MWANAMKE JITAMBUE HATA KAMA MMEO NI MKIMYA KIASI GANI.
Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekua umemkosea
nini ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu
wako hautagusa moyo wake....
Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume humfanyii jeuri na kiburi, akinuna na
wewe unanuna asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa yako. Ni mume
wako wa ndoa unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba.
Asipokutafuta mtafute, asipoongea na wewe ongea naye wewe. Hakunaga mke
anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe.
Kunyenyekea hakukugeuzi housegirl na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke, ila
kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana.
Ujeuri weka pembeni!
#ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa zao#
NOTE: Kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu. Panapotakiwa hekima na akili zitumie!
No comments:
Post a Comment