MKUU WA MKOA ALITAKA JIJI LA MBEYA KUKAMILISHA MADARASA KUMI ILI WANAFUNZI 352 WAINGIE KIDATO CHA KWANZA PIA AWATAKA WANANCHI KULINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla
amelitaka jiji la Mbeya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi kukamilisha madarasa 10 ili wanafunzi 352 ambao Matokeo yao yamezuiliwa kutokana na kukosekana kwa vyumba vya madarasa
Hayo ameyasema Leo wakati wa kikao maalum na madiwani, watendaji wa kata na mitaa, wakuu wa idara , wajumbe wa bodi za Shule na wakuu wa Shule wa Shule ambazo zina upungufu wa madarasa
Amewataka kwa pamoja kujielekeza katika kuhakikisha madarasa hayo mapema mwezi januari ili wanafunzi hao waweze kuingia kidato cha kwanza
Ana imani ukamilishaji utawezekana kwakuwa madarasa hayo yapo ktk hatua ya upaauaji na ameshukuru jiji kwa kutoa sh 2.000,000 kwa kila darasa ili kuchangia umaliziaji
Amesema kushindwa kukamilika kwa ujenzi huo ni aibu kwa viongozi , watendaji na yeye mwenyewe hivyo nguvu ya pamoja inahitajika kukamilisha madarasa hayo

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya madiwani wa mbeya sanjari nas meya wa jiji la mbeya.

Mbunge Viti maalum Mkoa wa Mbeya Dkt.Mary Mwanjelwa Akichangia hoja Katika Kikao cha
bodi ya Barabara Mkoa wa Mbeya Ambapo Mkuu Wa Mkoa wa Mbeya Mh.Makalla Awashukia wanaon'goa alama barabarani na wanaoharibu Barabara kwa kuchoma matairi, kuburuza nondo barabarani
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amewataka wananchi kulinda miundombinu ya Barabara Kwani Barabara hizo zimejengwa kwa gharama kubwa
Hayo ameyasema katika kikao cha bodi ya Barabara Mkoa wa Mbeya pamoja na mambo kikao kimejadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Barabara ktk Mkoa wa Mbeya
Amekemea tabia ya baadhi ya wananchi wanaon'goa alama za barabarani na wengine kuharibu Barabara hizo kwa kuchoma matairi huku wengine wakisafirisha nondo na vyuma kwa kuviburuza na kuharibu Barabara
Amewaonya watu wenye tabia za kuharibu miundombinu YA barabara kuacha mara moja tabia hiyo na hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao
Amesema ni jukumu la kila Mwananchi kulinda alama za barabarani na miundombinu ya Barabara isiharibiwe.
Na Mr.Pengo MMG Mbeya.
No comments:
Post a Comment