Rais Dkt Magufuli afanya uteuzi wa mabalozi Wapya 21
December 03 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa Mabalozi 15 ili kujaza nafasi zilizo wazi katika Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali.Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mabalozi hao wameteuliwa kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika vituo vifuatavyo;Beijing – ChinaParis – UfaransaBrussels – Makao Makuu ya Jumuiya ya Nchi za UlayaMuscat – OmanRome – ItalyNew Delhi – IndiaPretoria – Afrika ya KusiniNairobi – KenyaBrasilia – BrazilMaputo – MsumbijiKinshasa – Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoKampala – UgandaAbuja – NigeriaMoroni – ComoroGeneva – Umoja wa MataifaAidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi 6 kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Balozi mpya 6 ambazo zitafunguliwa hivi karibuni katika nchi za Algeria, Israel, Korea ya Kusini, Sudan, Qatar na Uturuki.Orodha kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;Balozi Mbelwa Brighton KairukiBalozi Samuel W. ShelukindoBalozi Joseph E. SokoineBalozi Silima K. HajiBalozi Abdallah KilimaBalozi Baraka LuvandaBalozi Dkt. James Alex MsekelaBw. Sylvester Mwakinyuke AmbokilePindi ChanaDkt. Emmanuel J. NchimbiRajab Omari LuhwaviLut. Jenerali (Mstaafu) Paul Ignace MellaGrace MgovanoMohamed Said BakariJob MasimaOmar Yusuf MzeeMatilda S. MasukaFatma M. RajabSylvester M. MabumbaProf. Elizabeth KiondoGeorge Madafa (Uteuzi wake ulishatangazwa)Vituo vya kazi vya mabalozi hawa 21 vitatangazwa baadaye. Mabalozi wote waliobaki katika vituo ambavyo si kati ya vituo hivi 15 vilivyotajwa wataendelea na nafasi zao za uwakilishi wa Tanzania katika vituo walivyopo.Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemhamisha Balozi Modest Jonathan Mero kutoka kituo chake cha sasa cha Geneva, kwenda Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (New York) ambako atakuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.Balozi Modest Jonathan Mero anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Tuvako M. Manongi ambaye atastaafu ifikapo tarehe 06 Desemba, 2016.Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi Grace A. Martin kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Itifaki (Chief of Protocal) – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kuanzia leo tarehe 03 Desemba, 2016.Kabla ya uteuzi huo Grace A. Martin alikuwa akikaimu nafasi hiyo. Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Balozi Peter Kallaghe kuwa Afisa Mwandamizi Mwelekezi – Mambo ya Nje katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College)Kabla ya uteuzi huo, Balozi Peter Kallaghe alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza hadi mwanzoni mwa mwaka huu 2016.
No comments:
Post a Comment