Trending News>>

KABETE KUPEPERUSHA BENDERA KESHO MISS AFRIKA 2016



Julieth Kabete

MWAKILISHI wa Tanzania katika shindano la Miss Afrika mwaka 2016,  Julitha Kabete, kesho Jumamosi  atapanda jukwaani moja na washiriki wenzake 18 kuwania taji la mrembo wa michuano hiyo linalofanyika nchini Nigeria.

Mashindano haya yatakayofanyika nchini Nigeria, jimbo la Cross River, mjini Calabar mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajipatia kitita cha dola za Kimarekani 25,000 ni sawa na sh.milioni 52 ya Tanzania na pamoja na gari jipya.

Mshindi  wa pili katika shindano hilo atapata kitita cha dola ya Kmarekani 15,000  ni sawa na sh.milioni 33 za Kitanzania na wa tatu  dola 10,000 ni sawa na sh.milioni 22. Mshiriki huyo amesema kikubwa ni Watanzania wenzake kumuombea dua ili aweze kupeperusha bendera ya nchi yetu na kuweza kushinda taji hilo.

Kabete amesema kuna upinzani mkali, lakini nae kwa upande wake anajiamini anauwezo mkubwa wa kufanya vizuri na kubeba taji la shindano hilo, "Nina nafasi ya kufanya vizuri, kikubwa naomba dua zetu Watanzania wenzangu, niweze kufaya vizuri na kubeba taji".

Mrembo huo ameenda kushiriki shindano hilo akiwa chini ya kampuni ya Millen Magese  Group (MMG),  inayoongozwa na mkurugenzi mtendaji Happiness 'Millen' Magese, anayefanya shughuli zake za mitindo nchini Marekani.

No comments:

Powered by Blogger.