WAZIRI NAPE AMKABIDHI BENDERA MREMBO JULIETH KABETE KUIWAKILISHA NCHI MISS AFRIKA
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amekabidhi bendera ya Taifa kwa mlimbwende Julieth Kabete ambaye ameshiriki Shindano la Miss Tanzania na kufanikiwa kushika namba nne Julietha ambapo anakwenda nchini Nigeria kushiriki shindano ya Afrika, litakalofanyika baadae mwezi huu.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika nchini humo katika jimbo la Cross River, mjini wa Calabar, kuanzia Novemba 14, kilele itakuwa Novemba 26 ambapo kwa heshima iliyopewa mji na jimbo lake, Gavana wa Cross River Profesa Ben Ayade ameongeza zawadi ya gari jipya litakalosafirishwa mpaka nchi husika anayotoka mshindi mbali na zawadi ya dola 5000 atakazozipata.
Akizungumza jana, wakati wa shughuli hiyo, Waziri Nape alisema, wanaimani mrembo huyo aliyechaguliwa kwa kuzingatia vigezo vyote atafanya vizuri kwenye mashindano hayo na kuiwakilisha vema Tanzania.
Nnauye amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha washiriki wa shindano la Miss Tanzania wanapata fursa nyingine na sio kama mshindi akishapatikana wengine wanaachwa, na tukishaongea na waandaji wa shindano hilo na walituhakikishia kuwa watafanya vizuri kuweza kuhakikisha wanaangalia fursa zingine kwa warembo walioshiriki na hivyo tunaamini mrembo huyo anavigezo vyote na atakwenda kufanya vizuri.
Mratibu wa Millen Magese Group (MMG), Matukio Chuma, amesema kuwa, wanamitindo kutoka kwenye shindano hilo wameweza kuendelea kufanya vizuri kupitia Swahili Fashion Week na anaamini kuwa Julieth ataiwakilisha nchi yetu vyema.
Taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli zake ndani na nje ya bara la Afrika, ikiwemo nchini Marekani, Millen Magese amekuwa Kinara, Balozi wa kuheshimika na aliye mfano ndani na nje ya Bara la Afrika.
Shindano hilo la Miss Afrika 2016 ambalo limebeba kauli
mbiu ya Kutunza, Kujali na Kuthamini Uchumi wenye kutoa kipaumbele kwa Mazingira kama nyenzo kwa ajili ya Maendeleo endelevu litashirikisha warembo mbalimbali kutoka nchi za Afrika na Julieth amechaguliwa katika shindano lililoendeshwa na kampuni ya Millen Magese (MMG), inayoshughulika na kusaka vipaji vya warembo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekabidhi bendera ya Taifa kwa mlimbwende Julieth Kabete ambaye ameshiriki Shindano la Miss Tanzania na kufanikiwa kushika namba nne Julietha ambapo anakwenda nchini Nigeria kushiriki shindano ya Afrika, litakalofanyika baadae mwezi huu. Katika picha akiwa pamoja na baadhi ya waandani wa Miss Tanzania Hashim Lundenga na mwakilishi wa Milen Magese Matukio Chuma na mama mzazi wa Julieth.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kabla ya makabidhiano ya bendera kwa mrembo Julieth Kabete (kushoto) anayekwenda nchini nigeria kushiriki shindano la Miss Afrika mapema mapema mwezi huu.
Mwakilishi wa Millen Magese Group (MMG) Matukio Chuma (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari kabla ya makabidhiano ya bendera kwa mrembo Julieth Kabete (kushoto) anayekwenda nchini nigeria kushiriki shindano la Miss Afrika mapema mapema mwezi huu.
Picha na Zainab Nyamka.
No comments:
Post a Comment