CHUKUA DAKIKA ZAKO KIDOGO KUSOMA HUU UJUMBE,UTAJIFUNZA KITU.
"CHUNGA NA CHAUREMBO.."
Miaka iliyopita alimfukuzia mdada wa watu kwa heshima na adabu zote.
Hakusita kumuonyesha tabasam na hakufikiria mara mbili kumwambia neno `nakupenda` `nakuhitaji` na mengine mazuri yapendezayo masikioni na rohoni.
Hakujali muda wake wala pesa mbele ya mwanamke huyo.Kujitoa sadaka ndilo hasa lililoweza kukidhi hali aliyomo,kwani alijitolea kwa kila kitu kihali na mali ilimradi tu amtie nguvuni mdada wa watu,aiteke imani yake na auvumishe upepo wa mahaba upande wake.
Alitumia mvuto wake wa sura,mavazi na pesa kama silaha moto katika mapambano.Vijizawadi vya hapa na pale na mitoko ya huku na kule vilikuwa havikauki.
Mdada wa watu akajua kapata.
Maisha si ndo haya bwana!!
Akamsahau mchumba wake wa muda mrefu Geofrey,aliekuwa anasoma chuo.
Akaipuuzia ahadi yake na maagano aliyoweka kuwa atamsubiri na watakuwa wote mpaka pale atakapofanikiwa kufaulu mtihani wa kupata ajira.
Msichana akaanza kushine,kupendeza na vitunyodo vikapendezesha tabia yake.
Nywele za kubond,kope za bandia,kucha za kuweka,viatu virefu,mikoba ya Louis Vutton,mikufu na hereni ya dhahabu vikahamia upande wake.
Maisha yanataka nini zaidi ya hapo???
Imani na mapenzi yote yakahamia kwa mwanaume huyo.
Akajidanganya kuwa ndiye mkweli na anaefaa,kwanza,anavutia kisura,bila ya kuangalia kuwa anavutia kiroho,pili,ana
vutia kimavazi bila ya kuangalia anavutia kinafsi,tatu anavutia kipesa,bila ya kuangalia anavutia kifikra,na nne anavutia kwa swaga ambazo zinamfanya atembee kifua mbele kwa wanawake wenzake akijivunia,bila ya kuangalia kuwa anavutia kiakili,kimawazo na kimaamuzi.
Macho ya mdada yakafumba,na masikio yakaziba.Hakuelewa kuwa sura hiyohiyo ya huyo mwanaume,pesa na swaga zake zinaweza zikamlaghai mwanamke mwingine yeyote mwenye hulka kama yake,popote pale.
Maisha yakaendelea mbele,Wazungu wanasema life goes on.
Nguvu ya ushawishi wa pesa na mvuto wa yule mwanaume hazikuishia tu kwake,ziliendelea mbele kutafuta na kuwatafuna wanawake wengine kama yeye,silaha zikiwa ni zilezile zilizomuangamiza zikawaangamiza na wengine.
Ubaya alikuja kugundua hilo akiwa kachelewa mno,kwani alikuwa tayari ameshawekwa ndani kama mke.
Heshima na adabu alizokuwa anazitoa yule mwanaume zilipotea,maneno matamu ya `nakupenda` `nakuhitaji` na mengineyo yaligeuka na kuwa `nimekuchoka` na `nakuchukia`.
Alianza kuleta wanawake ndani bila ya hofu,mbele ya mwanamke yuleyule aliyemhusudu miaka iliyopita,kwa kumtunza na kumlea mpaka akapata kiburi chenye afya mbele ya wenzake.
Kilio na uchungu kikawa rafiki mkubwa wa yule mwanamke.Akawa anajifungia chumbani akilia asile wala kunywa.
Urembo wake wote ulipukutika.Hakuwa tena yule mwanamke wa zamani aliyegeuza shingo za watu na kuwatoa mate wakora.Alichoka.
Kama hiyo haitoshi,maisha yalizidi kuwa magumu kupita maelezo pale pesa za mumewe zilipoanza kukata.
Alikuja kugundua kuwa zilikuwa ni pesa za urithi na si za mwanaume kama alivyodanganywa.
Mwanaume alirithishwa baadhi ya miradi na marehemu baba yake,na kufuja kwake hizo rasilimali kwa mambo yasiyo na mana na starehe zisizo na msingi,zilimrudishia umasikini.
Maisha yakawa magumu magumu plus.Mume akajiingiza kwenye biashar ya madawa ya kulevya kumaintain hali na muonekano wake town.Alimlaghai na mkewe akajiingiza katika hizo biashara haramu akiwa kama tester,yani anaejaribu madawa ipate onekana kama ni ya ukwele au lah!....Mwanamke akawa teja.
Siku ikawa haiendi bila ya kupata madawa,naye mume akawa anamtunza kwa kumlisha hayo madawa kwakuwa alikuwa hataki kumpoteza,vilevile alikuwa anataka kumfanya aendelee kuwa teja ili yeye apate mwanya wa kufanya mambo yake bila ya shida,ikiwemo umalaya.
Mwanamke wa watu akakonda na kudhoofika zaidi akabaki skeleton.
Alikuwa anatia huruma na imani alivyokuwa anaonekana akijikuna udenda ukimchirizika.
Alikuwa anatia huruma zaidi pale alipokuwa anakosa madawa kwa kuumwa akiharisha mpaka akipoteza fahamu.
Alikuwa mdhoofu mno na hakutamanika.Kimavazi na kiafya pia.Huruma ya majirani ndiyo iliyomkomboa kwa kumsaidia kumpeleka katika kituo cha kusaidia waathirika wa madawa(REHABILITATION CENTRE) pale mume wake aliposafiri kwenda Pakistan kupeleka madawa.
Ilikuwa ni Mungu tu kwani ilibaki kidogo angekufa kwa wingi wa sumu ya madawa damuni.Shukrani kwa daktari wa kituo aliyemsimamia mpaka akaanza kupata unafuu,na kurudi katika hali ya ubinadamu.Akajichanganyana waathirika wengine wenye unafuu kuendlea kupata somo na kujifunza vitu mbalimbali kupata ujuzi.
Siku moja,wadhamini walikuja katika kituo chao kutoa misaada,ilikuwa ni kampuni moja kubwa ya mawasiliano nchini.Wahusika wote wakaitwa kukutana nao na kuwasalimia.
Kama mzaha,Geofrey naye alikuwa ni miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni hiyo,tena akiwa katika kitengo cha Afisa masoko.
Macho ya mwanamke yule hayakuamini kumuona mchumba wake wa zamani akiwa katika uniform za kampuni ile ya mawasiliano iliyokuja kutoa misaada.
Machozi yalimtoka na alianza kushusha kilio kikali kilichowashangaza wageni.
Aliomba Geofrey amsamehe na warudiane,Geofrey akamwambia,
"nimekusamehe,ila nina mke,samahani!"
Mwanamke wa watu akazirai kwa mshangao.
.
.
Note;Watu wengi wanatabia ya kuficha makucha yao watimize lengo.Wanapofan
ikiwa wanayakunjua,unakuwa umeshachelewa.
USILEWE NA UZURI WA NJE.TULIA,TAFAK
ARI,CHUNGUZA,CHUKUA HATUA.
***************************************
No comments:
Post a Comment