuc**………..!!!!!”
 
Dokta Maliki alijikuta akipiga mgumi nzito kwenye mskani wake hadi honi ya gari lake ikalia kwa nguvu. Gafla taa za mbele za gari yake zikafifia sana, akaiweka pembeni simu yake kwani kufifi kwa taa za gari yake hiyo mpya aina ya Breves, kilimstua akafungua mkanda wa siti yake, gafla taa zake zikarudi katika hali ya ukawaida, cha kumshangaza zadia mbele ya gari lake amesimama mtu aliye mpa mgongo, jambo lililo mtisha Doktar Maliki. 
 
Akaminya honi zake kwa nguvu ili mtu uyo kuweza kupisha njiani, na mbaya zaidi dokta Maliki aligundua amasimama katikati ya daraja la Sarenda. Kwa haraka akilini mwake akahisi ni majini ambao mara kwa mara inasadikika yanaonekana kwenye daraja hilo. Akawasha gari yake ila haikuwaka akajaribu kuliwasha gari lake ila halikuwaka kabisa. 

Mtu aliye simama mbele ya gari lake taratibu akaanza kugeuka huku sura yake akiwa ameiinamisha chini. Alipo inyanyua sura yake, macho ya Dokta Maliki yakamuona vizuri Samson akiwa amsimama mbele yake, huku akiwa tumbo wazi, mikononi mwake akiwa amshika bastola mbili zilizo elekea chini.

==> ITAENDELEA

No comments:

Powered by Blogger.