Trending News>>

Jangili ajirusha korongoni na kufa papo hapo wakati akikimbia huku akiwa na pingu mikononi


MTUHUMIWA wa ujangili wa kuua tembo aliyekuwa akisakwa na askari wa wanyamapori, amekufa baada ya kutumbukia ndani ya korongo wakati akikimbia kujaribu kutoroka akiwa amefungwa pingu mikononi.


Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuua tembo mmoja katika Kitongoji cha Rwakibaga Kijiji cha Mugaba Kata ya Businde wilayani humu.

Ametajwa kwa jina la Fulbert Dagobart (8), mkazi wa Kitongoji cha Nyakabumbwe Kijiji cha Businde Kata ya Businde wilayani hapa.

Tukio hilo lilitokea juzi ambapo marehemu Dagobart anadaiwa kumuua tembo mmoja pamoja na kumng’oa meno kwa kutumia msumeno wa moto.

Alikamatwa na Polisi wa Kituo Kidogo cha Mabira
na kukabidhiwa kwa Askari wa Kikosi Dhidi Ujangili (KDU) kutoka mkoani Mwanza wakiongozwa na Askari wa Wanyamapori wa kikosi hicho, Paul Mbeya, kwa kushirikiana na watumishi wa Maliasili toka Wilaya ya Karagwe pamoja na Askari Polisi Wilaya ya Kyerwa.

Katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa mtuhumiwa Gobart, ilipatikana bunduki moja aina ya Rifle 404 imyoaaminika kuwa akitumia katika shughuli za ujangili ikiwa imefichwa katika shamba la kahawa.

Baadhi ya wananchi wakizungumza na Nipashe, walisema wamefurahishwa na kazi ya kuwasaka majangili na kuahidi kuwa watatoa ushirikiano.

Kikosi Dhidi Ujangili toka Mwanza kwa kushirikiana na polisi kutoka Wilaya za Karagwe na Kyerwa pamoja na watumishi wa Idara za Maliasili za wilaya hizo, wanaendelea na msako wa maangili waliosalia na kwamba kazi hiyo ni endelevu.

Daktari wa Kituo cha Afya Nkwenda, Jackson Kamugisha, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya Kyerwa, aliufanyia uchunguzi mwili wa mtuhumiwa huyo wa ujangili na kuukabidhi kwa ndugu zake kwa ajili ya maziko nyumbani kwao Kijiji cha Businde wilayani humu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Olomi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Source: Nipashe

No comments:

Powered by Blogger.