Trending News>>

Vigogo 3 wa TPA akiwemo aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TPA na mfanyabiashara 1 wapandishwa kizimbani.


Tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru), imewapandisha kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu vigogo wanne akiwemo aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya DB Sharpiya and Company Ltd, Kishor Shapriya wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kuomba rushwa ya dola za Marekani 4 milioni zaidi shilingi bilioninane ili watoe tenda ya ujenzi wa bomba la kupakulia mafuta.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba, wakili wa serikali, Emmanuel Jacob kwa kushirikiana na wakili wa serikali mkuu, Mutalemwa Kishenyi wamesema washtakiwa hao walifanya makosa hayo kati ya mwaka 2009 na 2012.

Ambapo mshtakiwa Ephraim akiwa mkurugenzi mtendaji wa TPA, bakari kilo akiwa mkurugenzi wa uhandisi TPA na Theophil Kimaro akiwa meneja wa manunuzi TPA kwa pamoja na kwa nafasi zao waliomba rushwa kupitia kampuni ya DB Sharpiya and Company Ltd   kama kishawishi ili kuwezesha kampuni kupata tenda katika uwekezaji wa bomba la kupakulia mafuta katika ras ya mamlaka ya bandari ya  mjimwema.

Katika kosa la pili, linamkabili Shapriya pekee ambapo anashtakiwa katika tarehe tofauti kati mwaka 2008 na 2009 akiwa kama mkurugenzi wa DB Shapriya alitoa rushwa ya dola za Marekani milioni nne kwa vigogo hao ikiwa ni kishawishi wakuiwezesha kampuni ya Leighton Offoshore pte kupata zabuni ya ujenzi wa bomba la kupakulia mafuta kwenye rasi ya mji mwema ya TPA.

Washtakiwa wote wamekana mashtaka dhidi yao na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika, washtakiwa wameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana kwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja amesaini bondi ya sh milioni 500, na kusalimisha hati zao za kusafiria mahakamani hapo na waliyakamilisha.

Kesi imeahirishwa hadi Novemba 7,2016.

No comments:

Powered by Blogger.