Trending News>>

Onyesha furaha mpenzio akufikishapo patamu-acha kununa




Shoga yangu, kabla sijaelezea ‘topiki’ yangu ya leo, napenda kukupa pole kwa kuondokewa na Kapteni John Komba aliyefariki dunia siku ya Jumamosi.
Hakika taifa limepata pigo kubwa sana kuondokewa na kada huyo mkongwe wa CCM aliyekuwa mtunzi na muimbaji mahiri wa nyimbo mbalimbali.Kwa kuwa kazi ya Mola haina makosa, hatuna budi kumshukuru na kumuomba ailaze roho ya marehemu Komba mahali pema peponi, amina.
Leo shoga yangu nataka kuzungumza nawe kuhusu suala la kupiga vigelegele mwenza wako anapokufurahisha mnapokuwa kwenye eneo lenu tulivu ambalo wengine uliita uwanja wa fundi seremala.
Nimekuandalia mada hii ili kuwaweka sawa wenzetu ambao hata wakifurahishwa vipi na waume zao wanapokula ‘msosi’ wa usiku, hutulia tuli kama maji mtungini.
Shoga, kufanya hivyo ni sawa na kupika mboga bila kuweka viungo kwani ni wazi itapooza na kutowavutia walaji ambao watakula ilimradi washibe kisha wakaendelee na pilika zao. Mwanamke unapaswa kuwa mahiri wa sanaa ya malovee na kama ni uzembe ufanye kwenye maeneo mengine lakini linapokuja suala la wewe kuwa na mkuu wa kaya katika dimbwi la mahabati, onesha ubunifu wako wote.
Shoga, mtu asikudanganye, hakuna kitu ambacho wanaume wanakipenda kama wenza wao kutoa mihemko inayochanganyikana na vilio wanapokula chakula cha usiku.Mwanamke anapofanya hivyo, huongeza ‘spidi’ ya baba kumlisha chakula ili ashibe wala asiwaze kwenda kudoea kwa watu wengine au kulalamika kwamba mumewe hampi chakula cha kutosha.
Shoga, kama ulikuwa hulijui hilo na kuishia kununa wakati wa kula chakula cha usiku, hebu anza kutoa mihemko, mlilie mumeo na mnapofikia hatua ya kushiba kwa pamoja piga kigelegele kama siyo vigelegele.
Kufanya hivyo utampa raha mumeo na kujiona chakula anachokupatia unakifurahia, hivyo hatathubutu kwenda kula nje ya nyumba yenu.Hata kama huna kawaida hiyo kwa sababu mashetani yako yapo mbali, hebu igiza kutoa mihemko au kuangua kilio wakati mnapata mlo huo wa usiku unaokuwa maalum kwenu.
Baada ya kila mmoja kushiba, mshukuru mumeo kwa kukupatia chakula kitamu kisichoisha hamu, nakwambia licha kabla ya kulala kula chakula chako mara mbili, alfajiri  atakuamsha na kuomba mshiriki tena kula chakula cha asubuhi ambacho huwa kitamu kupita maelezo.

No comments:

Powered by Blogger.