Kichuya, Msuva waingia katika vita kali ligi kuu
Shiza Kichuya (Kushoto), Saimon msuva (Kulia)
Unaweza kusema kuwa sasa vita kali ya ufungaji bora katika msimu huu wa 2016/17 imetangazwa rasmi kati ya vijana wawili wa kitanzania Saimon Msuva na Shiza Kichuya baada ya wote kufikisha mabao 9 katika michezo 16 waliyocheza.
Vijana hawa ambao wote wanacheza nafasi zinazofanana yaani kiungo mshambualiaji wa pembeni (Winga) wanatoka katika vilabu viwili hasimu, ambapo Saimon Msuva anakipiga Yanga, na Shiza Kichuya anakipiga Simba.
Vita hii ya mabao imewekwa hadharani mwishoni mwa wiki baada ya Saimon Msuva kuiongoza Yanga kupata ushindi wa mabao 3-0 huku yeye akipiga mawili na kumfikia Kichuya ambaye katika mchezo wake wa jana ambao Simba ilishinda 2-0 dhidi ya Ndanda hakufunga bao lolote.
Hadi mzunguko wa kwanza unamalizika, Msuva alikuwa na mabao 7 huku Kichuya akiwa na mabao 9, na nafasi ya tatu ilikuwa ikishikiliwa na Amis Tambwe wa Yanga aliyekuwa na mabao 5.
Kwa hivi sasa katika klabu ya Simba, anayemfuatia Kichuya kwa mabao ni Mzamiru Yassin ambaye jana alifunga bao lake la tano.
Wakati kichuya akiwa amejiunga Simba msimu kutokea Mtibwa Sugar ambako alikuwa mfungaji bora wa klabu na hajawahi kuwa katika tatu bora ya wafungaji bora wa ligi, Msuva amekaa Yanga misimu mitatu, na huu ni wa nne, huku akiwa na rekodi ya kuwa mfungaji bora katika msimu mmoja wa ligi.
Je, endapo vijana hawa wakiendeleza vita hii hadi mwisho wa msimu, ni yupi ataibuka shujaa? tusubiri tuone.
No comments:
Post a Comment