Trending News>>

Label ya ‘We The Best’ ya Nigeria ipo tayari kumsaini msanii huyu kutoka Tanzania

Bongofleva inazidi kwenda kimataifa zaidi, nimeipata hii good news inayomhusu msanii kutoka Bongofelavani, Tammy The Baddest ambaye amekaa kwenye Exclusive interview na AyoTV na millardayo.com na ametueleza kuwa yupo kwenye harakati za kusaini mkataba na label ya ‘We the best’ ambayo inawamiliki wasanii kama Harrysong na Skibii kutoka Nigeria.

Tammy amesema label hiyo ilifanya naye mazungumzo tangu December 2015 juu ya uwezekano wa kumsaini kwenye label yao kwani ana vigezo wanavyohitaji kutoka kwa msanii ili waweze kumsaini kwenye label yao.

‘Nilikuwa Nigeria December mwaka jana, nikakutana na label ya ‘We The Best Music’ nikakaa nao na wakasema wamependa muziki wangu, style yangu na mwisho wa siku wakaniambia kuna kitu tumeona kwako, na tunahitaji mtu kama wewe na tulikuwa tunamtafuta mtu kama wewe’ –Tammy

No comments:

Powered by Blogger.