Trending News>>

KUTANA NA MTANGAZAJI WA KWANZA MWENYE VAZI LA HIJAB CANADA

Kwa mara ya kwanza mtangazaji wa kike mwenye vazi la hijab ataruhusiwa kutangaza habari kwenye kituo cha televisheni nchini Canada.

Mtangazaji wa kwanza mwenye vazi la hijab Canada

Ginella Massa ambaye ni mwanahabari wa kike wa Canada mwenye asili ya Panama na anayejitanda hijab, aliarifu kwamba atakuwa akisoma habari za usiku katika kituo cha televisheni ya CityNews.

Massa alitoa tangazo hilo kupitia ujumbe aliousambaza kwa kutumia akaunti yake ya mtandao wa jamii wa Facebook.

Massa pia alifahamisha kuridhishwa na uamuzi huo kwa kuwa hapo awali hakukutokea mwanamke yeyote wa hijab aliyewahi kutangaza habari.

No comments:

Powered by Blogger.