Trending News>>

Polisi asakwa akidaiwa kumpiga polisi mwenzake hadi kumuua


JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga linamsaka askari wa jeshi hilo, Michael Komba kwa tuhuma za kumpiga askari mwenzake wa kike hadi kumsababishia kifo.


Taarifa zilizothibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, David Mngambugha, zinamtaja marehemu kuwa ni polisi Elizabeth Stefano wa Kituo cha Polisi Kati, Chumbageni, jijini Tanga.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 9:00 usiku wa kuamkia juzi, eneo la Sahare jijini Tanga ambako ni nyumbani kwa marehemu.

Wakizungumza na Nipashe kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, baadhi ya majirani walidai kuwa chanzo cha ugomvi huo kinadhaniwa kuwa ni wivu wa mapenzi, wakidai kwamba Kombo alikuwa akimtuhumu Elizabeth kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao.

Source: Nipashe

No comments:

Powered by Blogger.