Yanga, Simba katika ubora wao
Pengine ni ubora wa safu ya ulinzi ya Simba au ubutu wa washambuliaji wa timu pinzani Ligi Kuu. Hivyo, ndivyo unaweza kuelezea rekodi ya klabu ya Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam kuruhusu mabao manne msimu huu katika mechi 12, ingawa watani zao, Yanga nao wamejiwekea rekodi ya kuvuna mabao 27, yakiwamo 15 kwenye mechi tano zilizopita.
Kimichezo, Simba imemaliza mechi tano bila nyavu zake kuguswa, jambo linampagawisha kocha wake, Joseph Omog ambaye amefichua kuwa siri ya kiwango hicho bora zaidi klabuni hapo.
Msimu huu, Simba haijapoteza mchezo, imeruhusu mabao manne kwenye mechi dhidi ya Ndanda, Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar na Yanga, kiasi kwamba imecheza mechi tano, sawa na dakika 450 bila nyavu zake kutikiswa.
Mechi ya mwisho kwa Simba kuruhusu bao ilikuwa siku 30 zilizopita dhidi ya Yanga, Oktoba Mosi ilipopata sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na baada ya hapo imecheza dhidi ya Mbeya City, Kagera Sugar, Mbao FC, Toto Africans na Mwadui FC bila nyavu zake kuguswa, hivyo kuifuta rekodi ya Yanga ya kucheza mechi nne, sawa na dakika 360 bila kuruhusu bao mwanzoni mwa msimu huu.

No comments:
Post a Comment