Trending News>>

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 41 & 42


Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Agnes akaingia ndani ya choo alicho elekezwa, akavua koti lake dogo alilo livaa kutokana na baridi kali, kisha akavua na gloves nyeusi alizo zivaa. Akaminya kitufe kwenye choo cha kukalia na kuyafanya maji kuweza kuzunguka, ili kumdanganya dada huyo kwamba amemaliza haja yake ya kujisaidia.
 
Kabla hajatoka akasikia mlango ukigongwa, jambo lililo mfanya kujiandaa na kujiweka tayari kwa lolote kisha akamruhusu mtu anaye gonga kuweza kuingia ndani. Akaingia dada mfanyakazi huku akiwa na vifaa vyake, gafla Agnes akampiga ngumi nzito shingoni dada huyo na kumfanya aanguke mzima mzima kama mzoga.

ENDELEA
Akamvuta dada huyo na kumuingiza ndani ya choo. Akatoka ndani ya choo na kuufunga mlango kwa ndani wa kuingilia ofisini hapo, kisha akasimama kwenye moja ya dirisha na kuangalia nje. Kwa bahati nzuri katika sehemu alipo simama anaweza kuona vizuri kwenye mlango wa hotel atakayo ingilia kiongozi huyo, ambapo kumejaa wananchi wengi wakiwa wamejipanga kwa kumpokea kiongozi huyo. Akachukua darubin yake, akatazama kila sehemu ya magorofa ya pembeni ili kuhakikisha usalama wake kama upo. 

Alipo ridhika hakuna walenga shabaha wa serikali ambao mara nyingi hujitegega kwenye magorofa makubwa kama hayo. Akafungua kabki kake na kuanza kuchomoa kipande kimoja baada ya kingine cha silaha yake. Akaanza kuiunga kwa utaalamu mkubwa hadi ikakamilika. Akaweka magazine yenye risasi  ishirini, kisha akafunga kiwambo cha kuzuia sauti.
 
Akasimasa kwenye moja ya sehemu ambapo si rahisi kwa mtu wa nje kuweza kumuona. Saa yake ya mkononi akaiweka vizuri, huku ikionyesha zimesalia dakika kumi kabla ya kiongozi huyo kuweza kufika katika eneno hilo. 
 
“Mmmmmmmm”
Agnes aliguna badaa ya kuanza kuona magari meusi yakianza kusimama katika eneo alipo ielekezea bunduki yake, kwa kutumia lensi iliyopo juu ya bunduki yake, akaona baadhi ya walinzi wa waziri huyo wakishuka kwenye magari hayo aina ya GVC. Walinzi hao wakaendelea kuwa macho huku wakijipanga mstati mmoja kuhakikisha kwamba waziri wao anakuwa salama. Kajasho kembamba kakaanza kumchuruzika Agnes, huku mapigo ya moyo yakinza kumpiga kwa mbali jambo lililo anza kumpa wasiwasi kwani katika kazi kama hiyo mtu hutakiwi kuwa na wasiwasi wa aina yoyote.
 
“Shitiiii!!!!”
Agnes alizungumza huku akitingisha kichwa chake, akijitahidi kutoa wasiwasi mwingi alio kuwa nao. Gari ndefu yene milango sita, ikasimama kwenye zulia jekundu la kuingialia kwenye hoteli hiyo. Walinzi wanne walio valia suti nyeusi wakaufwata mlango wa nyuma wa gari hiyo, mmoja akashika kitasa na kuufungua.
 
Agnes akashuhudia mguu mmoja ukitangulia kutoka kwenye gari hiyo, akatulia kidogo kutazama vizuri. Akamuona kiongozi Bwana Paul Henry Jr, akitoka kwenye gari hilo, huku akizungukwa na askari hao wanne. Mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio Agnes baada ya kumuona mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka kama nane akitoka ndani ya gari hilo, na mtoto huyo anafanana sana na bwana Paul Henry Jr.
Agnes akataka kufyatua risasi ila akajihisi vibaya sana huku pumzi akiihisi inakwenda kumuishia, kila allipo jaribu kuiweka sawa bunduki yake, mikono yote ikamtetemeka, akajikuta akiwa ameduwaa akimtazama mtoo huyo aliye nyanyuliwa na bwana Paul Henry Jr na kumbeba kifuani mwake.
 
Bwana Paul Herny Jr akaendelea kuwasalimia wananchi walijitokeza kumpokea, huku akiwa amembeba mwanaye anaye mpenda kuliko kitu chochote na mara nyingi huwa anapenda kwenda naye kwenye dhiara kubwa kama hii ya hapa nchini Russia.
Mlio wa simu ukamstua Agnes, kwa haraka akachukua ear phone na kuiweka sikioni kisa akaminya kitufe kilichopo kwenye hiyo earphone na kuipokea simu hiyo.
 
“Unafanya nini wewe, muue huyo”
Sauti ya bwana Rusev alisikika kwenye simu hiyo akizungumza kwa kufoka. Agnes hakujibu kitu chochote zaidi ya kuishika bunduki yake vizuri, akayang’ata meno yake kwa nguvu na kuikaza misuli yake, ili kuuzuia wasiwasi mwingi ulio mtawala.
“Uaaaaaa”
Sauti ya bwana Rusev ikaendelea kumshawishi Agnes kufanya tukio alilo tumwa kuweza kulifanya, mshale wa msalaba uliopo kwenye lensi ya bunduki yake, ukatua kichwani bwana Paul Henry Jr, tayari kwa kufyatua risasi.
 
         ***
       Baada ya Raisi Praygod kuondoka, Rahab akaendelea kuitazama picha ya Eddy, iliyopo sebleni. Jambo  lililo mfanya Bi Magret kugundua hilo.
“Muheshimiwa, kuna tatizo kwenye picha ya mwanangu?”
Bi Magret alimuliza Rahab kwa sauti ya chini pasipo mtu mwengine kusikia.
“Naomba tuzungumze”
Rahab alizungumza huku akitoka nje ya jumba hilo, bi Magret akafwa kwa nyuma huku akiwa na wasiwasi na maswali mengi juu ya mwanaye huyo.
“Umesema mwano yupo nje ya nchi?”
 
“Ndio muheshimiwa”
“Nchi gani?”
“Mmmm kusema kweli ni historia ndefu sana,  kwa maana Eddy nilipotezana naye kwa kipindi kirefu sana. Na hadi ninavyo zungumza kwa sasa sijui yupo nchi gani”
“Ila wewe kama mama unatakiwa kutambua kwamba mwanao yupo wapi, isitoshe una mamlaka makubwa sana kwenye hii nchi”
“Kweli ila  hata mimi ninatamani sana kuweza kuwa na mwanagu kwa wakati huu ila ndio hivyo sijapata nafasi hiyo”
Rahab akayafumba macho yake kwa muda huku akilini mwake akiivuta taswira ya picha ya Eddy alipo. Virusi vilivyo ingia mwilini mwa Rahab, vimemfanya kuwa ni binadamu wa tofauti na mwenye uwezo mkubwa sana wa kuweza kujua ni wapi mtu alipo. 

Kitu kilicho weza kutokea baada ya Rahab kunywa sumu na kuwahishwa hospitalini. Uhai wake uliweza kupotea, na uhai unao ongwazwa na virusi hivyo ambavyo hadi sasa hivi havijajulikana jina lake, ukachukua nafasi katika mwili wa Rahab, ambaye Rahab halisi tayari roho yake imesha rudi kwa muumba wa mbigu na ardhi, na aliyepo sasa ni Rahab anaye ongozwa na virusi japo mwili, kumbukumbu na akili yake ni ile ile.
 
“Waoooo mwano ni mzuri sana”
Rahab alizungumza huku akiwa ameyafumba macho yake.
“Anauwezo mkubwa wa kupambana, naona sasa hivi anapambana na magaidi anamuokoa waziri wa marekani na familia yake”
Bi Magret akabaki akiwa ameduwaa akimtazama Rahab machoni asipate kumuelewa ni nini anacho kizungumza kwa wakati huo.
“Mwanao yupo Mexco na kwasasa yupo mikononi mwa wanajeshi wa Marekani fanya uwasiliane na ubalozi wa Marekani hapa Tanzania waweze kumfwatili mwanao. Huo ndio msaada wangu kwako”
Rahab akayafumbua macho yake na kutabasamu kisha akaondoka na kumuacha Bi Magret akimshangaa.
                                                                                               ***
     Raisi Praygod na Thomas wakafika kwenye eneo ambalo, yupo muongoza shuhuli(MC), aliye pewa jukumu la kuongoza ratiba nzima inayo endelea.
“Samahani MC unaitwa pale”
Thomas alimnon’oneza MC huyo ajulikanaye kwa jina la Maulid, mtangazaji wa kituo cha televishion ya Taifa.
 
“Na nani?”
Alizungumza huku maiki yake akiwa ameiweka pembeni, ili sauti isisikike kwa watu walio jumuika katika uwanja huu.
“Wewe nenda tu utamuona”
“Basi ngoja mara moja”
Maulidi alizungumza huku akiitazama karatasi aliyo ishika mkononi mwake, akamtazama mchungaji aliye maliza kufanya sala kisha akaisogeza maiki yake karibu na mdomo wake na kuzungumza.
“Anaye fwata sasa ni shehe mku bwana Seif Suleiman”
Baada ya kumkaribisha kiongozi huyo bwana Maulid akapiga hatua hadi alipo simama Thomas pamoja na mtu ambaye hakuweza kumfahamu mara moja kwamba ni nani. 
 
“Kijana habari yako”
Raisi Praygod alizungumza huku akiivua kofia yake na kumfanya bwana Maulid kustuka kidogo, huku macho yake akiwa amemtumbulia Raisi Praygod Makuya.
“Usiogope kijana, ni mimi”
“Mumuuu….hee heeshim…iwa shikamoo”
Bwana Maulid alibabaika huku akiendelea kutetemeka. Raisi Praygod akaivaa kofia yake na kutazama pende zote za uwanja wa taifa, akawaona jinsi wananchui walivyo furika na sura zao zikiwa zimejawa na huzuni huku wengine wakiwa wanamwagikwa na machozi. Akameza fumba la mate kisha akamtazama bwana Maulid.
 
“Nahitaji maiki yako”
Bwana Maulid akaitoa maiki aliyo ishika pasipo kujishauri mara mbili, akamkabidhi Raisi Praygod Makuya, kisha akasimama pembeni akisubiria kuona ni kitu gani ambacho raisi atakizungumza. Raisi Prargod akanyamaza kimya huku akisikiliza sala anayo ifanya shehe Seif Suleima. Baada ya dakika kumi na tano shehe huyo akamaliza kusali na kutoa risala fupi aliyo iandaa, ambayo iliwahusia watanzania kwa ujumla kuweza kuendelea kufanya ibada kwa bidii kwani kifo kipo kwa kila mmoja na haijalishi uwe kiongozi, tajiri au fukara. 

Uwanja mzima ukakaa kimya huku vilio vya chini chini vikiendelea kwa wamama baadhi walio kusanyika katika uwanja. Kila mmoja akawa anamsubiria MC kuweza kusoma ni nani anaye fwata kutua maneno yamwisho kwa majeneza karibi kumi na sita yaliyo wekwa sehemu maalumu kwa ajili ya kuagwa. 

Baadhi ya waandishi wa habari wa televishion, ikawalazimu kuzielekezea camera zao sehemu alipo simama bwana Maulid, kwani wengi wao walihisi ukimya wake unaweza kutokana na mawaidha aliyo yatoa shehe mkuu. Kila mchukua video akabaki akiwa na kigugumizi, kwani walihisi kama walicho kichukua katika sehemu alipo simama bwana Maulid ni miujiza ambayo hakua aliye ifikiria.
 
Si waachukua kamera tu walio weza kushangaa, bali hata wananchi wanao fwatilia tukio zima kupitia luninga zao za majumbani walibaki wakiwa na mshangaa. Tv kubwa lililopo uwanjani likaionyesha sura ya Raisi Praygod akiwa anamwagikwa na machozi, ya huzuni. Viongozi walio kuwa wamekaa katika sehemu maalumu wakasimama kwa mashangao huku kila mmoja akiwa haamini kitu alicho kiona. Raisi Praygod akajifuta machozi kisha akakohoa kidogo na kuzungumza.
 
“Ndugu wananchi”
Sauti ya Raisi Praygod Makuya ikawafanya watu wote kuamini kwamba wanacho kiono ni kweli, walio na udhaifu wa miili yao, nguvu ziliwaishia na kuanguka chini na kupoteza fahamu. Wengine wakachia matabasamu pana kwenye mioyo yao, wakifurahi uwepo wa kiongozi wao waliye mpenda yu ngali hai. Hali ikawa toauti kwa makamu wa raisi, hasira kali ikamkamata na kumnong’oneza mlinzi wake atoe amri kwa askari raisi Praygod Makuya akamate mara moja.
                                                                                         
                                    SHE IS MY WIFE(42)

“Ni huzuni kubwa kwa kila mmoja aliye weza kukusanyika katika uwanja huu kuweza kuiaga miili ya wapendwa wetu”
Raisi Praygod Makuya alizungumza huku akipiga hatua kwenda katika jukwaa lililopo katikati ya uwanja. Askari walio tumwa na makamu wa raisi wakafika hadi sehemu alipo Raisi Praygod Makuya. Badala ya kufanya walicho agizwa na makamu huyo, waliamua kumzingira Raisi Praygod Makuya na kuimarisha ulinzi wake, ili bada lisiweze kutokea. Raisi Praygod akapanda kwenye jukwaa hilo, akatazama kila kila upande wa uwanja na kuona jinsi wananchi walivyo katika hali ya mshangao mkubwa.
“Ndugu wananchi, ni stori ndefu iliyo weza kunikuta mimi kama kiongozi wenu, na nitumie fursa hii kuweza kuwasimulia kabla sijaendelea na mambo mengine”
 
         ***
Agnes kila alipo mtazama mtoto mzuri wa bwana Paul Henry Jr, roho ya huruma ikamtawala, akaona  hakuna haja ya yeye kuweza kufanya mauaji kwa kiongozi huyo ambaye bado upendo wake unahitajika kwa mtoto wake huyo. Agnes akaiweka bunduki yake chini, akamtazama bwana Paul Henry Jr, jinsi anavyo malizia kuagana na wananchi kisha akaingia ndani ya hotel hiyo huku walinzi wake wakiendelea kuimarisha ulinzi.
“Agnes ni nini umefanya?”
Bwana Rusev alizungumza kwa sauti ya upole, iliyo jaa msisitizo mkubwa.
“Target ilikaa vibaya muheshimiwa, ila nipe dakika kadhaa nitafanya”
 
“Una dakika kumi kuweza kulitekeleza hilo”
“Sawa muheshimiwa”
Agnes akavua kifaa cha mawasiliano alicho kichomeka kwenye sikio lake, kisha akaingia chooni na kumkuta dada mfanya usafi akiwa bado hajielewi. Akaanza kumvua nguo zake zote kisha naye akavua za kwake na kuzivaa nguo  za dada huyo. 
 
Akajitazama vizuri kwenye kioo na kuona anafananiana na wafanya usafi katika ofisi hizo. Akaziweka nywele zake ndefu mgongoni, kisha akatoka na kusimama kwenye dirisha akatizama nje kwenye gorofa la Hotel alipo fikizia kiongozi huyo. Hakuona kitu chochote kinacho endelea zaidi ya wananchi wali kusanyika wakianza kutoka mmoja baada ya mwengine. Akaichukua bunduki yake na kuishika vizuri, akayatazama magari magari baadhi yaliyo simama nje ya hotel hiyo. 
 
Akafyatua risasi moja kwenye tank la moja ya gari na kulifanya lilipuke. Wananchi wakanza kutawanyika kuyaokoa maisha yao, magari yaliyo pembeni nayo yakaanza kulipuka baada ya kukutwa na moto wa gari hilo lakwanza. Agnes akaichangua bunduki yake kisha akairudisha kwenye kibegi chake, akakibeba mdongoni na kutoka kwenye ofisi hiyo.
 
Askari wakuimarisha ulinzi wakanza kuchanganyikiwa kwani hawakujua mlipuko huo umesabishwa na nini. Agnes akaingia kwenye lifti na kushika hadi chini. Akataka kwenye goroafa hilo, akakutana na wananchi wengie wakijaribu kuyaokoa maisha yao. Akaanza kukimbia kuelekea kwenye hoteli hiyo, huku akiwa makini akitazama kila kona walipo askari.
 
Mlipuko wamagari, ukawafanya askari wote wanao mlinda bwana Paul Henry Jr pamoja na raisi wan chi hiyo wawazunguke viongozi wao na kuwawekea ulinzi ulio imara ziaid huku kila mmoja bunduki yake ikiwa mkononi, kwani hali ya hatari tayari ilisha jitokeza nje ya Hotel. Moja kwa moja wakawaingiza kwenye moja ya chumba ambacho kimetengenezwa maalumu kwa ajili dharura, kama hizo. Chumba hicho kuta zake, milango na madirisha hayaingizi risasi ya aina yoyote.
 
“Waheshimiwa mupo salama humu ndani”
Mkuu wa ulinzi aliwaambia viongozi hao, walio tawaliwa na wasiwasi mkubwa. Agnes akafanikiwa kufika kwenye mlango wakuingia kwenye hotel hiyo, ambapo askari wakawaida walisimama mlangoni wakizuia wananchi wasiweze kuingia ndani ya mlango huo, kwani hawakujua ni nani mbaya aliye sababisha tukio hilo. 

Agnes akatazama gari zipatazao nne za zima moto zikiwa zimesimama kwenye eneo hilo wakijitahidi kuzima moto wa magari hayo. Akakimbia hadi sehemu yalipo, akazunguka nyuma ya moja ya gari na kumkuta kijana mmoja, zima moto akiwa amechuchumaa akiunganisha moja ya bomba lililo lete itilafu
 
“Miss……”
Kijana huyo hakumalizia sentesi yake, tayari teke zito lilitua kwenye shingo yake na kumlaza kwenye barabara. Agnes akatazama kila kona, hakuona mtu aliye weza kumfwatilia. Kwa haraka akamvua kijana huyo mavazi yake kisha akavaa juu ya nguo alizo zivaa.

 Akavaa likofia la kijana huyo, ambalo lina  kioo mbele. Alipo jihakikisha anafanania na zima moto wengine, akasukumia kijana huyo aliye muacha na boxer chini ya gari hilo. Alicho kifanya ni kuchukua kisu kidogo kwenye kabegi kake kisha akakaingiza kwenye mfuko wa jinguo hilo alilo livaa. 

Akawaona baadhi ya zima moto wakiingia kwenye mlango wa Hoteli hiyo, kibegi kake akakirusha juu ya gari hilo, kisha akachukua kiboksi kidogo cha chuma, ndani chenye vifaa maalumu kwa kazi hiyo ya zima moto. Akakimbilia hadi kwenye mlango  wa kuingilia kwenye hotel, pasipo kustukiwa akaingia ndani ya  Hotel hiyo. Kutokana maelekezo yote alisha yapata kwa mkuu wake bwana Rusev aliweza kulijua eneo zima la Hotel hiyo, kazi aliyo anza kuifanya ni kumtafuta ni wapi alipo Bwana Paul Henry Jr.
                                                                                         ***
Rahab akamchukua mbwa wake, na kuomba chumba ambacho anahitaji kupumzika, akapelekwa kwenye chumba chawageni. Akakichunguza chumba kizima, alipo hakikisha kipo salama akajitupa kitandani huku akiwa amembema mbwa wake.
 
“Heii mamy nataka kupumzika, lala eheee”
Rahab aliuzungumza huku akiwa amembeba mbwa wake na kumlaza kifuani mwake. Akakabembeleza kambwa kake hadi kalala. Alipo hakikisha kamelala, akajaribu kuyafumba macho yake, ila sura ya Eddy ikamjia machoni mwake. Moyo wake ukajikuta ukiwa katika shinikozo kubwa la kuhitaji kukutana na Eddy, ila kwawakati alio kuwa nao ni ngumu sana, kwani tayari amesha kuwa mke wa mtu anaye heshimiwa kupita watu wote nchini Tanzania
“Nitahakikisha unakuwa wangu, maisha yangu yote”
Rahab alizungumza kuku akiachia tabasamu pana usoni mwake, na akilini mwake mume wake alianza kupotea taratibu taratibu.
                                                                                           ***
Makamu wa raisi akawatumbulia macho askari alio waagiza kufanya kazi ya kumkamata Raisi Praygod, mapigo ya moyo yakamuenda mbio baada ya kuwaona askari hao wakiimarisha ulinzi wa Raisi Praygod Makuya, na wasifanya kile alicho waagiza.
 
“Pumbavu……”
Alitoa maneno hayo huku akikaa kwenye kiti chake na macho yake akimtazama raisi Praygod Makuya jinsi anavyo waadisia wananchi mambo yote yaliyo toke kwenye ndege hadi alipo pata msaada wa mke wake wa sasa ambaye ni Rahab. Wananchi walio adisiwa stori hiyo  ya kusisimua, machozi yafuraha yaliwamwagika kila mmoja akajawa na furaha ya kiongozi wao huyo waliye mpenda na kumuona kwamba yupo hai na katika hali ya furaha.
 
“Leo nimezidi kuamini kwamba munanipenda sana, na kuuthamini mchango wangu kwenye maisha yetu yakila siku”
Raisi Praygod Makuya alizungumza huku akiunyanyua mkono wake wakulia  kuwasalimia wananchi wote jambo lililo nyanyua shangwe na nderemo kwenye uwanja mzima wa taifa. Shangwe na nderemo zilivyo zidi kuendelea, mtu mmoja aliye valia  kofia na nguo nyeusi kama waaombolezaji wengine, alifanikiwa kuruka fensi za kuingilia uwanjani  na kuanza kukimbia kuelekea alipo Raisi Praygod Makuya huku akimtaja jina lake.
“Muheshimiwa Praygod Makuya, Muheshimiwa Praygod Makuya”
Askari walio na bunduki wakamuwahi kumdaka kijana huyo na kumuangusha chini. Wakampiga pingu za mikononi.
 
“Muacheni tafadhali”
Raisi Praygod Makuya alizungumza na kuwafanya askari hao kumuachia na kuifungua pingo ya mikono mwake, kijana huyo akakimbilia hadi kwenye jukwaa kisha akaivua kofia yake, ndevu nyingi zilizo tanda kwenye sura yake, zilimfanya kuonekana kama mzee wamiaka stini na kitu, kumbe nikijana mdogo mwenye miaka ishirini na saba.
 
Kwanza kijana huyo akamkumbatia raisi Praygod Makuya, nakumfanya raisi Praygod Makuya kujitahidi kuvuta kumbukumbu zake niwapi alipo muona kijana huyu anaye mwagikwa na machozi. Kumbukumbu za raisi Praygod Makuya zikagota kwenye ndege na kukumbuka kijana huyu ndio yule aliye kuwa akishirikiana na Rahab.
 
“We…weee si…”
Raisi Praygod alizungumza kwa kigugumizi, kwani kama kijana huyu alimkosa kwenye ndege basi leo amekuja kumuua kwenye alaiki ya watanzania.
“Samson, Samson muheshimiwa.”
Samson alizungumza huku machozi ya uchungu yakimwagika, akazidi kumkumbatia Raisi Praygod Makuya kwa nguvu zake zote.

==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia MANYAMAJR

No comments:

Powered by Blogger.