Mahakama ya Uganda yatoa hati ya kukamatwa Wizkid
Mahakama nchini Uganda imetoa hati ya kukamatwa kwa mwanamuziki Wizkid, baada ya kushindwa kutokea kwenye show nchini humo.
Uhenda Wizkid akakabiliwa na kifungo cha miaka 11 jela baada ya kushindwa kutokea kwenye show wakati alikuwa ameshalipwa pesa zake zote.
Show hiyo ilitakiwa kufanyika Disemba 3 mwaka huu katika mji mkuu wa Uganda, Kampala lakini Wizkid akashinda kutokea baada ya kueleza kuwa alikosa ndege ya kwenda nchini humo kutokea Marekani.
Kampuni iliyomlipa, Face TV, kupitia mwanasheria wake, Fred Muwema, imepata kibali cha kumkamata muimbaji huyo kwa kuchukua dola $60,000 na kushindwa kutokea kwenye show. Gharama zingine walizotoa ni brokerage fee, $5,000 na per die, $3,000 kwa muda ambao Wizkid angekaa Uganda.
Mwandaaji wa show hiyo amepata hasara ya zaidi ya $300,000 kutokana na maandalizi aliyofanya kwenye show hiyo.
Zaidi ya watu 25,000 walikuwa wamenunua tiketi kwaajili ya kuhudhuria show hiyo iliyotakiwa kufanyika jijini Kampala.
No comments:
Post a Comment