TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE YAFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KAMBI MAALUM YA UPASUAJI YA WAGONJWA WA MOYO
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiongea jambo na Dkt. Jayme Bennetts ambaye ni bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia.
Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Godwin Shalau akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tatizo la ugonjwa wa moyo kwa watoto katika mkutano wa waandishi wa Habari . Kulia ni Russell Lee kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa (katikati) akimuonyesha takwimu za upasuaji wa wagonjwa wa moyo Dkt. Jayme Bennetts ambaye ni bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia. Kulia ni Russell Lee kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kumalizika kwa kambi maalum ya siku sita ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo iliyofanywa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia. Kulia ni Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Dk. Godwin Shalau akifuatiwa na Russell Lee kutoka OHI.
Dkt. Jayme Bennetts ambaye ni bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kambi maalum ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo iliyomalizika jana ambapo wagonjwa waliofanyiwa upasuaji ni 17 kati ya hao watoto ni 12 na watu wazima ni watano. Kushoto ni Bingwa wa magonjwa ya moyo Dkt. Peter Kisenge, akifuatiwa na Dkt. Benjamin Bierbach ambaye ni bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto, na kulia ni Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu Bashir Nyangasa.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
No comments:
Post a Comment