Trending News>>

NSSF YAWAONDOA WAPANGAJI WALIOSHINDWA KULIPA KATIKA NYUMBA ZA MTONI KIJICHI, DAR ES SALAAM


Vyombo vya baadhi ya wakazi wa nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam vikitolewa nje baada ya wamiliki wa nyumba kushindwa kulipia nyumba hizo kwa mujibu mikataba waliyokubaliana na Shirika hilo. (Picha na Francis Dande).
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendelea na kazi ya kuwaondoa wadaiwa sugu ambao wlinunua nyumba na kushindwa kulipa deni lililobaki kwa muda uliopangwa.
Akizungumza jjijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Radhia Tambwe, alisema kwamba nyumba hizo ni za Mtoni Kijichi jijini Dar es salaam ambapo alisema kwamba kazi hiyo itafanyika kwa wadaiwa  saba.
“Wakazi wa nyumba zote hizo walitolewa na kampuni ya udalali ya Majembe Action Mart kwa kushirikiana na NSSF,”alisema.
Aidha alisema kwamba wadaiwa hao waliondolewa katika nyumba hizo baada ya taratibu za kisheria kufuatwa hivyo nyumba hizo zitauzwa kwa watu wengine.
Aidha alisema kwamba kazi hiyo ni endelevu kwa wale watakaoshindwa kulipa madeni yao kama mikataba inavyosema.
Shirika la NSSF limewataka walionunua ama kupanga nyumba kulipa kwa mujibu wa mikataba yao ili kuepuka adha ya kutolewa vyombo vyao nje na kupata hasara.

No comments:

Powered by Blogger.